Huruma Yangu Inashinda Ghadhabu Yangu (sehemu ya 2 kati ya 2)
Maelezo: Rehema ilienea kwa maadui na wanyama.
- Na Hala Salah (Reading Islam)
- Iliyochapishwa mnamo 03 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 5,286 (wastani wa kila siku: 5)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Je, Hii Inaweza Kuwa Vita?
Pia rehema katika Uislamu inawafikia maadui, wakati wa vita na amani, kama Mtume Muhammadalivyokuwa akiwahimiza maswahaba zake kudumisha uhusiano wa kifamilia na jamaa ambao bado walikuwa makafiri kwa kuwaita na kuwapa zawadi.
Kwa nyakati za vita, Mwenyezi Mungu anawaamrisha Waislamu kuwapa hifadhi maadui ikiwa watawaomba, na anakataza mtu yeyote kuwadhuru. Haya yameelezwa katika Quran, ambapo Mwenyezi Mungu anasema nini maana yake:
“Na ikiwa mmoja wapo katika washirikina akikuomba ulinzi, basi mpe ulinzi apate kusikia maneno ya Mwenyezi Mungu. Kisha mfikishe pahala pake pa amani. Haya ni kwa kuwa hao ni watu wasiojua kitu.” (Quran 9:6)
Kwa Mtume, aliwakataza Maswahaba wake kuwadhuru wazee, majeruhi, wanawake, watoto na watu katika nyumba za ibada. Pia, kuharibu mashamba kulikatazwa. Kuharibu maiti za maadui kulipigwa marufuku kabisa na kuzika haraka haraka kuliamriwa kwa heshima.
Amri za Mtume kuhusu mateka zilifatwa kikamilifu na Maswahaba zake. Katika moja ya hadithi kuhusu vita inayohusiana nasi na mateka, anasema kwamba alikuwa akiishi na familia ya Kiislamu baada ya kutekwa. Kila walipokuwa wakila, walikuwa wakimpa upendeleo kwa kumpa mkate huku wao wakila tende tu.
Mtume rehema na baraka ziwe juu yake alipoingia Makka kwa ushindi baada ya kuwashinda Maquraishi, aliwaendea na kuwauliza:
“Unatarajia nikutende vipi?”
Wakajibu, “Wewe ni ndugu mtukufu na mtoto wa mtukufu! Hatutarajii chochote bali wema kutoka kwako.”
Kisha Mtume akatangaza: “Nina zungumza nanyi kwa maneno yale yale kama Yusuf (Nabii Yusuf) alivyo waambia ndugu zake:
“Akasema: Leo hapana lawama juu yenu. Mwenyezi Mungu atakusameheni, naye ni Mwingi wa kurehemu kuliko wote wanao rehemu.” (Quran 12:92).
Nenda, kwani wewe uko huru.”
Katika siku hii, wakati uvumilivu na msamaha haukutarajiwa sana, Mtume aliweka mfano wa rehema na msamaha kwa kuwaachilia mateka wote bila fidia, na kuwasamehe kwa kifungo na mateso ya kikatili ya Waislamu, ambayo yalikuwa yanaendelea katika miaka 13 ya mwanzo. ya kufikisha ujumbe wa Uislamu.
Viumbe vyote vya Mungu
Wanyama hawakupuuzwa na walipewa haki nyingi katika Uislamu. Kwa mfano, Mtukufu Mtume alipomwona punda mwenye uso wenye chapa, alisema:
“Je, hukusikia kwamba nime mlaani yeyote anayempiga mnyama usoni mwake au anayempiga usoni?” (Saheeh Muslim).
Mtume alisema wakati fulani kwamba mwanamke alipelekwa Motoni kwa sababu ya paka ambaye alimfunga, hakumlisha wala kumuacha huru kuwinda chakula chake. Kwa upande mwingine, Mtume alisema, mtu mmoja alikwenda Peponi kwa ajili ya kumpa maji mbwa aliyekuwa akihema kwa kiu huko jangwani.
Mtume alikataza kuwa visu vinolewe mbele ya wanyama kabla ya kuchinja. Aidha, kuchinja mnyama kabla ya mwingine ilikuwa marufuku. Hili liko wazi katika moja ya semi za Mtume:
“Mwenyezi Mungu anaitaji rehema katika kila jambo, basi fanyeni huruma mnapoua na mnapochinja, noeni makali yenu ili kupunguza maumivu yake” (Saheeh Al-Bukhari).
Swahaba mmoja alisimulia tukio hili: Walipokuwa safarini na Mtume walimkuta ndege pamoja na watoto wake, wakawachukua kutoka kwa mama yao. Ndege akaja na kuanza kupiga mbawa zake, hivyo Mtume akauliza:
“Ni nani aliyemsumbua ndege huyu kwa kuchukua makinda yake? Warudishe humo mara moja” (Saheeh Al-Bukhari).
Haki za wanyama zilithibitishwa na Mtume aliposema kwamba mtu yeyote aliyechukua kitu kilicho hai kama shabaha amelaaniwa. Kuwalazimisha wanyama kupigana hadi mmoja kumchoma mwingine pia kulipigwa marufuku vikali, kwa kuwa wanyama wanahisia na haya yangekuwa mateso dhahiri kwao.
Dhana ya Kiislamu ya rehema ni ya kiujumla na inasisitiza kuunganishwa kwa viumbe vyote na yenyewe na kwa Muumba. Rehema huanza na Mungu na hutolewa Naye kwa kila kiumbe hai. Wanyama na wanadamu kwa pamoja huonyeshana rehema, kuishi kwa upatano wao kwa wao, na kwa upande wao, kwa kuonyesha rehema hiyo, wao wenyewe wanaonyeshwa rehema hata zaidi kutoka kwa Mungu. Mtazamo huu wa Uislamu unahimiza kuvunjwa kwa vizuizi kati ya watu na ndio msingi ambao maisha na ustaarabu hujengwa juu yake.
Ongeza maoni