Lengo la Maisha (sehemu ya 2 kati ya 3): Maoni ya Kiislamu

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Ufafanuzi wa Uislamu kuhusiana na lengo la maisha, na mjadala mfupi juu ya maana ya ibada.

  • Na Imam Mufti
  • Iliyochapishwa mnamo 10 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 4,382 (wastani wa kila siku: 4)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Je, Ukristo Unaweza Kujibu Swali?

Katika Ukristo, maana na lengo la maisha linategemea imani katika injili ya Yesu Kristo, katika kumkubali Yesu kama Mwokozi. “Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.” Hata hivyo, pendekezo hili halikosi matatizo makubwa. Kwanza, kama hii ndiyo kusudi la uumbaji na sharti la uzima wa milele, kwa nini haikufundishwa na manabii kwa mataifa yote ya ulimwengu? Pili, Mungu angegeuka kuwa mwanadamu wakati wa Adamu wanadamu wote wangekuwa na nafasi sawa ya uzima wa milele, ila wale waliokuja kabla ya wakati wa Yesu walikuwa na lengo lingine la kuwepo kwao! Tatu, jinsi gani watu wa leo ambao hawajasikia habari za Yesu watatimiza kusudi la Kikristo la uumbaji? Kwa kawaida, kusudi na lengo hilo ni jembamba sana na linakwenda kinyume na haki ya Mungu.

Jibu

Uislamu ndio jibu la binadamu katika utafutaji wake wa maana na lengo. Kusudi la uumbaji kwa wanaume na wanawake wote kwa nyakati zote limekuwa moja: kumjua na kumwabudu Mungu.

Qurani inatufundisha kwamba kila mwanadamu amezaliwa akimfahamu Mungu,

"Na pale Mola wako Mlezi alipo waleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Wakasema: Kwani! Tumeshuhudia. Msije mkasema Siku ya Kiyama sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo. Au mkasema: Hakika baba zetu ndio walio shirikisha kabla yetu, na sisi ni dhuriya zao tu baada yao. Basi utatuangamiza kwa sababu ya waliyo yafanya wapotovu?’"(Quran 7:172-173)

Nabii wa Uislamu anatufundisha kwamba Mungu aliumba haja hii ya kimsingi katika asili ya binadamu wakati Adamu alipoumbwa. Mwenyezi Mungu alichukua agano kutoka kwa Adamu alipo muumba. Mungu aliwaondoa wazao wote wa Adamu ambao bado hawajazaliwa, kizazi baada ya kizazi, akawatandaza, akachukua agano kutoka kwao. Akaziambia nafsi zao moja kwa moja, akiwashuhudia kwamba Yeye ndiye Mola wao Mlezi. Kwa kuwa Mungu aliwafanya wanadamu wote kuapa kwa Ubwana wake alipomuumba Adamu, kiapo hiki kinachapishwa kwenye nafsi ya binadamu hata kabla ya kuingia kwa mtoto tumboni, na hivyo mtoto anazaliwa na imani ya kiasili katika Umoja wa Mungu. Imani hii ya kiasili inaitwa fitra kwa Kiarabu. Kwa hivyo, kila mtu hubeba mbegu ya imani katika Umoja wa Mungu ambayo iko kwa undani na imezikwa chini ya matabaka ya kutoshughulikiwa na kudhoofishwa na hali ya kijamii. Ikiwa mtoto huyo angeachwa peke yake, angekua kwa ufahamu wa Mungu - Muumba mmoja - lakini watoto wote wanaathiriwa na mazingira yao. Nabii wa Mungu alisema,

"Kila mtoto amezaliwa katika hali ya 'fitra', lakini wazazi wake humfanya Myahudi au Mkristo. Ni kama vile mnyama anavyozaa watoto wa kawaida. Je! Umemwona mtoto aliyezaliwa akiwa ameshakatwa kabla hujamkata?"[1]

The_Purpose_of_Life_(part_2_of_3)_001.jpg

Kielelezo 1 Ajabu ya maisha. Mtoto aliye tumboni akinyonya kidole chake.

