Ishara za Utume katika Maisha Matukufu ya Mtume Muhammad (sehemu ya 2 kati ya 2): Baada ya Utume

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Maisha ya Mtume Muhammad yalibadilika sana baada ya ufunuo kuanza. Jinsi alivyojirekebisha ilikuwa ni moja ya dalili za wazi za Utume.

  • Na Aisha Stacey (© 2013 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 10 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 4,671 (wastani wa kila siku: 4)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

SignsProphethood2.jpgAkiwa na umri wa miaka 40, Mtume Muhammad alikuwa mfanyabiashara imara na mwanafamilia aliyepewa vipindi vya kutafakari na kujitathmini. Alikuwa ni raia mwenye kuheshimika sana Makka na watu walikuwa na desturi ya kuja kwake ili kusuluhisha mabishano, ushauri, na kuhifadhi vitu vyao vya thamani. Haya yote hata hivyo yalikuwa karibu kubadilika kwa sababu katika moja ya vipindi vyake vya kutengwa na kutafakari alitembelewa na malaika Jibrili na aya za Kurani zilianza kufunuliwa kwake. Kazi yake ilikuwa imeanza; maisha yake hayakuwa yake tena - sasa yalikuwa yamejitolea kueneza neno la Uislamu.

Labda kwa sasa baadhi ya matukio katika maisha yake yalianza kuwa na maana. Labda aliweza kuona kuwa Mungu alikuwa ameyapanga mambo kwa ajili yake, kwa kuangalia nyuma tunaweza kuona kuwa dalili za Utume zilikuwa zikionekana katika nyanja nyingi na matukio mengi katika maisha yote ya Mtume Muhammad. Kabla ya kazi yake, maisha ya Muhammad yalikuwa mepesi. Alikuwa na ndoa nzuri na yenye furaha, watoto, hakuwa na wasiwasi wa kifedha na bila shaka alizungukwa na marafiki na familia ambayo ilimpenda na kumheshimu.

Kutangaza Utume wake kwa haraka kulimfanya kuwa masikini, mtu aliyetengwa na jamii, na maisha yake yalitishiwa kwa zaidi ya tukio moja. Ukuu, nguvu, mali, na utukufu vilikuwa vitu vya mbali zaidi kuwepo kwenye akili yake. Kwa hakika, tayari alikuwa na vitu hivi, ingawa kwa kiwango kidogo. Hakuwa apate faida yoyote kwa kuutangaza Utume wake pamoja na azma ambazo hazikuwa za ukweli. Mtume Muhammad, familia yake, na wafuasi wake walidhihakiwa, kukashifiwa, na kupigwa kimwili, mtindo wake wa maisha ulibadilika sana na kuwa mbaya zaidi.

Mmoja wa sahaba wa Muhammad, alisema, “Mtume wa Mwenyezi Mungu hakuona mkate uliotengenezwa kwa unga laini tangu Mungu alipomtuma (kama Mtume) hadi alipokufa.”[1] Mwingine amesema kuwa" Mtume alipofariki, hakuacha pesa wala kitu kingine chochote isipokuwa punda wake mweupe, silaha zake na kipande cha ardhi alichokiacha kama sadaka."[2]

Kabla ya Mtume Muhammad kufa, alikuwa kiongozi wa himaya, iliyokuwa na uwezo wa kupata hazina ya kitaifa lakini aliishi maisha ya kawaida, akishughulika tu na kukamilisha kazi yake na kumwabudu Mungu. Licha ya majukumu yake kama Mtume, mwalimu, mwanasiasa, jenerali, hakimu, na mpatanishi, Muhammad alikuwa akiwakamua mbuzi wake mwenyewe, akitengeneza nguo na viatu vyake, na pia kusaidia kazi za jumla za nyumbani.[3] Maisha ya Mtume Muhammad yalikuwa ni mfano bora wa utu na ukawaida. Mavazi na mtindo wake wa maisha haukumtofautisha na wafuasi wake. Pindi Mtu alipoingia kwenye mkusanyiko hapakuwa na kitu chochote kuhusu Mtume Muhammad ambacho kilimtofautisha na watu wengine kwenye mkusanyiko huo.

