Lengo la maisha (sehemu ya 1 kati ya 3): Sababu na Ufunuo
Maelezo: Je, “Mantiki” ni chanzo cha kutosha katika kutafuta madhumuni ya maisha?
- Na Imam Mufti
- Iliyochapishwa mnamo 10 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,247 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Utangulizi
'Ni nini maana na lengo la maisha? ' Hili labda ni swali muhimu zaidi ambalo limewahi kuulizwa. Katika miaka yote, wanafalsafa wameona kuwa ni swali la msingi zaidi. Wanasayansi, wanahistoria, wanafalsafa, waandishi, wanasaikolojia na watu wa kawaida wote hupambana na swali hilo wakati fulani katika maisha yao.
Je, Mantiki ni Mwongozo wa Kutosha?
“Kwa nini tunakula?” “Kwa nini tunalala?” 'Kwa nini tunafanya kazi? ' Majibu tunayopata ya maswali haya yatakuwa yale yale. “Nala ili niishi.” “Nalala ili nipumzike.” 'Nafanya kazi ili nijisaidie na nisaidie familia yangu. ' Lakini linapokuja kwa suala la maana ya maisha, watu wanachanganyikiwa. Tunaona tahayuri wao katika aina ya majibu tunayopokea. Vijana wanaweza kusema, “Ninaishi kwa ajili ya pombe na usherati.” Mtaalamu mwenye umri wa kati anaweza kusema, “Ninaishi kuchanga ya kutosha ili kustaafu vizuri.” Mtu mzee anaweza kusema, “Maisha yangu yote, nimekuwa nikijiuliza kwa nini niko hapa. Ikiwa kuna lengo, sijali tena.” Na labda jibu la watu wengi litakuwa, “Kwa hakika Sijui!”
Je, basi, utagunduaje lengo la maisha? Tuna hiari mbili. Ya kwanza ni kuwacha 'mantiki ya mwanadamu'- mafanikio yaliyoadhimishwa ya enzi ya Elimu ya Kisayansi- kutuongoza. Baada ya yote,enzi hiyo ilitupatia sayansi ya kisasa kulingana na uchunguzi wa makini wa ulimwengu wa kiasili. Lakini wanafalsafa waliokuja baada ya enzi hiyo walielewa lengo hilo? Camus alielezea maisha kama “upuuzi”; Sartre alizungumzia “uchungu, kutelekezwa na kukata tamaa.” Kulingana na hao, maisha hayana maana. Wadarwini walidhani maana ya maisha ni kuzaana. Will Durant, kupambana na msiba wa mtu wa kisasa, aliandika, “Imani na matumaini yametoweka; shaka na kukata tamaa yamekuwa ada ya kila siku... si nyumba zetu na hazina zetu ndizo tupu, ni 'mioyo yetu.” Linapokuja kwa lengo la maisha, hata wanafalsafa wenye hekima wanakisia tu. Will Durant, mwanafalsafa aliyejulikana zaidi karne iliyopita, na Dk. Hugh Moorhead, profesa wa falsafa katika Chuo Kikuu cha Illinois Kaskazini, wote waliandika vitabu tofauti vilivyoitwa 'Maana ya Maisha.'[1] Waliandika kwa wanafalsafa maarufu, wanasayansi, waandishi, wanasiasa, na wasomi wa wakati wao duniani, wakiwauliza “Ni nini maana ya maisha?” Kisha walichapisha majibu yao. Wengine walitoa dhana zao , wengine walikiri kwamba walijitungia wenyewe lengo la maisha, na wengine walikuwa waaminifu kwa kusema kuwa hawakuwa na mwelekeo. Isitoshe, idadi kadhaa kati ya wasomi maarufu waliwauliza waandishi wawaandikie na kuwaambia kama lengo la maisha limegunduliwa!
