Dhana Kumi Kubwa kuhusu Uislamu (sehemu ya 2 kati ya 2): Dhana Zaidi Zimekamatwa

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Muendelezo wa sehemu ya kwanza, ambayo tumeangalia dhana ya nne hadi ya kumi.

  • Na Aisha Stacey (© 2014 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 04 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 6,015 (wastani wa kila siku: 6)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

4.Uislamu hauvumilii itikadi na imani ya watu wengine.

TopTenMyths2.jpgKihistoria mara zote Uislamu umekuwa ukiheshimu kanuni za uhuru wa Kidini. Kurani na nakala zingine za kanuni ikiwemo tamaduni za Mtume Muhammad uhubiri uvumilivu juu ya dini nyingine na wasio amini. Wasiokuwa Waislamu wanaoishi katika utawala wa Waislamu wanaruhusiwa kuabudu na hata kuwa na mahakama zao.

5.Uislamu umeanza tu miaka 1400 iliyopita.

Mzizi wa neno Uislamu (sa-la-ma) ni mzizi sawa uliochanganya na Neno la Kiarabu lenye maana amani na ulinzi - salam. Kwa msingi, Uislamu unamaana, Utii kwa Mungu na ikijumuisha amani na usalama inayokuja kwa kuishi kulingana na mapenzi ya Mungu. Hivyo katika historia mtu yoyote anaye abudu Mungu mmoja (monothiezimu) anachukuliwa kuwa Muislamu. Binadamu amekuwa akiishi katika Uislamu tangu kuumbwa kwa Adam. Tangu kale Mungu ametuma Manabii na Mitume kuwaongoza na kuwafunza watu wao. Ujumbe wa Mitume hawa wote mara zote ilikuwa kuna Mungu Mmoja tu wa Kweli na Yeye pekee ndiye anapaswa kuabudiwa. Mitume hii ikianzia na Adam na ikiwemo Noah, Abraham, Moses, David, Solomon, Yohana Mbatizaji na Yesu, amani iwe juu yao. Mungu amesema kwenye Kurani:

"Na hatukumtuma kabla yako(Wewe Muhammad Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipo kuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu.’" (Kurani 21:25)

Ila, ujumbe wa mitume hii labda ulipotea au kupotoshwa baada ya muda. Hata vitabu vya karibuni, Torati na Injili vimechafuliwa na hivyo kukosa uaminifu wa kuwaongoza watu kwenye njia sahihi . Hivyo miaka 600 baada ya Yesu, Mungu aliufufua ujumbe uliopotea wa mitume iliyopita kwa kumtuma Mtume Muhammad kwa Ufunuo Wake wa mwisho, Kurani Tukufu, kwa binadamu wote. Mungu Mtukufu amesema kwenye Kurani:

" Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui. " (Kurani 34:28)

"Na anaye tafuta Dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye kukhasiri. " (Kurani 3:85)

6.Waislamu hawamuamini Yesu.

Waislamu wanawapenda mitume wote; kumkataa mmoja ni kukataa nguzo za Uislamu. Kwa maneno mengine, Waislamu huwamini kwenye, upendo, na kumpenda Yesu, ambae anajulikana kwa Kiarabu kama Eesa. Tofauti ni kuwa Waislamu wanaelewa majukumu yake kulingana na Kurani, na tamaduni na hadithi za Mtume Muhammad. Hawamini kuwa Yesu ni Mungu, wala kuwa mtoto wa Mungu na hawaamini katika wazo la Utatu.

Sura tatu za Kurani zimeeleza maisha ya Yesu, mama yake Mariamu na familia zao, na kila mmoja ameeleza wasifu wa maisha ya Yesu ambayo hayapatikani kwenye Biblia. Waislamu huwamini alizaliwa kiajabu bila baba kwa bikra Mariamu na hakuwai kujiita mwana wa Mungu au kusema aabudiwe. Waislamu pia huwamini Yesu atarudi katika siku za mwisho.

7.Mtume Muhammad aliiandika Kurani.

Dai hili liliwekwa kwa mara ya kwanza na wapinzani wa Mtume Muhammad. Walikuwa na tamaa kubwa ya kulinda maslai yao ambayo yalikuwa yamefunikwa na Uislamu na walijaribu kutia shaka kuhusu Uandishi wa Utukufu wa Kurani.

Kurani ilifunuliwa kwake Mtume Muhammad, kwa malaika Gabriel, katika kipindi cha miaka 23. Mungu Mwenyewe anayaeleza madai ya Kurani yenyewe.

"Na wanapo somewa Aya zetu zilizo wazi, walio kufuru husema juu ya haki inapo wajia: Huu ni uchawi dhaahiri. Au wanasema: Ameizua mwenyewe!’..." (Kurani 46:7–8)

Katika kuongezea kwenye hili Mtume Muhammad hakuwa msomi, hivyo kuwa hakujua kusoma wala kuandika. Mungu amelitaja hili kwenye Kurani.

