Mungu ni al-Mujeeb - Mwenye kujibu maombi

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Maelezo ya mojawapo ya jina zuri la Mungu, al-Mujeeb, ambalo linatia matumaini ndani yetu na hutufariji na kutufanya tutambue kwamba hatuko peke yetu.

  • Na islamtoday.net [edited by IslamReligion.com]
  • Iliyochapishwa mnamo 03 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 27 Aug 2023
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,827 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

God_is_al-Mujib___The_Answerer_of_Prayers._001.jpgJina hili la Mwenyezi Mungu linapatikana katika aya ya Kurani ifuatayo: "Basi mwombeni msamaha, kisha mtubu kwake. Hakika Mola wangu Mlezi yupo karibu, anaitikia maombi." (Kurani 11:61)

Mungu hujibu maombi ya wale wanaomwomba. Anawapa nafuu wale wanaokimbilia Kwake na Anawatuliza hofu zao. Anajibu hata maombi ya makafiri na walioghafilika wanapo muita katika hali ya kukata tamaa.

Yeye ndiye anaye kuendesheni bara na baharini. Hata mnapo kuwa majahazini na yakawa yanakwenda nao kwa upepo mzuri wakaufurahia, upepo mkali ukawazukia, na yakawajia mawimbi kutoka kila upande, na wakaona wameshazongwa, basi hapo humwomba Mwenyezi Mungu kwa kumsafishia niya: "Ukituokoa na haya bila ya shaka tutakuwa miongoni mwa wanao shukuru." Lakini akisha waokoa, mara wanafanya jeuri tena katika nchi bila ya haki! (Kurani 10:22-23)

Mwenyezi Mungu alimjibu Nuhu (amani iwe juu yake) katika dhiki yake, akamuokoa yeye na wafuasi wake katika Safina pale Alipowazamisha watu wakosefu katika Gharika. "Na hakika Nuhu alitwita, na Sisi ni bora wa waitikiaji." (Kurani 37:75)

Mungu alijibu maombi ya Ayubu (amani iwe juu yake): "Na Ayubu, alipo mwita Mola wake Mlezi, akasema: 'Mimi yamenipata madhara. Na Wewe ndiye unaye rehemu kuliko wote wanao rehemu.’ Basi tukamwitikia, na tukamwondolea madhara aliyo kuwa nayo, na tukampa watu wake na mfano wao pamoja nao kuwa ni rehema inayo toka kwetu, na ukumbusho kwa wafanyao ibada." (Kurani 21:83-84)

Mungu alijibu maombi ya Yona (amani iwe juu yake) alipolia kutoka tumboni mwa nyangumi: "Na Dhun-Nun alipoondoka hali ameghadhibika, na akadhani ya kwamba hatutakuwa na uwezo juu yake. Basi aliita katika giza: Hapana mungu isipo kuwa Wewe Subhanaka Uliye takasika. 'Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa wenye kudhulumu!’ Basi tukamwitikia na tukamwokoa kutokana na dhiki. Na hivyo ndivyo tunavyo waokoa Waumini." (Kurani 21:87-88)

Kadhalika, Mungu alijibu maombi ya Ibrahimu, Zakaria, Yohana Mbatizaji, Yesu, na hakika kila mmoja wa Mitume na Mitume wake (amani iwe juu yao wote). Walimuomba Mola wao Mlezi kwa unyenyekevu na unyofu wa hali ya juu, basi Yeye, kwa fadhila yake isiyo na kikomo, akawalinda, akawaongoza, akawaheshimu na akakubali maombi yao.

Mungu ndiye anayejibu maombi ya wale wanaomwomba na kuweka matumaini yao kwake. Ni Mungu peke yake ndiye ambaye sala na dua zote zinapaswa kufanywa kwake.

"Na Mola wenu Mlezi anasema: "Niombeni nitakuitikieni. Kwa hakika wale ambao wanajivuna na kuniabudu Mimi wataingia Jahannamu wadhalilike"" (Kurani 40:60)

Mungu ametuamrisha dua na ameahidi kujibu maombi yetu. Ndiyo maana Umar alikuwa akisema: "Sina wasiwasi kwamba dua zangu zitajibiwa. Nina wasiwasi na dua zangu wenyewe."

Kwa maneno mengine, mtu anapobarikiwa kumsihi Bwana, hii yenyewe ndiyo faida. Kuhusu jibu, hilo ni jambo ambalo tayari limetolewa.

