Kuukubali Uislamu (sehemu ya 2 kati ya 2): Dini ya Msamaha

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Kuukubali Uislamu kunafuta madhambi yaliyopita.

  • Na Aisha Stacey (© 2010 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 09 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 4,962 (wastani wa kila siku: 4)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Accepting_Islam_(part_2_of_2)_001.jpgTulihitimisha sehemu ya 1 ya makala hii kwa kupendekeza kwamba iwapo mtu anaamini kweli hapana mungu mwingine isipokuwa Allah, anapaswa kuukubali Uislamu mara moja. Kadhalika, tunaweka wazi ya kuwa Uislamu ni dini ya msamaha. Haijalishi ni madhambi mangapi ameyafanya mtu, asiweze kusamehewa. Mwenyezi Mungu ni mwingi wa Kusamehe, Mwingi wa Rehema na Kurani inasisitiza sifa hizi zaidi ya mara 70.

“Na ni vya Mwenyezi Mungu vyote vilivyomo katika Mbingu na vilivyomo katika Ardhi. Yeye humsamehe na humuadhibu amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Msamehevu, Mwenye kurehemu.” (Kurani 3:129)

Hata hivyo, kuna dhambi moja ambalo Mungu hatolisamehe na hilo ni dhambi la kumshirikisha Mwenyezi Mungu na washirika au wasaidizi wengine. Muislamu anaamini kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja, hana washirika, vizazi, au wasaidizi. Yeye ndiye Pekee anayestahiki kuabudiwa.

“Sema (Ewe Muhammad), Yeye Mwenyezi Mungu ni wa pekee. Mwenyezi Mungu Mkusudiwa (Mwenye kutosheleza mahitaji yote, Ambaye viumbe vyote humhitaji, Hali na wala hanywi). Hakuzaa wala hakuzaliwa; Wala hana anayefanana naye hata mmoja.” (Kurani 112)

“Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye...” (Kurani 4:48)

Inaweza kuonekana ni jambo la ajabu kusema kuwa Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa Rehema, na kusisitiza kuwa Uislamu ni dini ya msamaha huku pia ukisema kuna dhambi moja halisameheki. Hili sio jambo geni ama dhana isiyo na mashiko pale unapoelewa kuwa dhambi hili kubwa haliwezi kusameheka iwapo mtu atakufa bila kutubia kwa Mwenyezi Mungu. Wakati wowote, hadi mtu mwenye dhambi avute pumzi yake ya mwisho, anaweza kumgeukia Mungu kwa dhati na kuomba msamaha, akijua kwamba hakika Mungu ni Mwingi wa Rehema na Mwenye kusamehe. Toba ya kweli inauhakikisha msamaha wa Mungu.

“Waambie wale walio kufuru, wakikoma (kukufuru) watasamehewa yaliyo kwisha pita...” (Kurani 8:38)

Mtume Muhammad, rehema na amani za Mwenyezi Mungu zimshukie, alisema: "Mwenyezi Mungu atakubali toba ya mja wake maadamu mtitigo wa kifo bado haujafika kooni mwake.”[1] Kadhalika, Mtume Muhammad alisema, "Uislamu hufuta yaliyokuja kabla yake (madhambi)”.[2]

Kama ilivyojadiliwa katika makala iliyopita, mara kwa mara mtu anapotafakari kuukubali Uislamu huchanganyikiwa au hata kuaibika na madhambi mengi waliyoyatenda wakati wa maisha yao. Watu wengine hushangaa ni vipi wanaweza kuwa watu wema, wenye maadili ilhali katika giza hujificha wakitenda madhambi yao na uhalifu wao.