"Na wewe hukuwa kabla yake unasoma kitabu chochote, wala hukukiandika kwa mkono wako wa kulia…" (Kurani 29: 48)

Kurani imejaa ukweli mwingi, hivyo ili kuthibitisha Mtume Muhammad hakuandika Kurani tunauliza imekuwaje mtu wa karne ya saba K.W.K kujua vitu ambavyo sasa hivi vinakubaliwa kuwa ukweli kisayansi. Aliwezaje kujua mawingu ya mvua na mvua ya mawe jinsi inavyojitengeneza, au ulimwengu unatanuka? Aliwezaje kuelezea kwa taarifa sahihi jinsi kijusi kinavyokuwa bila uvumbuzi wa kisasa kama vile mashine ya utrasaundi?

8.Mwezi mwandamo ni alama ya Uislamu.

Jamii ya Waislamu wenye kuongozwa na Mtume Muhammad hawakuwa na alama. Wafanyabiashara na wanajeshi walitumia bendera kwa sababu za utambuzi ila ilikuwa rangi ang'avu kikawaida nyeusi au kijani. Waislamu hawana alama inayowakilisha Uislamu kama Msalaba unavyo wakilisha Ukristo au Nyota ya David ikiwakilisha Uyahudi.

Alama ya mwezi muandamo in historia inayohusiana na Waturuki na kabla ya Uislamu ilikuwa kwenye sarafu zao. Mwezi muandamo na nyota imeingiliana katika ulimwengu wa Kiislamu pindi Waturuki walipoichukua Constatinople (Istanbul) ndani ya 1453 K.W.K. Walichagua kuchukua bendera iliyokuwepo na alama na kuweka alama ya Utawala wa Ottoman. Tangia kipindi hicho mwezi muandamo umekuwa ukiigwa na mataifa mengi ya Kiislamu na bila ukweli ikaja kujulikana kama alama ya imani ya Uislamu.

9.Waislamu humwabudu mungu mwezi.

Watu walio pumbazwa muda mwingine wanamlenga Allah kama tafsiri ya sasa ya mungu wa zamani wa mwezi. Ubainishaji huu siyo wa kweli. Allah ni jina moja wapo la Mungu na anakusudiwa kwa jina lake kwa watu wote wenye kuongea Kiarabu ikiwemo idadi kubwa ya Wakristo na Mayahudi. Allah hausiani na ibada ya kuabudu mwezi au miungu ya mwezi.

Kuna taarifa chache kuhusu dini ya Waarabu kabla ya kuja Mtume Abraham Ila hakuna shaka kuwa Waarabu kimakosa walikuwa wakiabudu masanamu, maiti, miti, na mawe. Waliojulikana sana walikuwa Manat, al-Lat, na al-Uzza, ila hakuna ushahidi unao onganisha miungu ya mwezi au mwezi.

10.Jihad inamaana ya vita Takatifu.

Neno la kiarabu lenye kumaanisha vita siyo jihad. Matumizi ya maneno ‘vita takatifu’ kwa watu wasiopata taarifa litakuwa lina chimbuko lake katika kutumia msemo ndani ya Ukristo kipindi cha Vita takatifu ya Msalaba. Neno Jihad ni neno la Kiarabu likiwa na maana ya harakati au Kujitahidi. Mara nyingi imekuwa ikielezwa kuwa na viwango kadhaa. Kwanza, harakati za ndani dhidi ya mtu mwenyewe katika kujitahidi kuwa karibu na Mungu. Ya pili ni harakati za kujenga jamii ya Kiislamu kwa misingi ya usawa na haki za binadamu. Ya tatu ni jeshi au harakati za mapambano.

Harakati za mapambano zinaweza kuwa za kujihami au kuhami. Jihad ya kujihami inapiganiwa ardhi ya Muislamu ikivamiwa ikiwa maisha ya watu, mali zao au heshima kuwa hatarini. Hivyo Waislamu wanajibu mabigano kwa adui mvamizi katika kujilinda. Katikajihad ya kujihami wale watu wanapigania kwa wale wanaopinga kuanzishwa kwa utawala wa kiislamu na uislamu kuwafikia watu. Uislamu ni rehema kwa watu wote na ulikuja kuwatoa watu kutoka kwenye kuabudu mawe na watu na kumwabudu Mungu Mmoja wa kweli, kutoka katika dhuluma na uonevu wa kitamaduni, watu na mataifa kuwa sawa sawa na haki ya Uislamu. Pindi Uislamu utakapo pelekwa kwa watu, hakutakuwa na ulazima wa kuukubali – ni jukumu la watu.

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.