Vyanzo vya Uislam: Kurani na Sunnah (sehemu ya 1 kati ya 2)
Maelezo: Dini ya Uislamu imejengwa na Kurani (Neno la Mungu) na Sunnah (mafundisho na sifa za Mtume Muhammad). sehemu ya 1: Kurani: Chanzo cha kwanza cha Uislam.
- Na islaam.net
- Iliyochapishwa mnamo 06 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,386 (wastani wa kila siku: 4)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Ufunua wa mwisho wa neema ya Mungu kwa mwanadamu, hekima ya mwisho, na uzuri wa mwisho wa wazo: kwa kifupi, neno la Mungu. Hivi ndivyo Msomi wa Kijerumani, Muhammad Asad, pindi alipoielezea Kurani. Iwapo mtu angelimuuliza Muislam yoyote kuifafanua, kuna uwezani mkubwa wakusema maneno sawa. Quran, kwa Muislam, ni takatifu, neno la Mungu lisilo na mfano. Ilifunuliwa na Mungu Mtukufu, kwa kupitia njia ya Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake. Mtume mwenyewe hakuwa na jukumu la kuiandika Kurani, alikuwa ni Mjumbe tu, akirudia maono ya Mtukufu Muumba:
“Wala hatamki kwa matamanio.Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa; .” (Kurani 53:3-4)
Kurani ilifunuliwa kwa Kiarabu, kwa Mtume Muhammad, katika kipindi cha miaka ishirini na tatu. Imeundwa katika mdindo wa kipekee, kwamba haiwezi kuchukuliwa kama shairi au nathari, ila kwa jinsi flani ni mchanganyiko wa vyote. Kurani haina mfananisho wake; haiwezi kuigwa wala kunakiliwa, na Mungu Mtukufu ametoa mtihani kwa binadamu kujaribu kama wanahisi wanaweza:
“ Ama wanasema ameizua? Sema: Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite (kukusaidieni) muwawezao, isipo kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnasema kweli.” (Kurani 10:38)
Lugha ya Kurani hakika ni ya mafumbo, usomaji wake unavutia, kama mmoja ya msomi asiye Muislam alivyo elezea, “kilikuwa kitulizo cha mapigo yangu ya moyo”. Juu ya mtindo wa kipekee wa lugha, Kurani siyo tu inasomeka sana, ila pia ni rahisi kukumbukwa. Katika hali hii ya mwisho imekuwa na jukumu kubwa siyo tu katika uhifadhi wa Kurani,buli hata katika maisha ya kiroho kwa Waislam pia. Mungu mwenyewe amesema,
“Na kwa hakika, Sisi tumeisahilisha Kurani ifahamike (upesi), lakini je, yupo anayekumbuka?” (Kurani 54:17)
Moja ya sifa muhimu ya Kurani ni kwamba imebaki hadi leo, kitabu pekee cha dini ambacho hakijabadilika; kimebaki huru kutoka kwenye uchafuzi wowote. Bwana William Muir ameeleza, “Inawezekana ikawa kitabu pekee duniani kilichokaa karne (kumi na nne) kikiwa na maandishi safi.”The Kurani was written down during the lifetime and under the supervision of the Prophet, who himself was unlettered. Thus its authenticity is unblemished, and is its preservation is seen as the fulfillment of God’s promise:
“Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutakaoilinda.” (Kurani 15:9)
Kurani ni kitabu ambacho kinampa mwanadamu lishe ya kiroho na kiakili anayotamani. Mada yake kuu ikiwemo Mungu kuwa Mmoja, kusudi la uwepo wa mwanadamu, imani na utambuzi wa Mungu, Maisha ya baadae na umuhimu wake. Kurani pia inaweka umuhimu mkubwa wa sababu na uelewa. Ndani ya duara hili la uelewa wa mwanadamu, Kurani inakwenda zaidi katika kuiridhisha akili ya mwanadamu; inasababisha mtu kujitafakari. Tofauti na maandiko mengine, Kuna maswali ya Kurani na utabiri. imejaa ukweli ambao umekuja kutambulika hivi karibuni; Sehemu moja ya kufurahisha ambayo imegunduliwa hivi karibuni ni kuwa na taarifa nyingi za kisayansi katika Kurani, ikiwemo tukio la bigibengi, taarifa za embryolojiko, na taarifa nyingine zinazohusu unajimu baioloji, nk., hakuna taarifa hata moja ambayo haijathibitishwa na vumbuzi za kisasa. Kwa kifupi, Kurani inakamilisha moyo, roho, na akili. Labda wasifu bora wa Kurani ulitolewa na Ali, mpwa wa Mtume Muhammad alipokuwa akifafanua kuwa,
“Ni Kitabu cha Mungu. Ndani yake kuna nakala ya yaliyopita, hukumu ya kile kilichopo kati yenu, na ubashiri wa nini kitakuja baada yenu. ni maamuzi, siyo swala la utani. Yoyote aliye dhalimu na kuipuuza Kurani ataangamizwa na Mungu. yoyote mwenye kutafuta mwongozo kwa wengine bila Mungu atapotezwa. Kurani ni fundo lisilovunjika la muunganiko na Mungu; ni ukumbusho wa hekima na njia iliyo nyooka. Kurani haiwezi kuja kupotoshwa na ndimi; wala haiwezi kubadilika kwa upotovu. Haikinaishi kutokana na utafiti unaorudiwa; Wasomi mara zote wataitaka zaidi. Maajabu ya Kurani hayawezi kuisha. Yeyote mwenye kuongea nayo ataongea ukweli, yoyote atakaye tawala nayo atakuwa muadilifu, na yoyote atakaye ishikaataongozwa katika njia iliyo nyooka.” (Al-Tirmidhi)
Ongeza maoni