Habari za zamani
Maelezo: Hadithi zilizosimuliwa na Mtume Muhammad za watu wa zamani ni sehemu ya ushahidi wa Utume wake.
- Na Imam Mufti
- Iliyochapishwa mnamo 24 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 31 Aug 2024
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 3,493 (wastani wa kila siku: 3)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Moja ya ushahidi wenye nguvu zaidi wa ukweli wa Mtume Muhammad ni maarifa yake ya Ulimwengu uliojificha: maarifa yake sahihi ya mataifa yaliyopita na utabiri ujao. Haijalishi mwanadamu ana akili kiasi gani, mwanadamu hawezi kusema yaliyopita kwa kujiamini kwa kutegemea akili tu. Taarifa lazima ifunzwe. Muhammad alikuwa mwanadamu, ambaye hakuishi katikati ya mataifa aliyoyazungumzia, hakurithi maarifa yoyote ya ustaarabu wao, au kujifunza kutoka kwa mwalimu. Mwenyezi Mungu anasema:
"Hizi ni khabari za ghaibu tunazo kufunulia; nawe hukuwa nao walipo kuwa wakitupa kalamu zao nani wao atamlea Maryamu, na hukuwa nao walipo kuwa wakishindana." (Kurani 3:44)
"Hizi ni katika khabari za ghaibu tulizo kufunulia. Na hukuwa pamoja nao walipo azimia shauri yao, walipo fanya njama zao wakizua vitimbi." (Kurani 12:102)
Zingatia aya hizi:
"Na hakika bila ya shaka tulimpa Musa Kitabu baada ya kwisha ziangamiza kaumu za mwanzo, ili kiwafumbue macho watu, na kiwe uwongofu, na rehema, ili wapate kukumbuka. Wala wewe hukuwa upande wa magharibi tulipo mpa Musa amri, wala hukuwa katika walio hudhuria. Lakini Sisi tuliziumba kaumu, na ukawa mrefu umri juu yao. Wala hukuwa mkaazi na watu wa Madyana ukiwasomea Aya zetu. Lakini ni Sisi tulio kuwa tukiwatuma Mitume. Wala hukuwa kando ya mlima tulipo nadi. Lakini ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi ili uwaonye watu wasio pata kufikiwa na mwonyaji kabla yako, huenda wakakumbuka. Na usije kuwasibu msiba kwa iliyo yatanguliza mikono yao, wakasema: Ewe Mola wetu Mlezi! Mbona hukututumia Mtume nasi, tukafuata Ishara zako, na tukawa miongoni mwa Waumini?’" (Kurani 28:43-47)
Matukio haya katika hadithi ya Musa yalihusiana na Muhammad. Ama aliwashuhudia na alikuwepo pale, au alijifunza kutoka kwa wale wanaojua. Kwa vyovyote vile, hangekuwa nabii wa Mungu. Uwezekano mwingine, wa hitimisho lisiloweza kuepukika, ni kuwa Muhammad alifundishwa na Mungu Mwenyewe.
Mambo machache lazima yazingatiwe ili kutambua nguvu kamili ya hoja. Muhammad hakujifunza kutoka kwa mwanachuoni wowote wa kidini, hakukuwa na wanazuoni wa Kiyahudi au Wakristo huko Makka wakati huo, na hakujua lugha yoyote isipokuwa Kiarabu. Mbali na yaliyotangulia, hakujua kusoma wala kuandika. Hakuwa mwanamakka, Myahudi, au Mkristo aliyewahi kudai kuwa mwalimu wa Muhammad. Lau Muhammad angejifunza kutoka kwenye chanzo chochote, masahaba zake waliomwamini wangemfichua.
"Sema: Mwenyezi Mungu angeli taka nisingeli kusomeeni, wala nisingeli kujuvyeni. Kwani nalikwisha kaa nanyi umri mzima kabla yake! Basi, je! Hamzingatii?’" (Kurani 10:16)
Licha ya upinzani wao mkali, makafiri hawakuweza kuhusisha ujuzi wake wa zamani na sasa na chanzo chochote. Kushindwa kwa watu wa wakati wake ni uthibitisho tosha dhidi ya watu wote wenye kutilia shaka baadaye.
