Maswali Makuu (sehemu 3 kati ya 3): Umuhimu wa Ufunuo
Maelezo: Majibu ya Kiislamu kwa swali la tatu kati ya baadhi ya “Maswali Makuu” ambayo wanadamu wote bila shaka hujiuliza, Tunawezaje kumtumikia Muumba wetu?
- Na Laurence B. Brown, MD
- Iliyochapishwa mnamo 24 Jan 2022
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,041 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Katika sehemu mbili zilizopita za mfululizo huu, tulijibu “maswali makuu” mawili. Ni nani aliyetuumba? Mungu. Kwa nini tuko hapa? Ili kumwabudu Yeye na kumtumikia. Swali la tatu kwa kawaida linakuja: “Kama Muumba wetu alituumba ili tumtumikie na kumwabudu, tutafanyaje hivyo?” Katika makala iliyotangulia nilipendekeza kwamba njia pekee tunayoweza kumtumikia Muumba wetu ni katika kutii amriYake, kama ilivyotajwa kwenye ufunuo.
Lakini watu wengi watajiuliza yafuatayo kuhusiana na hilo: Kwa nini wanadamu wanahitaji ufunuo? Je, haitoshi tu kuwa mzuri? Je! Haitoshi kila mmoja wetu amwabudu Mungu kwa njia yake mwenyewe?
Kuhusiana na umuhimu wa ufunuo, napenda kutaja yafuatayo: Katika makala ya kwanza ya mfululizo huu nilibainisha kuwa maisha yamejaa dhuluma, lakini Muumba wetu ni wa haki na huweka haki yake si katika maisha haya, bali katika maisha ya baadaye. Hata hivyo, haki haiwezi kuwekwa bila vitu vinne—mahakama (yaani, Siku ya Hukumu); hakimu (yaani, Muumba); mashahidi (yaani wanaume na wanawake, malaika, vipengele vya uumbaji); na kitabu cha sheria cha kuhukumu nacho (yaani, ufunuo). Sasa, Muumba wetu atawezaje kuweka haki kama hakuwaamrisha wanadamu wafuate sheria fulani katika maisha yao? Haiwezekani. Katika hali hiyo, badala ya haki, Mungu angekuwa anafanya dhuluma, kwani angewaadhibu watu kwa makosa ambayo hawakuwa na njia ya kujua ni uhalifu.
Kuna sababu nyingine kwa nini tunahitaji ufunuo? Mwanzo, bila ya kuongozwa na kuonyeshwa njia, wanadamu hawawezi hata kukubaliana juu ya masuala ya kijamii na ya kiuchumi, kisiasa, sheria, n.k. hivyo tunawezaje kukubaliana kuhusu Mungu? Pili, hakuna mtu anayeandika mwongozo wa mtumiaji kwa njia bora zaidi kuliko yule aliyetengeneza bidhaa hiyo. Mungu ndiye Muumba, sisi ni viumbe, na hakuna mtu anayejua mpango wa viumbe kwa njia bora kuliko Muumba. Je, wafanyakazi wanaruhusiwa kubuni majukumu yao ya kazi, mshahara na fidia kama wanavyotaka? Je, sisi wananchi tunaruhusiwa kuandika sheria zetu wenyewe? Hapana? Vizuri basi, kwa nini turuhusiwe kuandika dini zetu wenyewe? Kama historia imetufundisha chochote, ni kuhusu majanga yanayotokea wakati wanadamu wanafuata matamanio yao. Ni wangapi ambao wamedai kuwa na bendera ya mawazo huru wameunda dini zilizowaletea wao wenyewe na wafuasi wao majanga na maafa duniani na katika Akhera?
Hivyo kwa nini haitoshi tu kuwa mzuri? Na kwa nini haitoshi kila mmoja wetu kumwabudu Mungu kwa njia yake mwenyewe? Mwanzo, maelezo ya watu kuhusu kitu “kizuri” hutofautiana. Kwa baadhi, ni maadili ya viwango vya juu na maisha safi, kwa wengine ni wazimu na ghasia. Vilevile, dhana za jinsi ya kumtumikia na kumwabudu Muumba wetu zinatofautiana pia. Muhimu zaidi na kwa uhakika, hakuna mtu anayeweza kutembea kwenye duka au hoteli na kulipa kwa fedha tofauti kuliko ile mfanyabiashara anakubali. Dini pia ni hivyo. Ikiwa watu wanataka Mungu akubali utumwa wao na ibada zao, wanapaswa kulipa kwa fedha ambazo Mungu anadai. Na fedha hiyo ni utii kwa ufunuo Wake.
