Maswali Makuu (Sehemu 1 za 3): Ni Nani Aliyetuumba?

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Majibu ya Kiislamu ya kwanza ya baadhi ya “Maswali Makuu” katika Maisha ambayo binadamu wote hatimaye huuliza, Ni Nani Aliyetuumba?

  • Na Laurence B.  Brown, MD
  • Iliyochapishwa mnamo 24 Jan 2022
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 2
  • Imetazamwa: 7,019 (wastani wa kila siku: 7)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

The_Big_Questions_(part_1_of_3)_001.jpgWakati fulani katika maisha yetu, kila mtu anajiuliza maswali makuu: “Ni nani aliyetuumba,” na “Kwa nini tuko hapa?”

Kwa hivyo ni nani aliyetuumba? Wakanaji Mungu wanasema Mshindo Mkubwa na mageuzi, huku wengine wote wanamzungumzia Mungu. Wale wanaojibu “Sijui” ni Wakanaji Mungu kwa makusudi, si kwa sababu wanakataa kuwepo kwa Mungu, bali kwa sababu wanashindwa kuthibitisha uwepo wake. Sasa, Mshindo Mkubwa unaweza kueleza asili ya ulimwengu, lakini hauelezi asili ya wingu la vumbi la kwanza. Wingu hili la vumbi (ambalo, kwa mujibu wa nadharia, limeungana na kisha kulipuka) lilipaswa kutoka mahali fulani. Isitoshe, lilikuwa na vipengele vya kutosha kutengeneza sio kundi letu la nyota tu, bali mabilioni ya makundi mengine ya nyota katika ulimwengu unaojulikana. Basi, hilo lilitoka wapi? Nani, au nini, iliunda wingu la vumbi la kwanza?

Vile vile, mageuzi yanaweza kueleza rekodi ya kisukuku, lakini hayawezi kueleza kiini ya maisha ya binadamu; nafsi. Sisi sote tuna nafsi moja. Tunahisi uwepo wake, tunaongelea kuwepo kwake na wakati mwingine kuomba wokovu wake. Lakini ni wenye dini tu ndio wanaweza kueleza ilitoka wapi. Nadharia ya uteuzi ya kiasili inaweza kueleza mambo mengi ya maisha yanayoonekana, lakini inashindwa kueleza nafsi ya binadamu..

Zaidi ya hayo, mtu yeyote anayechunguza utata wa maisha na ulimwengu hawezi kufanya mengi zaidi ya kushuhudia ishara na dalili za Muumba.[1] Ikiwa watu wanatambua ishara hizi ni jambo lingine—kama msemo wa kale unavyosema; kukataa sio mto tu nchini Misri. Hoja ni kwamba tukiona uchoraji, tunajua kuna mchoraji. Tukiona uchongaji, tunajua kuna mchongaji; tukiona sufuria, mfinyanzi. Hivyo tunapotazama uumbaji, je, hatupaswi kujua kuna Muumba?

Dhana ya kwamba ulimwengu ulilipuka na kisha ukatengenezeka kwa ukamilifu na uwiano kutokana na matukio ya kiholela na uteuzi wa kiasili ina tofauti ndogo na pendekezo la kwamba, kwa kuangusha mabomu ndani ya takataka, moja kati ya mabomu hizi italeta kila kitu pamoja na kuunda gari la Mercedes kamili.

Kama kuna jambo moja tunajua kwa uhakika, ni kwamba bila udhibiti, mifumo yote huharibika na kuchanganyika. Hata hivyo, Nadharia za Mshindo Mkubwa na mageuzi zinapendekeza kinyume kabisa, - msukosuko huu ulizua ukamilifu. Je, si jambo la busara zaidi kusema kwamba Mshindo Mkubwa na mageuzi yalikuwa matukio yaliyodhibitiwa? Yaliyodhibitiwa, yaani, na Muumba?

Mabedui wa Arabia husimulia hadithi ya mhamaji anayepata jumba la kufurahisha karibu na chemchemi katikati ya jangwa. Anapouliza jinsi ilivyojengwa, mmiliki anamwambia iliundwa na nguvu za kimaumbile. Upepo uliunda miamba na kuivuma hadi kwa eneo la chemchemi hili, halafu ukaiweka pamoja kutengeneza jumba hili la kifalme. Kisha ukapiga mchanga na mvua ndani ya nyufa ili kuyaimarisha pamoja. Kisha, ulivuma vipande vya pamba ya kondoo pamoja kuunda mazulia na matandiko, na kuleta kuni pamoja na kuunda samani, milango, na madirisha, na kuziweka kwa jumba hilo katika maeneo yanayofaa. Mapigo ya Umeme yaliyeyusha mchanga na kuunda vioo na kuviweka kwenye fremu za madirisha, na kisha kubadilisha mchanga mweusi kuwa chuma na kuiweka kwa uzio na mlango kwa usawa kamili na ulinganifu. Mchakato huo ulichukua mabilioni ya miaka na ulifanyika tu mahali hapa duniani—kibahati tu.