Katika miaka ya mwanzo ya kazi yake, muda mrefu kabla hata ya kuwa na uwezekano wa kufanikiwa, Muhammad alipokea ahadi ya kuvutia kutoka kwa viongozi wa Makka. Wakifikiri kuwa lazima Muhammad anasema madai hii ya Utume kwa ajili ya manufaa ya kibinafsi, kisha mjumbe alimjia na kusema “...Kama unataka pesa, tutakusanya pesa za kukutosha ili uwe tajiri kuliko sisi. Ukitaka uongozi, tutakuchukua wewe kama kiongozi wetu na kamwe tusiamue jambo lolote bila kibali chako. Ukitaka ufalme, tutakutawaza kuwa mfalme juu yetu...”. Kwa mwanadamu yeyote, katika kipindi chochote cha kihistoria, hii itakuwa ni ahadi ngumu sana kukataa; hata hivyo, Muhammad hakuwa na hamu ya kujinufaisha binafsi au kutambuliwa. Ingawa kulikuwa na sharti moja tu la ukarimu huu lilikuwa linakwenda kinyume na kila kitu ambacho Muhammad alikisimamia. Viongozi wa Makka walitarajia akate tamaa na mwito wake wa Uislamu na kuacha kumwabudu Mungu peke yake, bila mshirika yeyote. [4] Mtume Muhammad alikataa kabisa ahadi hiyo.

Katika tukio jingine, Abu Talib, ambaye ni ami yake Muhammad alihofia maisha ya mpwa wake na akamsihi aache kuwaita watu kwenye Uislamu. Tena jibu la Muhammad lilikuwa la maamuzi na la kweli, akasema, “Naapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, Ewe Mpwa wangu!, hata kama wataliweka jua kwenye mkono wangu wa kulia na mwezi katika mkono wangu wa kushoto kwa malipo ya kuacha jambo hili (kuwalingania watu katika kujiunga kwenye Uislamu), sitaacha kamwe mpaka Mwenyezi Mungu aushinde au niangamie nikiutetea.”[5]

Njia nyingi zilichukuliwa na makafiri wa Makka kuchafua tabia ya Muhammad na kudharau ujumbe aliokuwa akijaribu kueneza. Hawakuwa na huruma walipoidharau Kurani yenyewe. Walidai kwa dhati kuwa Kurani haikufunuliwa na Mwenyezi Mungu na kuwa Mohammad aliiandika yeye mwenyewe. Hili lilifanyika ili kuwakatisha tamaa watu kumfuata Muhammad au kuamini madai yake ya kuwa Mtume wa Mungu. Mtume Muhammad hakuandika Kurani. Alikuwa mtu asiye na elimu, asiyejua kusoma wala kuandika kabisa. Hakuweza kujua au hata kukisia baadhi ya ukweli wa kisayansi ambao Kurani inataja kwa urahisi na mara kwa mara.

Zaidi ya hayo, inaleta mantiki kusema kwamba lau kuwa Kurani ingeandikwa na Muhammad angejisifu na kujitaja zaidi. Kurani kwa hakika inawataja Manabii wawili Isa na Musa mara nyingi zaidi kwa majina kuliko inavyomtaja Mtume Muhammad. Kurani pia inamkemea na kumsahihisha Mtume Muhammad. Je, nabii muongo anaweza kujihatarisha kujifanya aonekane kama mtu anayeweza kufanya makosa?

Mtume Muhammad alikuwa mfanyabiashara wa Kiarabu asiye na elimu. Huenda maisha yake hayakuwa ya ajabu isipokuwa kwamba tangu mwanzo wa kuwepo kwake Mungu alikuwa pamoja naye, akimtayarisha kwa ajili ya Utume na kumwandaa kuuongoza ulimwengu wote katika enzi mpya ya ukuaji wa kidini. Muhammad alipokua, alijulikana kuwa mkweli, mwaminifu, muadilifu, mkarimu, na mpole. Pia alijulikana kuwa mtu wa kiroho sana na kwa muda mrefu alikuwa amechukia upotovu wa waziwazi na ibada ya sanamu katika jamii yake.

Tunapoyatazama maisha ya Mtume Muhammad kwa umbali wa muda tunaweza kuona kwa uwazi kwamba maisha yake yalikuwa ya kumtumikia Mwenyezi Mungu, lengo lake pekee lilikuwa kufikisha ujumbe. Uzito wa ujumbe huo ulimlemea sana mabegani mwake na hata kwenye mahubiri yake ya mwisho alikuwa na shaka na kuwataka watu washuhudie kwamba alikuwa ameufikisha ujumbe wa Mungu. Kama Muhammad angetaka madaraka au umaarufu angelikubali ahadi ya kuwa kiongozi wa Makka. Kama angekuwa anatafuta utajiri hangeishi maisha ya kawaida, akifa akiwa hana mali yoyote, tofauti na kiongozi mwingine yeyote mwenye mamlaka. Ukawaida wa maisha ya Mtume Muhammad na hamu yake isiyoyumba ya kueneza ujumbe wa Uislamu ni dalili zenye nguvu za uhalali wa madai yake ya Utume.



Vielezi-chini:

[1] Saheeh Al-Bukhari

[2] Ibid

[3] Saheeh Al-Bukhari, Imam Ahmad.

[4] Al-Serah Al-Nabaweyyah, Ibn Hisham, Toleo la. 1.

[5] Ibid.

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

(Soma zaidi...) Ondoa