Manufaa ya Kusilimu (sehemu ya 3 kati ya 3)

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Tunaendelea na majadiliano yetu kuhusu manufaa ya kusilimu.

  • Na Aisha Stacey (© 2011 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 09 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 5,472 (wastani wa kila siku: 5)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Manufaa ya kusilimu hayahesabiki, hata hivyo tumechagua machache yaliyobora zaidi ukiyalinganisha na mengine.

8. Kusilimu kunajibu maswali yote MAZITO ya maisha.

BenefitsOfConvertingPart3.jpgMojawapo ya manufaa makubwa ya kusilimu ni kwamba hukuondolea ukungu wa kufahamu mambo. Ghafla maisha, na hekaheka zake zote, yanaeleweka kwa urahisi zaidi. Majibu ya maswali mazito yaliyokuwa yakimsumbua mwanadamu kwa maelfu ya miaka yamewekwa wazi sasa. Muda wowote katika maisha yetu, tutakapofika kwenye maporomoko au ukingoni, ama kwenye njia panda, hujiuliza – “Ni haya tu; kweli kuna mengine?” Hapana, haya sio yaliyopo pekee. Uislamu huyajibu maswali na kutuomba tusizingatie sana mali ya hapa duniani bali tuyatazame maisha haya kuwa ni kituo cha mapito katika safari ya maisha ya milele. Uislamu hutoa malengo na madhumuni bayana ya maisha. Kama Muislamu tunaweza kupata majibu katika maneno matakatifu ya Mwenyezi Mungu, kupitia Kurani, na katika kiigizo cha Mtume wa Mwisho Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake.

Kuwa Muislamu kunadhihirisha unyenyekevu kamili kwa Muumba na ukweli kwamba tuliumbwa ili kumuabudu Mwenyezi Mungu Pekee. Hiyo ndiyo sababu iliyotuleta hapa, katika sayari hii inayozunguka kwenye ulimwengu usio na mwisho; kumuabudu Mwenyezi Mungu Pekee. Bila shaka, kusilimu kunatuokoa na dhambi isiyosameheka, ambayo ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu na chochote.

"Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi [Pekee]."(Kurani 51:56)

"...Enyi kaumu yangu! Muabuduni Mwenyezi Mungu. Nyinyi hamna Mungu ila Yeye." (Kurani 7:59)

Hata hivyo, ni lazima isemwe kwamba, Mwenyezi Mungu hahitaji ibada ya mwanadamu. Ingekuwa hakuna mwanadamu hata mmoja anamuabudu Mwenyezi Mungu, isingepunguza utukufu Wake kwa namna yoyote ile, na ikiwa wanadamu wote wangemuabudu Yeye, isingezidisha utukufu Wake kwa namna yoyote ile.[1] Sisi, wanadamu ndio tunahitaji faraja na ulinzi kupitia kumuabudu Mwenyezi Mungu.

9. Kusilimu kunasababisha kila kipengele cha maisha kuwa tendo la ibada.

Dini ya Uislamu iliteremshwa kwa manufaa ya wanadamu wote watakaokuwepo hadi Siku ya Hukumu. Ni njia kamili ya maisha, sio inayofanywa wikendi ama katika sherehe za kila mwaka. Uhusiano wa muumini na Mwenyezi Mungu huwa muda wa saa ishirini na nne kwa siku, siku saba kwa wiki. Haimaliziki haianziki. Kupitia kwa huruma Yake isiyo na kikomo, Mwenyezi Mungu ametupatia mtazamo wa jumla wa maisha; ambao unashughulikia vipengele vyote, vya kiroho, kihisia na kimwili. Hajatuacha peke yetu kupotea gizani lakini Mwenyezi Mungu ametupatia Kurani, kitabu cha mwongozo. Kadhalika, mwenendo sahihi wa Mtume Muhammad ambao unaelezea na kufafanua mwongozo wa Kurani.

Uislamu hutosheleza na kuyasawazisha mahitaji yetu ya kimwili na kiroho. Mfumo huu, uliyoundwa na Muumba kwa viumbe wake, hautarajii tu kiwango cha juu cha tabia, uadilifu na maadili bali pia huruhusu kila tendo la mwanadamu kubadilishwa na kuwa ibada. Kwa hakika, Mwenyezi Mungu anawaamrisha waumini wajitolee maisha yao kwa ajili Yake.

“Sema: ‘Hakika sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.’” (Kurani 6:162)

10. Kusilimu husawazisha kila aina ya uhusiano.

Mwenyezi Mungu anajua kile kinachofaa kwa viumbe Wake. Mwenyezi Mungu ana elimu kamili ya akili ya mwanadamu. Kwa hivyo, Uislamu unafafanua kwa uwazi haki na wajibu tulionao kwa Mwenyezi Mungu, wazazi wetu, mume na mke, watoto, jamaa, majirani, n.k. Hatua hii huleta nidhamu badala ya vurugu, maelewano badala ya mtafaruku na amani mahali pa migongano na migogoro. Kujiunga na Uislamu huruhusu mtu kukabiliana na hali zozote kwa ujasiri. Uislamu unaweza kutuongoza katika hali zote za maisha, za kiroho, kisiasa, kifamilia, kijamii na kishirika.

Tunapotimiza wajibu wetu wa kumtukuza na kumtii Mwenyezi Mungu, moja kwa moja tunakuwa na adabu na viwango vya juu vya uadilifu unaohitajika katika Uislamu. Kujiunga na Uislamu kunamaanisha kujisalimisha na matakwa ya Mungu na hatua hii inahusisha kutukuza na kuheshimu haki za wanadamu wote, viumbe vyote vinavyoishi na hata mazingira. Tunapaswa kumjua Mungu na kujisalimisha Kwake ili kufanya maamuzi yatakayotupatia radhi Yake.

Kwa kuhitimisha, kuna faida moja ya kusilimu inayoifanya kila siku kuwa yenye furaha. Haijalishi ni hali gani ambayo kila Muislamu anajipata kwayo, wapo salama wakifahamu kwamba hakuna lolote katika ulimwengu huu litakalotokea bila ya idhini ya Mwenyezi Mungu. Mitihani, majaribio na ushindi yote hayo ni mambo mazuri na yanapokabiliwa na imani ya Mwenyezi Mungu, yatakuwa ni sababu ya mwisho mwema na kutosheka kwa dhati. Mtume Muhammad alisema, “Hakika mambo ya muumini hushangaza! Yote ni kwa manufaa yake. Ikiwa atapewa wepesi basi hushukuru, na vivyo hivyo hilo ni jambo zuri kwake. Na anapokumbwa na dhiki, huvumilia, na vivyo hivyo ni jambo zuri kwake".[2]



Rejeleo la maelezo:

[1] Lengo la Uumbaji na Dkt Abu Ameena Bilal Phillips.

[2] Saheeh Muslim

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.