Yesu, mwana wa Maryamu (sehemu ya 4 kati ya 5): Je, ni Kweli Yesu Alikufa?

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Makala hii inaelezea imani ya Waislamu kuhusu Isa na kusulubiwa. Pia inakanusha dhana ya uhitaji wa ‘dhabihu’ ili kulipia dhambi ya asili kwa niaba ya wanadamu.

  • Na Aisha Stacey (© 2008 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 09 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 4,318 (wastani wa kila siku: 4)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Wazo la Yesu kufa msalabani ni msingi wa imani ya Kikristo. Inawakilisha kusadiki kwamba Yesu alikufa kwa ajili ya madhambi ya wanadamu. Kusulubiwa kwa Yesu ni fundisho muhimu katika Ukristo; hata hivyo Waislamu wanaikataa kabisa. Kabla ya kueleza kile ambacho Waislamu wanaamini kuhusu kusulubiwa kwa Yesu, ni muhimu kuelewa hoja ya Kiislamu ya dhana ya dhambi ya asili.

Adam na Hawa walipokula tunda la mti waliokatazwa peponi, hawakushawishiwa na nyoka. Shetani ndiye aliyewahadaa na kuwarai, wakatumia hiari yao na kufanya uamuzi wa makosa. Hawa hakubeba mzigo wa kosa hili peke yake. Kwa pamoja, Adam na Hawa walitambua kuwa kutotii kwao, wakajuta na kumwomba Mungu awasamehe. Mungu, kwa huruma yake zisizo na kifani na hekima yake isiyo na kikomo, aliwasamehe. Uislamu hauna dhana ya dhambi ya asili; kila mtu atawajibika kwa matendo yake.

“Na mbebaji habebi mzigo wa mwingine...” (Kurani 35:18)

Hakuna haja ya Mwenyezi Mungu, mwana wa Mungu, au hata Mtume wa Mwenyezi Mungu kujitoa muhanga kwa ajili ya madhambi ya wanadamu ili awasamahe. Uislamu unakataa katakata mtazamo huu. Msingi wa Uislamu umejikita katika kujua kwa yakini kwamba hakuna apasaye kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu pekee. Msamaha unatoka kwa Mungu Mmoja wa Kweli; kwa hiyo, mtu anapoomba msamaha, ni lazima amgeukie Mungu kwa unyenyekevu na majuto ya kweli na kuomba msamaha, akiahidi kutorudia dhambi hilo. Hapo ndipo tu madhambi yatasamehewa.

Katika mwanga wa ufahamu wa Uislamu wa dhambi ya asili na msamaha, tunaweza kuona kwamba Uislamu unafundisha kwamba Yesu hakuja kufidia madhambi ya wanadamu; badala yake, lengo lake lilikuwa ni kuthibitisha ujumbe wa Mitume kabla yake.

“...Na hakuna mungu ila Mwenyezi Mungu tu...” (Kurani 3:62)

Waislamu hawaamini kusulubiwa kwa Yesu, wala hawaamini kwamba alikufa.

Kusulubiwa

Ujumbe wa Yesu ulikataliwa na wengi wa Waisraeli na vilevile wenye mamlaka Waroma. Wale walioamini waliunda kikundi kidogo cha wafuasi karibu naye, kilichojulikana kama wanafunzi. Waisraeli walipanga njama dhidi ya Yesu na kupanga mpango wa kuuliwa. Alipaswa kuuawa hadharani, kwa namna ya kutisha sana, inayojulikana sana katika Milki ya Roma: kusulubiwa.

Kusulubiwa kulizingatiwa kuwa njia ya aibu ya kufa, na "raia" wa Milki ya Kirumi walipewa udhuru wa kutopata adhabu hii. Iliundwa sio tu kuongeza muda wa uchungu wa kifo, lakini kukeketa mwili. Waisraeli walipanga kifo hiki cha kufedhehesha kwa ajili ya Masihi wao - Yesu, mjumbe wa Mungu. Mungu kwa huruma yake isiyo na kikomo alizuia tukio hili la kuchukiza kwa kuweka mfanano wa Yesu kwa mtu mwingine na kumpaisha Yesu akiwa hai, mwili na roho, hadi mbinguni. Kurani iko kimya kuhusu maelezo kamili ya mtu huyu alikuwa nani, lakini tunajua na tunaamini kwa uhakika kwamba hakuwa Mtume Yesu.