Tunapomaliza kukodoa macho, tunapata uhakika. Ni wazi kwamba jumba hilo lilijengwa na kubuniwa, na halikutokea kibahati. Ni kitu gani (au mtu yupi), basi, tunapaswa kusema kuwa ndiye alisababisha asili ya vitu vya utata mkubwa zaidi, kama vile ulimwengu wetu na sisi wenyewe?

Hoja nyingine ya kukataa dhana ya Uumbaji inalenga kile ambacho watu wanaona kuwa ni kutokamilika kwa uumbaji. Hizi ni kama “Jinsi gani kunaweza kuwa na Mungu ilhali vitu kama hiki na kile vinatokea?”. Suala linalojadiliwa linaweza kuwa lolote kuanzia maafa ya kimaumbile hadi kasoro za kuzaliwa, kuanzia mauaji ya halaiki hadi saratani ya nyanya wa mtu. Hiyo siyo hoja. Hoja ni kwamba kumkataa Mungu kulingana na kile tunachokiona kuwa ni udhalimu wa maisha ni kufikiri kwamba Mungu hangetengeneza maisha yetu kuwa kitu chochote isipokuwa kamilifu, na kungekuwa na uimara na haki duniani.

Hmm … je, hakuna chaguo jingine?

Tunaweza kwa urahisi kupendekeza kwamba Mungu hakutengeneza maisha duniani kuwa pepo, bali ni mtihani, adhabu au tuzo ambazo zinapaswa kutokea katika maisha ya pili, ambapo Mungu anaweka haki Yake ya mwisho. Kwa kuunga mkono dhana hii tunaweza kuuliza ni kina nani waliopata dhuluma zaidi katika maisha yao ya kidunia kuliko wapendwa wa Mungu, ambao ni manabii? Na ni nani tunatarajia kuchukua vituo vya juu zaidi peponi, ikiwa sio wale wenye imani ya kweli wanapokabiliwa na shida za kidunia? Kwa hivyo kuteseka katika maisha haya ya kidunia sio lazima kutafsiriwa kuwa ni hasira ya Mungu, na maisha ya kidunia yenye furaha haimaanishi kuwa maisha ya baadaye yatakuwa hivyo.

Natumai kuwa, kutokana na hoja hii, tunaweza kukubaliana kuhusu jibu la “swali kuu” la kwanza. Ni nani aliyetuumba? Je, tunaweza kukubaliana kwamba ikiwa tumeumbwa, Mungu ndiye Muumba?

Kama hatuwezi kukubaliana juu ya hoja hii, pengine hakuna haja kubwa ya kuendelea. Hata hivyo, kwa wale wanaokubali, tuendelee kwenye “swali kuu” la pili-kwa nini tuko hapa? Nini, kwa maana nyingine, ndiyo kusudi la maisha?

Hakimiliki © 2007 Dkt. Laurence B. Brown; imetumika kwa idhini.

Dr. Brown ni mwandishi wa The Eighth Scroll, kilichoelezwa na Seneta wa Jimbo la Carolina Kaskazini Larry Shaw kama, “Indiana Jones inakutana na The Da Vinci Code. The Eighth Scroll ni kitabu kinachokufanya ushike pumzi, kisichoweza kuwekwa chini baada ya kuanza, kinachopinga maoni ya Kimagharibi kuhusu ubinadamu, historia na dini. Hakina mfano, na ndicho kitabu bora katika kategoria chake!” Dr. Brown pia ni mwandishi wa vitabu vitatu vya kielimu vya ulinganisho wa kidini , Misgod'ed, God'ed, na Bearing True Witness (Dar-us-Salam). Vitabu na makala yake yanaweza kupatikana kwenye tovuti yake,www.EighthScroll.com na www.LevelTruth.com, na yanaweza kununulika katika www.Amazon.com.



Vielezi-chini:

[1] Kufikia hapa, na tukiacha mwelekeo wote wa kidini wa mwandishi kando, ninapendekeza kwa moyo wa dhati usomaji wa A Short History of Nearly Everything, ya Bill Bryson.

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.