Vyanzo vya Uislam: Kurani na Sunnah (sehemu ya 2 kati ya 2)
Maelezo: Dini ya Uislamu imejengwa na Kurani (Neno la Mungu) na Sunnah (mafundisho na sifa za Mtume Muhammad). sehemu ya 2: Sunnah: Chanzo cha Pili cha Uislamu
- Na islaam.net
- Iliyochapishwa mnamo 06 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 3,024 (wastani wa kila siku: 3)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Sunnah
Neno Sunnah linatokana na neno sanna, likimaanisha kuweka nafasi au kufanya njia ipitike kirahisi, hivyo ikaja njia ya kufuatwa na kila mtu baadae. Hivyo Sunnah inaweza kutumika kuelezea mtaa au barabara au njia ambayo watu, wanyama, na magari yanasafiri. Cha kuongezea, inaweza kutumika kwa njia ya kinabii, mf. sheria ambayo waliileta kama ufafanuzi au maelezo zaidi ya kitabu kilichofunuliwa na Mungu. Kwa kawaida, njia ya kinabii inahusisha marejeo ya aliyosema, vitendo, sifa za kimwili na tabia.
Kutoka katika mtazamo wa Kiislam, Sunnah inamaanisha kitu chochote kilichosemwa au kumuhusu Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, inafuatiliwa kwa kuthibitisha kwake ikihusisha mafunzo yake, vitendo, sifa, na idhini ya kimya kimya.
Kila simulizi imeundwa na sehemu mbili: isnad na matn. Isnad inahusisha mlolongo wa watu ambao wamesimulia kisa flani. Matn ni maandishi halisi ya kisa. Isnad lazima iwe na watu waadilifu na wakweli ambao uadilifu wao hauna shaka.
Maneno ya Mtume Muhammad
Maneno ya Mtume Muhammad yanachukuliwa kama misemo yake. Kwa mfano, alisema:
“Vitendo uhukumiwa kutokana na makusudio; kila mtu hutunzwa kulingana na makusudio yake. Hivyo mtu yoyote mwenye kuhama kwaajili ya Mungu na Mtume Wake basi uhamaji wake utanakiliwa kwasababu ya Mungu na Mtume Wake. kinyume chake, mtu akihama kwaajili ya sababu ya kidunia au kuoa, basi kuhama kwake kutakuwa na thamani ya alichokusudia.” (Saheeh Al-Bukhari)
Mtume pia amesema:
“Mtu yoyote mwenye kumuamini Mungu na Siku ya Mwisho, anatakiwa aseme kitu kizuri au akae kimya.”
Simulizi hizi mbili za juu zinaonyesha wazi kuwa Mtume ameongea maneno hayo. Kwa hivyo, hizi zinajulikana kama simulizi zake.
Vitendo vya Mtume Muhammad
Matendo yake yanamaana chochote alichokifanya, kama ilivyo thibitishwa na Sahabah (Maswahaba). Kwa mfano, Hudhayfah ameeleza kuwa Kila mtume akiamka usiku, alikuwa akisafisha meno yake na mswaki. Pia Aishah ameeleza kuwa Mtume anapenda kufanya kila kitu katika upande wake wa kulia - kuvaa viatu, kutembea, kujisafisha, na mambo yake yote kiujumla.
Idhini ya Kimya Kimya ya Mtume Muhammad
Idhini yake ya kimya kimya inamaana hapingi au kujali alichokiona, kusikia au kujua vitendo au misemo ya maswahaba zake. katika kipindi kimoja, kwa mfano, Mtume alijifunza vitendo vya baadhi ya maswahaba kutoka kwa maswahaba wengine. Mara baada ya vita ya Khandaq, Mtume Muhammad aliwaamuru maswahaba wake kwenda haraka kwenye kabila la Banu Quraydah, aliwahimiza kuharakisha ili angalau waswali Asr (swala ya jioni) kule. Baadhi ya maswahaba waliitikia haraka na kuondoka bila kuswali Asr. Walifika jioni, wakaweka kambi na kuswali Asr- baada ya jua kuzama. Muda huo huo, kundi lingine la maswahaba walitengeneza shauri lao kitofauti. Walifikiri Mtume aliwahimiza wafike haraka tu uko wanakokwenda, badala ya kuchelewesha Asr mpaka jua kuzama. Hivyo, waliamua wakae Madinah mpaka wawe wameswali Asr. Maramoja baada ya hapo walielekea kwenye kabila la Banu Quraydhah. Pindi Mtume alipoambiwa jinsi kila kundi lilivyoitikia tofauti maelekezo yake, aliyakubali mawazo ya wote.