Hebu Tuache mbingu “Ziseme”
Ikiwa mwanafalsafa hana jibu la uhakika, labda jibu linaweza kupatikana ndani ya moyo na akili ambayo sisi wenyewe tunamiliki. Je! Umewahi kutazama angani usiku ukiwa wazi? Utaona idadi isiyo hesabika ya nyota. Tazama darubini na utaona thurea ya nyota, nebula nzuri ambapo nyota mpya zinaundwa, mabaki ya mlipuko ya kale wa supanova yaliyoundwa katika mlipuko wa mwisho wa nyota, miviringo maridadi ya Zohali na miezi ya Mshtarii. Je, inawezekana mtu akose kuathirika na kuona nyota hizi nyingi katika anga ya usiku ikiangaza kama vumbi la almasi kwenye tandiko la mahameli nyeusi? Makundi ya nyota, yanayoendelea mpaka nyuma; yanayokuwa nzito sana kiasi kwamba yanaonekana yakiungana katika visima maridadi. Uadhama huu hutunyenyekeza, hutufurahisha, huhamasisha tamaa ya uchunguzi, na hutufanya tutafakuri. Ni jinsi gani ilikuja kuwa? Tunahusianaje na hilo, na tuna nafasi gani ndani yake? Je, tunaweza kusikia mbingu “zikizungumza” nasi?
”Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi na kukhitalifiana usiku na mchana ziko Ishara kwa wenye akili. Ambao humkumbuka Mwenyezi Mungu wakiwa wima na wakikaa kitako na wakilala, na hufikiri kuumbwa mbingu na ardhi, wakisema: Mola wetu Mlezi! Hukuviumba hivi bure. Subhanaka, Umetakasika!” (Qur'an 3:190 -191)
Tunaposoma kitabu, tunakubali kwamba kuna mwandishi. Tunapoona nyumba, tunakubali kuwa wajenzi wapo. Mambo hayo yote yalifanywa kwa kusudi na wale walioyafanya. Ubunifu, utaratibu, na utata wa ulimwengu pamoja na ulimwengu unaotuzunguka ni ushahidi wa kuwepo kwa akili kuu, mtengenezaji kamili. Sehemu zote za mbinguni zinadhibitiwa na sheria thabiti za fizikia. Je, kuna sheria bila mwanasheria? Mwanasayansi wa roketi Dr. von Braun alisema: “Sheria za kiasili za ulimwengu ni sahihi na thabiti sana kiasi kwamba hatuna shida ya kutengeneza roketi ya kupaa hadi kwa mwezi na tunaweza kuirusha na kuhesabu mwendo wake kwa kila sekunde. Lazima sheria hizi zimewekwa na mtu.” Paul Davies, profesa wa fizikia, anahitimisha kwamba kuwepo kwa mwanadamu sio tu jambo la kibahati lisilotarajiwa. Anasema: “Hakika tuliwekwa hapa.” Na anasema kuhusu ulimwengu: “Kupitia kazi zangu ya kisayansi, nimekuja kuamini zaidi na zaidi kwamba ulimwengu wa dhahiri umewekwa pamoja na ujuzi wa kushangaza sana kiasi kwamba siwezi kukubali tu kama ukweli usiopingika. Lazima, inaonekana kwangu, kuwa kuna kiwango cha kina cha maelezo.” Ulimwengu, ardhi, na vitu vilivyo hai duniani vyote vinatoa ushuhuda kwa ukimya kwa Muumba mwenye hekima, mwenye nguvu.
Ikiwa tuliumbwa na Muumba, basi hakika Muumba lazima awe na sababu, kusudi, katika kutuumba. Hivyo, ni muhimu kwamba tutafute kujua kusudi la Mungu kwa kuwepo kwetu. Baada ya kufikia lengo hili, tunaweza kuchagua kama tunataka kuishi kulingana na hilo. Lakini inawezekana tujue nini kingetokea iwapo tungeachwa pekee yatu bila mawasiliano yoyote kutoka kwa Muumba? Ni kawaida kwamba Mungu mwenyewe atatujulisha kuhusu kusudi hili, hasa kama tunatarajiwa kuitimiza.
Mbadala Wa Uvumi: Muulize Mungu
Hii inatuleta kwenye chaguo la pili: mbadala wa uvumi kuhusu maana na madhumuni ya maisha ni ufunuo. Njia rahisi zaidi ya kugundua madhumuni ya uvumbuzi ni kuuliza mvumbuzi. Ili kugundua lengo la maisha yako, muulize Mungu.
Vielezi-chini:
[1] “Kuhusu Maana ya Maisha” na Will Durant. chapa: Ray Long & Richard R. Smith, Inc New York 1932 na “Maana ya Maisha” na Hugh S. Moorhead (ed.). chapa: Chicago Tathmini Press, 1988.
Ongeza maoni