Waislamu wanaamini kwamba Kurani na hadithi sahihi za Mtume Muhammad zina elimu zote zinazohitajika na mwanadamu ili kuabudu na kuishi kulingana na amri za Mwenyezi Mungu. Kwa hivyo, ikiwa maelezo mafupi hayajafafanuliwa, ni kwa sababu Mungu kwa hekima Yake isiyo na kikomo amehukumu maelezo hayo kuwa hayana faida kwetu. Kurani inaeleza, kwa maneno ya Mungu mwenyewe, njama dhidi ya Yesu na mpango Wake wa kuwashinda Waisraeli na kumwinua Yesu mbinguni.

“Na makafiri walipanga mipango na Mwenyezi Mungu akapanga mipango, na Mwenyezi Mungu ndiye mbora wa wenye kupanga.” (Kurani 3:54)

“Na kwa kusema kwao: "Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu." Lakini hawakumuuwa wala hawakumsulubu, bali walifananishiwa tu. Na hakika waliokhitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi wowote nayo, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini.” (Kurani 4:157-158)

Isa Hakufa

Waisraeli na watawala wa Kirumi hawakuweza kumdhuru Yesu. Mungu anasema waziwazi kwamba alimchukua Yesu hadi kwake na kumwondolea taarifa za uongo zilizotolewa kwa jina la Yesu.

“...Ewe Isa! Mimi nitakufisha, na nitakunyanyua kwangu, na nitakutakasa na wale waliokufuru...” (Kurani 3:55)

Katika aya iliyotangulia, Mungu aliposema “atampaisha” Yesu, anatumia neno mutawaffeeka. Bila ufahamu wa wazi wa utajiri wa lugha ya Kiarabu, na ujuzi wa viwango vya maana katika maneno mengi, kuna uwezekano wa kutoelewa alichomaananisha Mungu. Katika lugha ya Kiarabu leo, ​​neno mutawaffeeka mara nyingine hutumiwa kuashiria kifo, au hata kulala. Katika aya hii ya Kurani, hata hivyo, maana ya asili imetumika na ufahamu wa neno hili unaashiria kwamba Mungu alimnyanyua Yesu kwake, kikamilifu. Kwa hivyo, alikuwa hai wakati wa kupaa kwake, mwili na roho, bila jeraha au kasoro yoyote.

Waislamu wanaamini kwamba Yesu hajafa, na kwamba atarudi katika ulimwengu huu katika siku za mwisho kabla ya Siku ya Hukumu. Mtume Muhammad aliwaambia masahaba zake:

“Mtakuwaje atakapoteremka Isa miongoni mwenu na atawahukumu watu kwa Sheria ya Kurani na sio kwa sheria ya Injili. (Saheeh Al-Bukhari)

Mungu anatukumbusha katika Kurani kuwa Siku ya Kiyama ni siku ambayo hatuwezi kuikwepa na anatutahadharisha kuwa kushuka kwa Yesu ni dalili ya ukaribu wake.

“Na kwa hakika yeye ni alama ya Saa ya Kiyama. Basi usiitilie shaka, na nifuateni. Hii ndiyo njia Iliyonyooka.” (Kurani 43:61)

Kwa hiyo, imani ya Kiislamu kuhusu kusulubiwa na kifo cha Yesu iko wazi. Kulikuwa na njama ya kumsulubisha Yesu lakini haikufanikiwa; Yesu hakufa, bali alipaa mbinguni. Katika siku za mwisho kuelekea Siku ya Hukumu, Yesu atarudi katika ulimwengu huu na kuendeleza ujumbe wake.

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.