Tabia za Kimwili na Kimaadili za Mtume Muhammad
Kila kitu kilichothibitishwa kinachosimuliwa kumuhusu Mtume kufanya na sifa zingine za mwili pia zinahusika katika maana ya Sunnah. Umm Ma’bad anasimulia aliona nini kwa Mtume. Anasema:
“Nilimuona mwanaume, uso wake uling'aa na mwanga mkali, sio mwembamba wala mnene, msafi na mtanashati. Macho yake yalikuwa na kiini cheusi yakiwa na kope ndefu. Sauti yake ilikuwa ya kupendeza na shingo yake ilikuwa ndefu. Alikuwa na ndevu nyingi. Nyusi zake ndefu zilikuwa zimepinda vizuri na zimeungana. kwa ukimya, alibaki kuwa na adabu, kuamrisha kwa hofu na kwa heshima. Kama akiongea, mazungumzo yake yalikuwa mazuri. kwa watu wote alikuwa ni mtanashati na msafi, hata akija kwa mbali. Ana kwa ana, alikuwa wa kipekee na kupendeza. haiba ya ufasaha, maongezi yake yalikuwa mazuri. Hoja zake zilikuwa zina mantiki kama zilikuwa safu za vito. Hakuwa mrefu wala mfupi, bali wa katikati. Katika watatu, anaonekana kwenye kun'gaa na imara. alikuwa na maswahaba ambao walimuheshimu. Alipokuwa akiongea, walikuwa wakimsikiliza kwa umakini mkubwa. Pindi akitoa amri, walikuwa kwa haraka wanatekeleza. Walijikusanya kwake wakimlinda. Hakuwahi kukunja uso wala kuongea upuuzi.” (Hakim)
Pamoja na wasifu wake, Masahaba zake wanasimulia tabia zake na tabia zake kwa watu. Anas anasimulia:
“Nimemtumikia Mtume wa Allah, amani iwe juu yake, kwa miaka kumi. kipindi iko chote, hajawahi kuongea sana zaidi ya ‘Oof’kama nikifanya kitu kibaya. Hajawahi kuniuliza, kama nimeshindwa kufanya kitu, ‘Kwanini haujafanya?,’ na hajawahi kuniambia, kama nimefanya kitu kibaya, ‘Kwanini umefanya?’”
Kutoka juu tumeona vizuri kuwa neno Sunnah linapoonekana katika muktadha wa jumla humuhusisha Mtume Muhammad hii inajumuisha chochote kinachosimuliwa kuhusu Mtume na kimethibitishwa kuwa kinatoka kwake. Pindi Muislamu anapojifunza uthibitishwaji wa simulizi zozote anawajibu wa kuufuata. Utiifu huu ni walazima kwa Mungu kama Alivyoeleza:
“... Mt'iini Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wala msijiepushe naye, nanyi mnasikia.” (Kurani 8:20)
Wakati mwingine,baadhi ya Waislamu wanashangaa watu wanaposema Sunnah ni kitu kilichopendekezwa tu na siyo cha lazima. Hivyo wanahitimisha kuwa tunatakiwa kufuata Kurani na siyo Sunnah. Hoja kama hiyo inaleta kutokuelewana Wasomi wa Kiislamu wa sheria hutumia neno Sunnah kuonyesha yepi yamethibitishwa kuanzishwa na Mtume Muhammad aidha ambayo hayakufanywa ya lazima na Mungu.
Wanazidi kushikilia kuwa hii inajumuisha misemo yoyote ya Mtume Muhammad ambapo aliwahimiza kufanya jambo flani na kuwapongeza wale ambao wamedumisha sifa hiyo. Hivyo kwao, neno Sunnah linahusisha nini kilicho “pendekezwa” na siyo cha lazima (fard au wajib).
Kutoka juu, tunaweza kuona vizuri kuwa neno Sunnah linachukua maana tofauti tofauti pindi linapotumiwa katika nidhamu za Uislamu.
Ongeza maoni