Mitume wa Quran: Utangulizi (sehemu ya 1 kati ya 2)
Maelezo: Kuamini manabii wa Mungu ni sehemu muhimu ya imani ya Kiislamu. Sehemu ya 1 itawataja manabii wote kabla ya Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, waliotajwa katika maandiko ya Kiislamu kuanzia Adamu mpaka Ibrahimu na wanawe wawili.
- Na Imam Mufti (© 2013 IslamReligion.com)
- Iliyochapishwa mnamo 10 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 6,683 (wastani wa kila siku: 6)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Kurani inataja manabii ishirini na watano, ambao wengi wao walitajwa katika Biblia pia. Manabii hawa walikuwa ni akina nani, waliishi wapi, walitumwa kwa nani, majina yao ni nini katika Qurani na Biblia, na baadhi ya miujiza walizofanya ni ipi? Tutajibu maswali haya rahisi.
Kabla hatujaanza, ni lazima tuelewe mambo mawili:
a.Kwa Kiarabu maneno mawili tofauti hutumiwa, Nabi na Rasool. Nabi ni nabii na Rasool ni mjumbe au mtume. Maneno haya mawili yanakaribiana kimaana kwa lengo letu.
b.Kuna watu wanne wanaotajwa katika Qurani ambao wanazuoni Waislamu hawana uhakika kama walikuwa manabii au la: Dhul-Qarnain (18:83), Luqman (Sura ya 31), Uzair (9:30), and Tubba (44:37, 50:14).
1.Aadam au Adamu ni nabii wa kwanza katika Uislamu. Pia ndiye mwanadamu wa kwanza kulingana na imani ya Kiislamu. Adamu anatajwa kwa aya 25 na mara 25 katika Qurani. Mungu alimuumba Adamu kwa mikono yake na kumuumba mkewe, Hawwa au Hawa kutokana na ubavu wa Adamu. Aliishi Peponi na akafukuzwa huko na kuletwa ardhini kwa sababu ya kutotii kwake. Hadithi ya wanawe wawili imetajwa mara moja katika Sura ya 5 (Al-Maidah).
2.Idrees au Henoki anatajwa mara mbili katika Qurani. Zaidi ya hiyo hakuna mengi yanayojulikana kuhusu maisha yake. Inasemekana aliishi Babeli, Iraki na kuhamia Misri na kwamba ndiye wa kwanza kuandika kwa kalamu.
3.Nooh au Nuhu anatajwa mara 43 katika Qurani. Inasemekana alikuwa mwenyeji wa Kirk, Iraki. Ushirikina (shirk) ulionekana kwa mara ya kwanza kati ya watu wake walioishi karibu na mji wa leo wa Kufa, kusini mwa Iraki. Mke wake alikuwa mkafiri kama ilivyoelezwa katika Sura ya 66 (At-Tahrim). Mwanawe pia alichagua kutoamini na alikufa majini. Hadithi yake inapatikana katika Sura ya 11 (Hud).
Mojawapo ya miujiza yake mikubwa ilikuwa Safina ambayo aliijenga kulingana na amri ya Mungu. Ilikaa juu ya Mlima Judi ambao unasemekana upo kati ya mpaka wa Syria na Kituruki leo karibu na mji wa Ayn Diwar.
4.Hud inasemekana ndiye Heberi kwa kiingereza. Anatajwa mara 7 katika Qurani. Hud ndiye mtu wa kwanza kuongea Kiarabu na alikuwa nabii Mwarabu wa kwanza. Alitumwa kwa watu wa Aad katika eneo linalojulikana kama Al-Ahqaf ambalo ni eneo karibu na Hadramaut nchini Yemen na Ar-Rub al-Khali (Robo Tupu). Mungu aliwaangamiza kwa upepo mkali uliovuma kwa siku 8 na usiku saba.
5.Salih anatajwa mara 9 katika Qurani. Alikuwa nabii Mwarabu aliyetumwa kwa watu wa Thamud walioishi katika eneo linalojulikana kama Al-Hijr kati ya Hijaz na Tabuk. Al-Hijr lilikuwa ni jina la kale. Leo, eneo hilo linajulikana kama “Madain Salih” huko Saudi Arabia na limeorodheshwa na UNESCO kuwa kati ya Maeneno yanayopaswa kuhifadhiwa duniani. Ni majengo makubwa sana yaliyochongwa ndani ya milima. Watu walidai atoe ngamia wa kike kutoka kwa milima ili kuthibitisha madai yake ya kuwa nabii. Akafanya, na akawaonya wasimdhuru ngamia huyo, ila wakamuua licha ya maonyo ya Salih. Ukelele mkubwa - saihah - uliwaua wote.
6.Ibrahim or Ibrahimu anatajwa mara 69 katika sura 25 za Qurani. Jina la baba yake lilikuwa Aazar. Waliishi katika mji wa Ur katika ufalme wa Wakaldayo. Alitoroka Ur kwenda Harran, kaskazini mwa bara Arabu, katika nchi ya Syria, wakati Nimrodi, mfalme, alijaribu kumchoma akiwa hai. Kutoka Harran alikwenda Palestina pamoja na mkewe Sara na mwana wa kaka yake, Lutu (Loot kwa Kiarabu) na mkewe. Kutokana na ukame, walilazimika kuhamia Misri.
Baadaye alirudi pamoja na Luti kwa upande wa kusini wa Palestina. Ibrahimu akakaa Bir Saba'a na Lutu akakaa karibu na Bahari ya Chumvi.
Ibrahimu kisha akahamisha mke wake wa pili, Hagari, kwenda Makka pamoja na mwanawe Ishmaeli na akawaacha huko kwa amri ya Mungu. Makka ilikuwa jangwa na kisima cha Zamzam kilitolewa na Mungu kwa ajili ya kuishi kwao. Kabila la kale la Jurhum liliweka makazi yao karibu na zamzam. Abrahamu inasemekana alizikwa huko Hebroni, Palestina.
7, 8. Ibrahimu alikuwa na wana wawili: Ishaq au Isaka na Ismael au Ishmaeli. Isaka anatajwa mara 16 katika Qurani ilhali Ishmaeli anatajwa mara 12. Isaka aliishi na baba yake Ibrahimu, na akafa huko Hebroni, Palestina. Mungu alimuamuru Ibrahimu amtoe Ishmaeli kama dhabihu. Alikwenda Makka pamoja na wazazi wake na akaachwa huko pamoja na mama yake. Ibrahimu alimtembelea Ishmaeli mara kadhaa huko Makka, na wakati mmoja kati ya nyakati hizo, Mungu aliwaamuru Ibrahimu na Ishmaeli wajenge Ka'bah (Nyumba Takatifu). Ismaili alikufa huko Makka na kuzikwa huko. Isaka ni baba wa Wayahudi na Ismaili ni baba wa Waarabu.
Ongeza maoni