Biblia Inakana Umungu wa Yesu (sehemu ya 3 kati ya 7): Yesu Si Mwenye Nguvu Zote, na Hajui Yote.
Maelezo: Biblia inaonyesha waziwazi kwamba Yesu hakuwa mwenye nguvu zote na ujuzi wote kama jinsi Mungu wa kweli anavyopaswa kuwa.
- Na Shabir Ally
- Iliyochapishwa mnamo 18 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 2
- Imetazamwa: 7,830 (wastani wa kila siku: 7)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Wakristo na Waislamu wanakubali kwamba Mungu ni muweza wa yote na mjuzi wa yote. Injili zinaonyesha kwamba Yesu hakuwa ni mwenye nguvu zote, na asiyejua yote, kwa kuwa alikuwa na mapungufu fulani.
Marko anatuambia katika injili yake kwamba Yesu hakuweza kufanya kazi yoyote yenye nguvu katika mji wake wa asili isipokuwa mambo machache tu: “Hakuweza kufanya miujiza yoyote huko, isipokuwa aliweka mikono yake juu ya wagonjwa wachache na kuwaponya.” (Marko 6:5). Marko pia anatuambia kwamba Yesu alipojaribu kumponya kipofu fulani, mtu huyo hakuponywa baada ya jaribio la kwanza, na Yesu alilazimika kujaribu mara ya pili (angalia Marko 8:22-26).
Kwa hiyo, ingawa tunampenda na kumheshimu sana Yesu, tunahitaji kuelewa kwamba yeye sio Mungu mwenye nguvu zote.
Injili ya Marko pia hufunua kwamba Yesu alikuwa na mipaka katika ujuzi wake. Katika Marko 13:32, Yesu alitangaza kwamba yeye mwenyewe hajui siku ya mwisho itatokea lini, lakini Baba peke yake ndiye anayejua hilo (angalia pia Mathayo 24:36).
Kwa hiyo, Yesu asingeweza kuwa Mungu ajuaye yote. Wengine watasema kwamba Yesu alijua siku ya mwisho itakuja lini, lakini aliamua kutosema. Lakini hilo linafanya mambo kuwa magumu zaidi. Yesu angeweza kusema kwamba anajua lakini hataki kusema. Badala yake, alisema kuwa hajui. Ni lazima tumwamini. Yesu hasemi uongo hata kidogo.
Injili ya Luka pia inafunua kwamba Yesu alikuwa na ujuzi mdogo. Luka anasema kwamba Yesu aliongezeka katika hekima (Luka 2:52). Katika Waebrania pia (Waebrania 5:8) tunasoma kwamba Yesu alijifunza utii. Lakini ujuzi na hekima ya Mungu daima ni kamilifu, na Mungu hajifunzi mambo mapya. Anajua kila kitu siku zote. Kwa hiyo, ikiwa Yesu alijifunza jambo jipya, hilo linathibitisha kwamba hakujua kila kitu kabla ya hapo, na hivyo hakuwa Mungu.
Mfano mwingine wa ufahamu mdogo wa Yesu ni kipindi cha mti wa mzaituni katika Injili. Marko anatuambia hivi: “Siku iliyofuata walipokuwa wakitoka Bethania, Yesu alikuwa na njaa. Akaona kwa mbali mti wa mzaituni kwenye majani, akaenda ili aone kama ulikuwa na matunda. Alipoufikia, hakuona kitu ila majani tu, kwa maana haukuwa msimu wake.” (Marko 11:12-13).
Ni wazi kutokana na aya hizi kwamba ujuzi wa Yesu ulikuwa na mipaka kwa mambo mawili. Kwanza, hakujua kwamba mti huo haukuwa na matunda hadi alipoufikia. Pili, hakujua kwamba haukuwa msimu mzuri wa kutarajia mizaituni kwenye miti.
Je, anaweza kuwa Mungu baadaye? Hapana! Kwa sababu kuna Mungu mmoja tu, naye ni Mungu tangu milele hata milele (angalia Zaburi 90:2).
Mtu anaweza kusema Yesu alikuwa Mungu lakini alichukua umbo la mtumishi na hivyo akawa na mipaka. Naam, hiyo ingemaanisha kwamba Mungu alibadilika. Lakini Mungu habadiliki. Mungu alisema hivyo kulingana na Malaki 3:6.
Yesu hakuwa Mungu kamwe, na hatakuwa kamwe. Katika Biblia, Mungu anatangaza hivi: “Kabla yangu hakuna mungu aliyeumbwa, wala hatakuwepo mwingine baada yangu.” (Isaya 43:10).
Ongeza maoni