Fikiria kuhusu kulea watoto katika nyumba ambapo umeanzisha “sheria za nyumba.” Kisha, siku moja, mmoja wa watoto wako anakuambia yeye amebadilisha sheria, na atafanya mambo tofauti. Utajibu vipi? Huenda ukamjibu kwa, “Unaweza kuchukua sheria yako mpya na kwenda Jahannamu!” Naam, fikiria kuhusu hilo. Sisi ni viumbe wa Mungu, tunaishi katika ulimwengu Wake, chini ya sheria Zake, na “kwenda Jahannamu” ndicho kile Mungu atamwambia yeyote anayepuuza sheria Zake.
Ukweli huwa ngumu katika hatua hii. Tunapaswa kutambua kwamba neema zote ni zawadi kutoka kwa Muumba wetu, na hustahili shukrani. Nani hutumia zawadi kabla ya kutoa shukrani? Hata hivyo, wengi wetu hutumia neema za Mungu kwa maisha yetu yote na kamwe hatushukuru. Au tunapeana shukrani baada ya muda kuisha. Mshairi wa Kiingereza, Elizabeth Barrett Browning, alikejeli maombi ya mwanadamu akiwa msibani katika Kilio cha Binadamu:
Na midomo inasema “Mungu nihurumie,”
Ambayo hayajawahi kusema: Mwenyezi Mungu atukuzwe!
Je, hatufai kuonyesha tabia njema na kumshukuru Muumba wetu kwa neema Zake sasa, na hatimaye kwa maisha yetu yote? Je, Yeye hatudai deni hilo?
Ulijibu “Ndiyo.” Lazima uwe umejibu hivyo. Hakuna aliyesoma hadi hapa bila kukubaliana, lakini tatizo ni hili: Wengi wenu walijibu “Ndiyo,” mkijua vizuri kwamba moyo wenu na akili zenu hazikubaliana kabisa na dini za matamaduni yenu. Unakubali kuwa tuliumbwa na Muumba. Unajitahidi kumfahamu. Na unatamani kumtumikia na kumwabudu Yeye kwa namna anavyotaka. Lakini hujui jinsi gani, na hujui ni wapi pa kutafuta majibu. Na hilo, kwa bahati mbaya, sio suala ambalo linaweza kujibiwa katika makala hii. Kwa bahati mbaya, hiyo inapaswa kushughulikiwa katika kitabu, au labda hata katika mfululizo wa vitabu.
Habari njema ni kwamba nimeandika vitabu hivi. Nawakaribisha kuanza na The Eighth Scroll. Kama umependa nilichokiandika hapa, utayapenda niliyoyaandika huko.
Hakimiliki © 2007 Dkt. Laurence B. Brown; Imetumika kwa idhini.
Dkt Brown ni mwandishi wa The Eighth Scroll, kilichoelezwa na Seneta wa Jimbo la Carolina Kaskazini Larry Shaw kama, “Indiana Jones inakutana na The Da Vinci Code. The Eighth Scroll ni kitabu kinachokufanya ushike pumzi, kisichoweza kuwekwa chini baada ya kuanza, kinachopinga maoni ya Kimagharibi kuhusu ubinadamu, historia na dini. Hakina mfano, na ndicho kitabu bora katika kategoria chake!” Dr. Brown pia ni mwandishi wa vitabu vitatu vya kielimu vya ulinganisho wa kidini , Misgod'ed, God'ed, na Bearing True Witness (Dar-us-Salam). Vitabu na makala yake yanaweza kupatikana kwenye tovuti yake www.EighthScroll.com na www.LevelTruth.com, na yanaweza kununuliwa hapa www.Amazon.com.
Ongeza maoni