Kusudi la Uumbaji (sehemu ya 2 ya 3): Jibu la Kiyahudi-Kikristo
Maelezo: Utangulizi kwa swali la kutatiza zaidi katika historia ya binadamu, na mjadala kuhusu vyanzo ambavyo vinaweza kutumika kupata jibu. Sehemu ya 2: Mtazamo katika Biblia na imani ya Kikristo kuhusu mada hii.
- Na Dr. Bilal Philips
- Iliyochapishwa mnamo 10 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,465 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Maandishi ya Kiyahudi na ya Kikristo
Utafiti katika Biblia humwacha mtafutaji wa ukweli mwaminifu akiwa amechanganyikiwa. Agano la Kale linaonekana kujihusisha zaidi na sheria na historia ya mwanadamu wa kwanza na Wayahudi kuliko kujibu swali muhimu kuhusu uumbaji wa binadamu. Katika kitabu cha Mwanzo, Mungu anaumba ulimwengu na Adamu na Hawa kwa siku sita na 'anapumzika' kutoka kazi yake siku ya saba. Adamu na Hawa wanavunja amri za Mungu na wanaadhibiwa, na mwana wao Kaini anamwua mtoto wao mwingine Abeli na kuenda kuishi katika nchi ya Nodi. Naye Mungu 'akasikitika' kwamba alikuwa amemuumba mwanadamu! Kwa nini majibu hayapo hapo kwa maneno wazi na yasiyo na shaka? Kwa nini lugha yote ni ya kimajazi tu, na huacha msomaji akikisia maana yake? Kwa mfano, katika Mwanzo 6:6 inasemwa:
“Binadamu walipozidi kuongezeka duniani na kuzaa wasichana, watoto wa kiume wa Mungu waliwaona hao wasichana wa watu kuwa ni wazuri, wakawachukua wale waliowapenda kuwa wake zao.”
Hawa “wana wa Mungu” ni kina nani? Kila madhehebu ya Kiyahudi na kila moja kati ya madhehebu mengi ya Ukristo yaliyowafuata yana maelezo yao wenyewe. Ni nini tafsiri sahihi? Ukweli ni kwamba kusudi la uumbaji wa mwanadamu lilifundishwa na manabii wa zamani, hata hivyo, baadhi ya wafuasi wao - kwa kushirikiana na mashetani - baadaye walibadilisha maandiko. Majibu yakawa yasiyoeleweka na mengi ya ufunuo yalifichwa kwa lugha ya kimajazi. Mungu alipomtuma Yesu Kristo kwa Wayahudi, alipindua meza za wafanyabiashara hao walioanzisha biashara ndani ya hekalu, naye alihubiri kinyume cha tafsiri ya ibada ya sheria iliyofanywa na marabbi wa Kiyahudi. Akaithibitisha Sheria ya Nabii Musa na akaifufua. Alifundisha kusudi la maisha kwa wanafunzi wake na kuonyesha jinsi ya kuitimiza mpaka wakati wake wa mwisho katika ulimwengu huu. Hata hivyo, baada ya kuondoka kwake kutoka dunia hii, ujumbe wake pia ulipotoshwa na wengine waliodai kuwa miongoni mwa wafuasi wake. Ukweli ulio wazi alioleta ukawa usio dhahiri , kama ujumbe wa manabii mbele yake. Ufananishi ulianzishwa, hasa kupitia “Ufunuo” wa Yohana, na Injili iliyofunuliwa kwa Yesu ikapotea. Injili zingine nne zilizotungwa na wanadamu zilichaguliwa na Athanasius, askofu wa karne ya nne, kuchukua nafasi ya Injili iliyopotea ya Yesu Kristo. Na vitabu 23 vya maandishi ya Paulo na vingine vilivyojumuishwa katika Agano Jipya vilikuwa vimezidi hata matoleo manne ya Injili. Matokeo yake ni kuwa wasomaji wa Agano Jipya hawawezi kupata majibu sahihi ya swali la “Kwa nini Mungu alimuumba mwanadamu?” Na mtu hulazimika kufuata kwa upofu mafundisho yaliyoundwa na madhehebu yake. Injili hutafsiriwa kulingana na imani za kila kundi, na mtafutaji wa ukweli anaachwa tena akishangaa, ni ipi iliyo sahihi?
Umwilisho wa Mungu
Pengine dhana pekee inayowaleta pamoja madhehebu mengi ya Ukristo kuhusu kusudi la uumbaji wa wanadamu ni kwamba Mungu akawa mwanadamu ili aweze kufa mikononi mwa watu ili kuwatakasa dhambi iliyorithiwa kutoka kwa Adamu na wazao wake. Kulingana nao, dhambi hii ilikuwa kubwa kiasi kwamba hakuna tendo la kibinadamu la upatanisho au toba lingeweza kuifuta. Mungu ni mwema kiasi kwamba mtu mwenye dhambi hawezi kusimama mbele yake. Kwa hivyo, kafara ya Mungu peke yake inaweza kuokoa wanadamu kutokana na dhambi.
Imani katika kisasili hiki kilichobuniwa na mwanadamu kikawa chanzo pekee cha wokovu, kulingana na Kanisa. Kwa hivyo, kusudi la Kikristo la uumbaji likawa kutambua 'kafara ya Kimungu' na kumkubali Yesu Kristo kama Bwana Mungu. Hii inaweza kueleweka kutoka kwa maneno yafuatayo yanayohusishwa na Yesu katika Injili kulingana na Yohana:
“Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanae pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.”
Hata hivyo, kama hii ndiyo kusudi la uumbaji na sharti la uzima wa milele, kwa nini haikufundishwa na manabii wote? Kwa nini Mungu hakuwa mwanadamu wakati wa Adamu na wazao wake ili watu wote wawe na nafasi sawa ya kutimiza kusudi lao la kuwepo na kufikia uzima wa milele. Au je, wale waliokuja kabla ya wakati wa Yesu walikuwa na lengo lingine la kuishi? Watu wote leo ambao Mungu hakutaka kamwe wasikie habari za Yesu pia hawana nafasi ya kutimiza lengo waliloumbiwa. Madhumuni hayo, ni dhahiri kwamba ni madogo zaidi na hayawezi kutimiza haja ya wanadamu.
Ongeza maoni