Kwa hivyo, kama mwili wa mtoto unavyojisalimisha kwa sheria za kimaumbile, zilizowekwa na Mungu ardhini, nafsi yake pia inajisalimisha kwa kawaida kwa ukweli kwamba Mungu ndiye Bwana na Muumba wake. Hata hivyo, wazazi wake wanamfanya afuate njia yao wenyewe, na mtoto hana uwezo wa akili wa kuipinga. Dini ambayo mtoto huifuata katika hatua hii ni ya mila na malezi, na Mwenyezi Mungu hatamuuliza kuhusu dini hii. Mtoto anapokua na kuwa mtu mzima, lazima sasa afuate dini ya elimu na sababu. Kama watu wazima, watu lazima sasa wapigane kati ya asili yao ya kumuelekea Mungu na tamaa zao ili kupata njia sahihi. Wito wa Uislamu unaelekezwa kwa hali hii ya kwanza, tabia ya kiasili, alama ya Mwenyezi Mungu juu ya nafsi, fitra, ambayo imesababisha nafsi za kila hai kukubali kuwa Yeye aliyewaumba ni Mola wao Mlezi, hata kabla ya kuundwa kwa mbingu na ardhi,

"Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi." (Quran 51:56)

Kulingana na Uislamu, kumekuwa na ujumbe wa msingi ambao Mungu ametufunulia kupitia manabii wote, tangu wakati wa Adamu hadi mwisho wa manabii, Muhammad, amani iwe juu yao. Manabii wote waliotumwa na Mungu walikuja na ujumbe huo muhimu:

"Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani...’" (Quran 16:36)

Manabii walileta jibu hilo hilo kwa swali la kutisha zaidi kwa wanadamu, jibu linalozungumzia hamu ya nafsi kwa Mungu.

Ibada ni Nini?

‘Uislamu' maana yake ni 'kujisalimisha', na kuabudu, katika Uislamu, maana yake ni 'utii kwa Mungu.’

Kila kitu kilichoumbwa 'kinajisalimisha' kwa Muumba kwa kufuata sheria za kimaumbile zilizoundwa na Mungu,

"Na vyake Yeye vilivyo mbinguni na katika ardhi. Vyote vinamt'ii Yeye." (Quran 30:26)

Wao, hata hivyo, hawapewi thawabu wala kuadhibiwa kwa 'kujisalimisha' kwao, kwa maana haihusishi hiari. Malipo na adhabu ni kwa wanao muabudu Mwenyezi Mungu, wanaokubali sheria ya kimaadili na kidini ya Mwenyezi Mungu kwa hiari yao. Ibada hiyo ndiyo kiini cha ujumbe wa manabii wote waliotumwa na Mungu kwa wanadamu. Kwa mfano, ufahamu huu wa ibada ulionyeshwa kinagaubaga na Yesu Kristo,

"Si kila mtu anayesema, ‘Bwana, Bwana,’ ambaye ataingia katika Ufalme wa mbinguni ila ni wale wanaofanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni."

‘Anachotaka Mungu' inamaanisha 'kile Mungu anataka wanadamu wafanye. 'Anavyovitaka Mungu' vinapatikana katika sheria zilizofunuliwa na Mungu ambazo manabii waliwafundisha wafuasi wao. Kwa hivyo, utii wa sheria ya Mungu ni msingi wa ibada. Ni wakati tu binadamu anapomwabudu Mungu wake kwa kujisalimisha kwa sheria Yake ya kidini ndipo anaweza kuwa na amani na maelewano katika maisha yake na matumaini ya kuingia peponi, kama vile ulimwengu unavyoendana kwa umoja kwa kujisalimisha kwa sheria za kimaumbile zilizowekwa na Mola Mlezi. Unapoondoa tumaini la kuingia mbinguni, unaondoa thamani na madhumuni ya maisha. Vinginevyo, kuna tofauti gani muhimu kama tunaishi maisha mema au mabaya? Hatima ya kila mtu itakuwa ni moja tu..



Vielezi-chini:

[1] Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim. Waarabu wangekata masikio ya ngamia na wanyama wengine kama ibada kwa miungu yao katika nyakati za kabla ya Uislamu.

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.