Marekebisho ya Kutoelewana kwa Wayahudi na Wakristo
Ifuatayo ni mifano miwili ya Kurani inayosahihisha kile ambacho kilikuwa kimepitia mabadiliko katika imani za Kiyahudi na Kikristo:
(1) Wayahudi wanadai Ibrahimu kuwa Myahudi, baba wa taifa la Kiyahudi, ambapo Wakristo wanamwona kuwa baba yao pia, kama vile Kanisa Katoliki linamwita Ibrahimu "baba yetu wa Imani" katika sala ya Ekaristi inayoitwa Canon ya Kirumi inayosomwa wakati wa Misa. Mungu anawajibu katika Kurani:
"Enyi Watu wa Kitabu! Mbona mnabishana juu ya Ibrahim, na hali Taurati na Injili hazikuteremshwa ila baada yake? Basi hamzingatii?" (Kurani 3:65)
(2) Kurani inakanusha kwa nguvu zote kusulubiwa kwa Yesu, tukio kubwa katika dini zote mbili:
"Basi kwa sababu ya kuvunja kwao ahadi zao, na kuzikataa kwao ishara za Mwenyezi Mungu, na kuwauwa kwao Manabii bila ya haki, na kusema kwao: Nyoyo zetu zimefumbwa; bali Mwenyezi Mungu amezipiga muhuri kwa kufuru zao, basi hawaamini ila kidogo tu. Na pia kwa kufuru zao na kumsingizia kwao Maryamu uwongo mkubwa. Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masihi Isa, mwana wa Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu - nao hawakumuuwa wala hawakumsalibu, bali walifananishiwa tu. Na hakika walio khitalifiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hawakumuuwa kwa yakini." (Kurani 4:155-157)
Kukanusha huku kwa Kurani kunazua baadhi ya maswali ya kimsingi.
Kwanza, ikiwa mafundisho ya Kiislamu yalichukuliwa kutoka kwenye Uyahudi na Ukristo, kwa nini yalikataa kusulubiwa? Baada ya yote, dini zote mbili zinakubali kwamba lilifanyika! Kwa Wayahudi, ni Yesu wa uongo ambaye alisulubiwa, lakini kwa Wakristo, alikuwa Mwana wa Mungu. Mtume Muhammad angeweza kukubali kwa urahisi kusulubishwa kwa Yesu, hii ingetoa sifa zaidi katika ujumbe wake. Iwapo Uislamu ungekuwa dini ya uwongo, uigaji wa Uyahudi au Ukristo, au kama Muhammad hakuwa mkweli katika madai yake, Uislamu usingechukua msimamo usiobadilika katika suala hili na kuzitangaza dini zote mbili kuwa ni potofu kabisa katika suala hili, kwakuwa hakuna kitu kingewezakupatikana kwa kukataa kwake.
Pili, kama Uislamu ungechukua hadithi ya kusulubiwa kutoka kwenye dini hizi mbili, ungeondoa nukta ya mabishano makubwa baina yao, lakini Uislamu ulileta ukweli na haukuweza kuthibitisha uzushi ili tu kuwaridhisha. Inawezekana kabisa Mayahudi waliwajibika katika kumsulubu Yesu, kwasababu makosa yao ya kihistoria dhidi ya manabii wa Mungu yameandikwa kwenye biblia na Kurani vile vile. Lakini kuhusu Yesu, Kurani inasisitiza:
"Wala hawakumuua, wala hawakumsulubu."
Je, inawezekana vipi, kusema kuwa Muhammad aliitengeneza Kurani kwa habari alizojifunza kutoka kwa wanazuoni wa Kiyahudi au Wakristo wakati alileta itikadi zinazong'oa mafundisho yao?
Tatu, kukataa kusurubiwa peke yake kuna kanusha imani zingine za Kikristo:
(i) Kafara ya Yesu kwa dhambi za binadamu.
(ii) Mzigo wa dhambi ya asili kubebwa na watu wote.
(iii) Kuondoa hadithi ya msalaba na heshima yake.
(iv) Karamu ya mwisho na Ekaristi.
Hivyo tunaona kuwa hadithi za Mtume, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alizosimulia kuhusu mataifa ya zamani hazikuwa hadithi za kale, wala hazikufundishwa kutoka kwa wasomi wa Kiyahudi au Wakristo. Bali yalifunuliwa kwake kutoka juu ya mbingu ya saba na Mungu wa uumbaji.
Ongeza maoni