Kwanini Uislamu?
Maelezo: Kuanzia Waliosilimu kwenye Uislam hadi wote watafuta ukweli.
- Na Laurence B. Brown, MD
- Iliyochapishwa mnamo 06 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 26 Mar 2023
- Ilichapishwa: 2
- Imetazamwa: 5,832 (wastani wa kila siku: 5)
- Imekadiriwa na: 106
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Ngoja tuzungumze kwa uwazi. Kamwe wasiokuwa Waislamu wanausoma Uislamu mpaka wachoke na dini zingine. Ni baada tu ya kutokuridhishwa na dini zinazofanana nazo, kwa maana ya Uyahudi, Ukristo na mitindo“-isms”—Buddhism, Taoism, Hinduism (na, kama mwanangu mdogo wa kike alipoongezea, “tourism”)—wanaangalia sasa Uislamu.
Labda dini zingine hazijibu maswali makubwa ya maisha, kama vile “Nani ametuumba?” na “Kwanini tupo hapa?” Labda dini zingine hazisuluhishi udhalimu wa maisha kwa haki na Muumba. Labda tunaona unafiki kwa viongozi, ubatili wa madhehebu katika ukweli, au uchafuzi katika maandiko. Kwa sababu yoyote, tunaona mapungufu ya dini tulizotembelea, na kuangalia kwengine. Na ya mwisho “sehemu nyingine” ni Uislam.
Sasa, Waislamu wanaweza wasipende kusikia mimi nikisema kuwa Uislamu ni “mwisho wa sehemu zingine.” Ila iko hivyo. Japokuwa Waislamu wanachukua robo hadi moja ya tano katika idadi ya watu duniani, vyombo vya habari visivyo vya Kiislamu vinaipa sifa mbaya dini ya Kiislamu hivyo wasiokuwa Waislamu ni wachache wanaiona dini katika mtizamo chanya. Hiyo, ni kawaida ya watafuta dini ya mwisho wachunguze.
Tatizo lingine ni kwamba katika muda ambao wasio kuwa Waislamu wanapouchunguza Uislam, dini zingine huongeza hofu kwao: iwapo maandiko “yalitolewa na Mungu” tuliyoyaona yamechafuliwa, inawezaje kuwa maandiko ya Kiislamu kuwa na utofauti? Kama walaghai wamebadilisha dini kukidhi matamanio yao, tutafikiriaje jambo kama hilo lisitokee kwenye Uislam?
Jibu linaweza kutolewa katika mistari michache, ila inahitaji kitabu kuelezea. Jibu fupi ni hili: Kuna Mungu. Yeye ni mwaminifu na mwadilifu, na anataka tupate malipo ya peponi. Ila, Mungu ametuleta katika dunia hii iwe kama mtihani, kuwatoa wanaostahili kutoka kwa wasiostahili. Na tutapotea kama tukiachwa katika vifaa vyetu. Kwa nini? Kwa sababu hatujui Anataka nini kwetu. Hatuwezi kuzunguka katika haya maisha bila Muongozo wake, na pia, Ametupa muongozo katika hali ya ufunuo.
Kweli, dini za mwazo zimechafuliwa, na hiyo ndiyo sababu moja wapo ya kuwa na mtiririko wa ufunuo. Jiulize: Mungu angetuma ufunuo mwingine kama maandiko yaliyopita yapo safi? Iwapo maandiko yaliyopita hayapo safi, mwanadamu angehitaji ufunuo mwingine, kumuweka katika njia iliyo nyooka ya muundo wake.
Kwa hivyo tunafaa kututarajia maandiko yaliyopita kuwa yamechafuka, na tutarajie ufunuo wa mwisho kuwa msafi na usiobadilishwa, sababau hatuwezi kuona Mungu mwenye Upendo akituacha tupotee. Tunachoweza kufikiria ni Mungu kutupatia maandiko, na wanadamu wameyachafua; Mungu ametupa maandiko mengine, na mwanadamu ameyachafua tena … na tena, na tena. Hadi Mungu alipotuma ufunuo wa mwisho na Kuweka ahadi ya kuhifadhi hadi mwisho wa muda.
Waislamu wanaamini ufunuo huu wa mwisho ni Kurani. Unafikiria … ni ya thamani kuiangalia. Sasa turudi kwenye kichwa cha nakala: Kwanini Uislam? Kwanini tuamini Uislam kuwa dini ya kweli, dini yenye ufunuo msafi na wa mwisho?
“Oh, niamini mimi.”
Sasa, mara ngapi umesikia mstari huo? Mchekeshaji maarufu alikuwa anapenda kusema kuwa watu wa miji tofauti wanatukanana kwa njia tofauti. Huko Chicago, wanatukanana kwa njia hii, ndani ya Los Angeles wanatukanana kwa njia ile , ila ndani ya New York wanasema tu, “Niamini mimi.”
Hivyo usiniamini mimi—muamini Muumba wetu. Soma Kurani, soma vitabu na chunguza kwenye tovuti nzuri. Ila chochote utakachofanya, anza, maanisha, na omba kwa Muumbaji wetu akuongoze.
Maisha yako yanaweza yasitegemee, ila roho yako kwa hakika hutegemea.
Haki miliki © 2007 Laurence B. Brown; inatumiwa kwa ruhusa.
Kuhusu mwandishi:
Laurence B. Brown, MD, kwa mawasiliano BrownL38@yahoo.com. Ndiye mwandishi wa Amri ya Kwanza na Mwisho (Chapisho la Amana) na Kutoa Ushahidi wa Kweli (Dar-es-Salam). Vitabu vijavyo vya kusisimua, The Eighth Scroll, na toleo la pili la Amri ya Kwanza na Mwisho, imeadikwa tena kwenda MisGod'ed na mwendelezo wake, God’ed.
Ongeza maoni