Madai ya Muhammad katika Utume (sehemu ya 2 katika ya 3): Je, Alikuwa Muongo?
Maelezo: Ushahidi wa dai kuwa Muhammad alikuwa nabii wa kweli na si muongo. Sehemu ya 2: Kuangalia dai la kuwa Muhammad alikuwa muongo.
- Na Imam Mufti
- Iliyochapishwa mnamo 24 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 5,970 (wastani wa kila siku: 5)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Uchambuzi wa Kimantiki wa Dai Lake
Kama ilivyojadiliwa hapo awali, Muhammad alitoa dai, ‘Mimi ni Mtume wa Mungu.’ Pengine alikuwa mkweli katika dai lake au hakuwa mkweli. Tutaanza kwa kuangalia dai la mwisho na kuchunguza uwezekano wote uliotolewa na wakosoaji wa zamani na wa sasa, tukijadili baadhi ya maoni yao potofu. Ni ikiwa tu uwezekano mwingine wote umekamilika ambapo mtu anaweza kudai kwamba uwezekano pekee uliobaki ni kwamba ulikuwa kweli katika kile alichodai. Pia tutaangalia Kurani inasemaje kuhusu suala hilo.
. Je, alikuwa Muongo?
Je, inawezekana kwa muongo kudai kwa muda wa miaka 23 kwa uhakika usiotikisika kwamba yeye ni nabii kama Ibrahimu, Musa na Yesu, kwamba hakutakuwako tena manabii baada yake, na kwamba andiko alilotumwa nalo kubaki kuwa muujiza wake wa kudumu hadi mwisho wa nyakati?
Mtu muongo atajikwaa wakati mwingine, labda kwa rafiki, labda kwa watu wa familia yake, mahali fulani atafanya makosa. Ujumbe wake, uliotolewa kwa zaidi ya miongo miwili, wakati mwingine utajipinga wenyewe . Lakini kile tunachokiona katika uhalisia ni kwamba andiko alilolileta linatangaza uhuru kutokana na kutofautiana kwa ndani, ujumbe wake ulibaki thabiti katika utume wake wote, na hata katikati ya vita, alitangaza utume wake![1]
Hadithi ya maisha yake ni kitabu kilichohifadhiwa kwa uwazi kwa kila mtu kuweza kukisoma. Kabla ya Uislamu, alijulikana sana kwa watu wake mwenyewe kuwa ni mwaminifu na mwenye kutegemewa, mtu mwaminifu, mtu mwadilifu, asiyesema uongo.[2] Ilikuwa ni kwa sababu hii wakamwita "Al-Ameen", au "Mwaminifu" Alipinga vikali kusema uongo na akaonya dhidi yake. Je, ingewezekana kwake kusema uongo thabiti kwa muda wa miaka 23, uongo wa kutisha sana ambao ungemfanya kuwa mtu wa kutengwa na jamii, wakati hakujulikana kamwe mwenye kusema uongo hata mara moja kwenye jambo lolote? Ni kinyume na saikolojia ya waongo.
Kama mtu angeuliza kwa nini mtu anajidai mtume na kusema uongo, jibu lao lingeweza kuwa moja kati ya mawili:
1)Umaarufu, utukufu, mali, na hadhi.
2)Maendeleo ya maadili.
Kama tungesema kuwa Muhammad alidai utume kwa ajili ya umaarufu na hadhi, tungeona kuwa kile kilichotokea kilikuwa kinyume kabisa. Muhammad, kabla ya madai yake ya Utume, alikuwa na hadhi ya juu katika nyanja zote. Alikuwa wa kabila tukufu zaidi, wa familia tukufu, na alijulikana kwa ukweli wake. Baada ya madai yake, alikua mtu aliyetengwa na jamii. Kwa muda wa miaka 13 huko Makka, yeye na wafuasi wake walikabiliana na mateso makali, ambayo yalipelekea vifo vya baadhi ya wafuasi wake, kejeli, vikwazo, na kukatizwa mawasiliano na jamii.
Kulikuwa na njia nyingine nyingi ambazo mtu angeweza kupata umaarufu katika jamii ya wakati huo, hasa kutokana na ushujaa, na ushairi. Kama Muhammad angetoa madai kwamba yeye mwenyewe ndiye aliyeandika Kurani, kama itakavyoelezwa baadaye, hilo lingetosha kwa jina lake na ushairi wake kuwekwa katika dhahabu na kutundikwa ndani ya Al-Kaaba milele, watu kutoka duniani kote wakimtukuza. Bali, alitangaza kwamba yeye hakuwa mwanzilishi wa ufunuo huu na kwamba ulitoka kwa Yule aliye juu, na kumfanya adhihakiwe katika wakati wake mpaka wakati wetu.
Mtume alikuwa mume wa mfanyabiashara tajiri, na alifurahia starehe za maisha zilizopatikana kwake katika wakati wake. Lakini baada ya madai yake ya utume, akawa miongoni mwa watu masikini. Siku zilipita bila moto wa jiko kuwashwa ndani ya nyumba yake, na wakati fulani njaa ilimpeleka msikitini kwa matumaini ya kupata riziki. Viongozi wa Makka katika zama zake walimuahidi utajiri wa dunia ili aache ujumbe wake. Kwa kuwajibu ahadi yao, alisoma aya za Kurani.. Zifuatazo ni baadhi ya aya hizi:
"Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu! Kisha wakanyooka sawa, hao huwateremkia Malaika wakawaambia: Msiogope, wala msihuzunike; nanyi furahini kwa Pepo mliyo kuwa mkiahidiwa. Sisi ni vipenzi vyenu katika maisha ya dunia na katika Akhera, na humo mtapata kinacho tamaniwa na nafsi zenu, na humo mtapata mtakavyo vitaka.Ni takrima itokayo kwa Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu.Na ni nani mbora wa kusema kuliko aitaye kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema, na akasema: Hakika mimi ni katika Waislamu? Mema na maovu hayalingani. Pinga uovu kwa lilio jema zaidi. Hapo yule ambaye baina yako naye pana uadui atakuwa kama rafiki jamaa wa kukuonea uchungu. Lakini hawapewi wema huu ila wanao subiri, wala hawapewi ila wenye bahati kubwa." (Kurani 41:30-35)
Kama mtu angesema kuwa Muhammad alisema uongo na kudai utume ili kuleta mageuzi ya kimaadili na kidini katika jamii iliyojaa maovu, hoja hii yenyewe haina maana, kwani mtu anawezaje kuleta mageuzi ya kimaadili kwa njia ya uongo. Iwapo Muhammad alikuwa na shauku kubwa sana la kusimamisha na kuhubiri maadili na ibada iliyonyooka kwa Mungu Mmoja, basi je, angeweza kujidanganya kwa kufanya hivyo? Iwapo tutasema kuwa hilo haliwezekani, jibu pekee ni kwamba alikuwa anaongea ukweli. Uwezekano mwingine uliobaki ni kwamba alikuwa mwendawazimu.
Ongeza maoni