Kuukubali Uislamu na kutamka maneno yanayojulikana kama Shahada au ushuhuda wa imani, (Nakiri “La ilah illa Allah, Muhammad rasoolu Allah.”[3]), hufuta rekodi kwenye kitabu cha mtu na kuwa safi. Anakuwa kama mtoto mchanga, huru kwa kutokuwa na dhambi kabisa. Ni mwanzo mpya, ambao madhambi ya zamani ya mtu hayawezi kamwe kumshika mtu mateka. Hakuna haja ya kuandamwa na madhambi yaliyotangulia. Kila Muislamu mgeni hutulika mzigo wake wa madhambi na kuwa huru kuishi maisha kulingana na imani ya kimsingi kwamba Mungu ni Mmoja

Pindi mtu akiachiliwa huru na hofu ya kuwa madhambi yao ya zamani au mtindo wao wa maisha unawazuia kuishi maisha mazuri, ndipo njia ya kuukubali Uislamu aghlabu inakuwa rahisi. Kujua kuwa Mwenyezi Mungu anaweza kumsamehe mtu yeyote, kwa lolote, kwa hakika ni tarajio linalofariji. Walakini, kuelewa umuhimu wa kutoabudu kitu chochote au mtu mwingine yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu ni jambo kuu kwa sababu ndio msingi wa Uislamu.

Mungu hakuumba wanadamu isipokuwa wamuabudu yeye peke yake (Kurani 51:56) na kujua jinsi ya kuweka ibada hiyo kuwa safi na isiyochafuliwa ni muhimu. Hata hivyo, maelezo yake aghlabu yatafahamika baada ya mtu kutambua ukweli adhimu wa njia ya maisha ambayo ni Uislamu.

“Na fuateni yaliyo bora kabisa katika yale yaliyo teremshwa kwenu kutoka kwa Mola wenu Mlezi, kabla haijakujieni adhabu kwa ghafla, na hali hamtambui. Isije ikasema nafsi: Ee majuto yangu kwa yale niliyo poteza upande wa Mwenyezi Mungu, na hakika nilikuwa miongoni mwa wanao fanya maskhara.” (Kurani 39:55-56)

Pindi tu mtu anapokubali ukweli wa Uislamu, na hivyo kukubali kwamba hapana mungu ila Mwenyezi Mungu Pekee, ana wakati wa yeye kujifunza kuhusu dini yake. Ana wakati wa yeye kuelewa uzuri wa mvuto na usahali wa Uislamu, pamoja na kujifunza kuhusu mitume na wajumbe wote wa Uislamu akiwemo mtume wa mwisho, Mtume Muhammad. Iwapo angepitisha Mwenyezi Mungu kwamba maisha ya mtu yangemalizika mara tu baada ya kukubali Uislamu inaweza kuonekana kama ishara ya huruma ya Mwenyezi Mungu; mtu safi kama mtoto mchanga atajaaliwa pepo ya milele; kwa rehema ya Mwenyezi Mungu, na hekima Yake isiyo na kikomo.

Wakati mtu anapotafakari kuukubali Uislamu, vizuizi vingi ambavyo alivifikiria sio chochote zaidi ya udanganyifu na hila kutoka kwa Shetani. Ni wazi kwamba mara tu mtu anapochaguliwa na Mungu, Shetani atafanya kila awezalo ili ampotoshe mtu huyo na kuwashambulia kwa minong'ono midogo na wasiwasi. Dini ya Uislamu ni zawadi, na kama vile zawadi nyingine yoyote lazima ikubaliwe, na ifunguliwe kabla ya kudhihirishwa thamani halisi ya yaliyomo kufunuliwa. Uislamu ni njia ya maisha ambayo inafanikisha ndoto ya kupata neema ya milele Akhera. Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, Mmoja Pekee, wa Kwanza na wa Mwisho. Kumjua Yeye ndio ufunguo wa mafanikio na kuukubali Uislamu ni hatua ya kwanza katika safari ya kuelekea Akhera.


Rejeleo la maelezo:

[1] At-Tirmidhi

[2] Saheeh Muslim

[3] Nakiri ya kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu na nakiri kwamba Muhammad ni mtume wa Mwenyezi Mungu. Kwa maelezo zaidi kuhusu Shahada tafadhali bonyeza hapa

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.