"Mwenyezi Mungu hukuokoeni kutoka hayo, na kutoka kila mashaka, na kisha nyinyi mnamshirikisha!." (Kurani 6:64)

Dua zetu kwa Mwenyezi Mungu ni njia za kuondoa balaa na matatizo, na kupata baraka na fursa kwetu. Walakini, dua sio sababu pekee ya athari hizi zinazohitajika. Kuna sababu zingine ambazo zina hitaji kutambuliwa pia, pamoja na uhusiano wa asili na athari.

Mungu, kwa hekima yake, anajua kilicho bora zaidi. Amefanya dua zetu kuwa mojawapo ya vitu vinavyo athiri maisha yetu, na Ameahidi kujibu maombi yetu. Hii ina maana kwamba wakati mwingine Yeye anatujibu kwa usahihi kile tunachoomba. Nyakati nyingine, Anaweza kuzuia majanga yasitupate ambapo vinginevyo tungekusudiwa kupata. Pia anaweza akaahirisha kutujibu maombi hayo mpaka siku ya Kiama, na atupe baraka zake siku hiyo kwa hukumu na malipo yetu huko Akhera kwa kuipima neema yetu siku hiyo wakati matendo yetu yanapimwa. Hili limehakikishwa kwa wote wanaomwomba Mungu kwa unyenyekevu na kujitolea. Na kuhusu jibu la maombi yetu yanayokuja katika ulimwengu huu na kile tunachoomba, hii ni kawaida.

Tunaposoma kuhusu maisha ya manabii, tunashuhudia matukio mengi ambapo Mungu alijibu maombi yao. Mtume Muhammad rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, alimuomba Mwenyezi Mungu kwa niaba ya idadi ya Masahaba wake. Alimwomba Mungu kuhusu Ibn Abbas akiuliza: "Ewe Mola! Mjaalie ujuzi wa kina wa dini." Aliomba kwamba Anas ibn Malik apate maisha marefu na watoto wengi. Aliomba kwamba Umar ibn al-Khattab angesilimu na kuongeza nguvu zake kwa umma wa Kiislamu. Alimwomba Mwenyezi Mungu kwa niaba ya makabila mengi aliyochangamana nayo, na akamuomba Mwenyezi Mungu kwa ajili ya Waislamu wote katika zama zote.

Tunapata masimulizi mengi, ya zamani na ya sasa, ya jinsi Mungu alivyojibu dua za watu. Popote ambapo watu wanamwamini Mungu, hata kama wanaweza kuwa wadhambi katika matendo yao na wamepotoshwa katika ufahamu wao wa kidini, tunawapata wakizungumza kuhusu jinsi Mungu alivyojibu maombi yao na kuondoa matatizo yao. Hili ni jambo ambalo haliwezi kukanushwa, uthibitisho zaidi unaothibitisha kuwepo kwa Mungu na rehema zake. Hii ndiyo sababu kwa nini hatupati mtu yeyote anapokabiliwa na majanga au taabu kubwa, ambaye anajizuia kumgeukia Mungu ili kumwondolea dhiki yake.

Faida ya Kulijua Jina hili la Mungu

Kufahamu kwamba Mungu ndiye Mjibu wa Sala ni faraja na chanzo cha nguvu kwa wale ambao wamekatiliwa mbali na tumaini lingine au mategemeo mengine, na ni Mungu pekee wa kumgeukia. Kwa wakati huu, wanamgeukia Mungu kwa moyo mnyofu na wa kujitolea zaidi, kwa hiyo Mungu huwaondolea mizigo yao haraka na kuwaondolea taabu zao.

Ndivyo ilivyo kwa wale wanaosota gerezani bila mtu wa kuwatetea. Ndivyo ilivyo kwa mtu aliyepotea peke yake nyikani. Ndivyo hali ilivyo kwa baharia ambaye meli yake inatupwa baharini katika dhoruba kali. Ndiye mgonjwa mahututi ambaye madaktari wamekata tamaa na anaye pata nafuu baada ya kumgeukia Mungu. Ndiye aliyedhulumiwa ambaye anadhulumiwa na mwenye nguvu, ambaye Mwenyezi Mungu anasema juu ya maombi yake: "Kwa uwezo wangu na utukufu wangu, nitakupa ushindi, ingawa ni baada ya muda."[1]



Rejeleo la maelezo:

[1]Sunan al-Tirmidhi, Sunan Ibn Majah

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.