Hadithi ya Maria kwa Ufupi

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Hadithi fupi ya mama yetu Maria na kuzaliwa kimiujiza kwa Yesu.

  • Na Marwa El-Naggar (Reading Islam)
  • Iliyochapishwa mnamo 10 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 3
  • Imetazamwa: 3,279 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Katika Uislamu, Yesu anahesabiwa kuwa mmoja kati ya manabii watano wakuu waliotumwa na Mungu kwa wanadamu. Maarifa ya Waislamu kuhusu Yesu yanatokana na vyanzo viwili vikuu vya elimu ya Kiislamu: Qurani na Hadeeth (maneno ya Mtume, rehma ziwe juu yake). Katika Qurani, Yesu anajulikana kama Isa ibn Maryam, au Yesu, mwana wa Mariamu. Hadithi ya Maria na Yesu inaelezwa vizuri kwenye Qurani katika sura ya 3 na 19.

Maria: Maisha Mazuri Utotoni

Hadithi inaanza na Maria, ambaye alibarikiwa na ulinzi wa Mungu akiwa mtoto. Maria alizaliwa katika nyumba ya wacha Mungu ya Aal Imran, au familia ya Imran. Watu wengi walitaka heshima ya kumtunza na kumlea mtoto huyo, lakini jukumu lilipewa Zekaria, ambaye alikuwa mzee na asiye na mtoto, na hapo hapo aligundua kuwa msichana huyo alikuwa wa kipekee. Siku moja, Zekaria aliona kwamba msichana alikuwa na vyakula fulani ambavyo hakuweza kujua vilitoka wapi. Akamwuliza jinsi alivyokuja kupata chakula na mtoto huyo akajibu,

“Hivi vinatoka kwa Mwenyezi Mungu; na Mwenyezi Mungu humruzuku amtakaye bila ya hisabu.” (Quran 3:37)

Jibu hili rahisi lilikuwa na athari kubwa kwa mzee Zekaria. Baada ya kutamani mwana kwa muda mrefu, Zekaria ambaye alikuwa mcha Mungu alimwomba Mwenyezi Mungu ampe watoto. Kama Qurani inavyoeleza katika aya zilizochini, maombi yake yalijibiwa mara moja, ingawa mkewe alikuwa tasa na alikuwa ashapita umri wa kubeba mimba:

“Pale pale Zakariya akamwomba Mola wake Mlezi, akasema: Mola wangu Mlezi! Nipe kutoka kwako uzao mwema. Wewe ndiye unaye sikia maombi. Alipo kuwa kasimama chumbani akisali, Malaika kamnadia: Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria Yahya, ataye kuwa mwenye kusadikisha neno litokalo kwa Mwenyezi Mungu, na ni bwana na mt'awa na Nabii kwa watu wema.” (Kurani 3:38-39)

Upekee wa Maria, ulioonekana na Zekaria, ulisemwa kwake na malaika:

“Na angalia pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Kwa hakika Mwenyezi Mungu amekuteuwa, na akakutakasa, na akakutukuza kuliko wanawake wote. Ewe Maryamu! Mnyenyekee Mola Mlezi wako na usujudu na uiname pamoja na wainamao [kwa sala].’” (Quran 3:42-43)

Hapa ndipo hadithi ya kuzaliwa kwa Maria na maisha yake ya utotoni, kama ilivyoelezwa katika Qurani, inaisha.

Muujiza wa Yesu

Katika sura ya 19, inayoitwa “Maryamu,” tunasikia mengi zaidi kuhusu hadithi ya mwanamke huyu wa kipekee, inayoelezwa vizuri na Qurani yenyewe.

“Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipo jitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki. Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu. (Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamungu. (Malaika) akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako Mlezi ili nikubashirie tunu ya mwana aliye takasika. Akasema: Nitampataje mwana hali mwanaadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba? (Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa. Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali.’ (Quran 19:16–22)

Kutokana na maelezo ya Qur'ani ya matukio hayo, tunaweza kuthibitisha kwamba Maria alitumia muda mwingi zaidi wa mimba yake akiwa peke yake. Kilichotokea kwake katika kipindi hiki hakijatajwa katika Qur'ani. Qurani inaendeleza hadithi wakati Maria alipofikia muda wa kujifungua.

“Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa! Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji!” (Quran 19:23-24)

Mungu, akijua itikio la jamii, alimwongoza zaidi kuhusu jinsi ya kukabiliana na hali hiyo:

“Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu. (Quran 19:25)

Alipomchukua mtoto Yesu na kumpelekea watu wake, walimhoji; na akiwa bado mtoto mchanga mikononi mwa mama yake, Yesu aliwapa jibu. Qurani inaeleza sehemu hii kwa undani:

“Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu. Akenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu! Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba. Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi. Akasema [Yesu], 'Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu, amenipa Kitabu na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai. Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai.’” (Quran 19:26-33)

Na hivyo mtoto Yesu alimtetea mama yake kutokana na mashtaka yoyote ya zinaa, na kwa kifupi, alieleza yeye ni nani na kwa nini alitumwa na Mungu.

Hapa ndipo inapoishia hadithi ya Maria na kuzaliwa kimuujiza kwa mmoja wa manabii wakuu wa Mungu, Yesu.

“Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka.” (Quran 19:34)

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.