Maelezo ya Kurani kuhusu asili ya Ulimwengu

Ukadiriaji: Chaguo la Mhariri
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Maelezo ya kisayansi na Kurani kuhusu uumbaji wa ulimwengu.

  • Na islam-guide.com
  • Iliyochapishwa mnamo 23 Nov 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 24 Dec 2023
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 3,760 (wastani wa kila siku: 4)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

The_Quran_on_the_Origin_of_the_Universe_001.jpgDondoo: Sayansi ya Kosmolojia ya kisasa, ya kiuchunguzi na ya kinadharia, inaonyesha wazi kwamba, kuna wakati ulimwengu wote haukuwa chochote ila wingu la 'moshi' (yaani, wingu jeusi zito na gesi zenye joto jingi).[1] Hii ni mojawapo ya kanuni za kosmologia ya kisasa zisizo pingika. Wanasayansi sasa wanaweza kuona nyota mpya zinazoundwa kutokana na mabaki ya 'moshi' huo (tazama picha 1 na 2).

The_Quran_on_the_Origin_of_the_Universe_002.jpg

Picha ya 1: Nyota mpya inayotokana na wingu la gesi na vumbi (nebula), ambalo ni mojawapo ya mabaki ya 'moshi' iliyokuwa asili ya ulimwengu wote. (The Space Atlas, Heather na Henbest, uk. 50.)

The_Quran_on_the_Origin_of_the_Universe_003.jpg

Picha ya 2: Nebula ya Lagoon ni wingu la gesi na vumbi, lililo na upana wa takriban miaka-nuru sitini. Inasisimuliwa na mionzi ya Urujuanimno ya nyota zenye joto jingi ambazo zimeundwa hivi karibuni ndani ya upana wake. (Upeo, Kuchunguza Ulimwengu, Mbegu, picha ya 9, kutoka Chama cha Vyuo Vikuu ya Utafiti wa Astronomia)

Nyota zenye kung'aa tunazoziona usiku zilikuwa, kama vile ulivyokuwa ulimwengu wote, katika nyenzo hiyo ya 'moshi'. Mungu amesema katika Kurani:

“Kisha akaziekelea mbingu, na zilikuwa moshi...” (Kurani 41:11)

Kwa kuwa ardhi na mbingu zilizo juu (jua, mwezi, nyota, sayari, galaksi n.k.) zimeundwa kutokana na 'moshi' huo huo, tunathibitisha ya kuwa ardhi na mbingu zilikuwa kipengele kimoja kilichounganishwa. Kisha kutoka kwa 'moshi' huu mkubwa, ziliundika na kutengana. Mwenyezi Mungu amesema katika Kurani:

“Je! Hao walio kufuru hawakuona kwamba mbingu na ardhi zilikuwa zimeambatana , kisha Sisi tukazibandua? ...” (Kurani 21:30)

Dr. Alfred Kroner ni kati ya wanajiolojia mashuhuri duniani. Yeye ni Profesa wa Jiolojia na Mwenyekiti wa Idara ya Jiolojia katika Taasisi ya Sayansi za Ardhi, Chuo Kikuu cha Johannes Gutenberg, Mainz, Ujerumani. Alisema: “Unapofikiria mahali Muhammad alitoka. Nadhani ni vigumu kwamba angeweza kujua kuhusu mambo kama asili ya ulimwengu, kwa sababu wanasayansi wamegundua tu kwa miaka michache iliyopita, kwa kutumia mbinu tata ya kiteknolojia. [2]. (Kutazama video ya RealPlayer ya maoni haya, bonyeza hapa). Pia alisema: “Mtu ambaye hakujua kitu kuhusu fizikia ya nyuklia karne kumi na nne iliyopita hakuweza, nadhani, kuwa katika nafasi ya kujua kutoka kwa akili yake mwenyewe, kwa mfano, kwamba dunia na mbingu zilikuwa na asili sawa.”[3] (Kutazama video ya RealPlayer ya maoni haya, bonyeza hapa).



Vielezi-chini:

[1]Dakika Tatu za Kwanza, Mtazamo wa Kisasa wa Asili ya Ulimwengu, Weinberg, uk. 94-105.

[2]Msemo huu umenukuliwa kutoka kwa Huu ndio Ukweli (videoe). Ili kupata nakala ya video hii, zuru ukurasa huu.

[3]Huu ndio Ukweli (video).

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.