Kwanini Waislamu wanawaita wengine kwenye Uislamu?

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Waislamu wanataka kusirikiana kimawazo katika maisha na kila mtu wanae kutana naye. Wanataka wajisikie vizuri kama wao na hii ndio sababu.

  • Na Aisha Stacey (© 2014 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 04 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 3,462 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

WhydoMuslimsCalltoIslam.jpgKama ukigundua kitu kizuri ukajihisi kama unataka kuruka juu na chini, kitu gani cha kwanza utataka kufanya? Iwapo umepata jibu la fumbo na unajua wengine wanajaribu kufanya kitu hicho hicho, utajisikiaje, utafanya nini? Iwapo utagundua maana ya maisha au siri ya ulimwengu, utafanya nini na maarifa hayo? Ikiwa umepata njia ya kuondoa hofu na uzuni na kuibadilisha na furaha ya milele ungefanya nini?

Watu wengi wangeshindwa kuzuia furaha yao na wangetaka kuwaambia watu wengi kadri iwezekanavyo. Wangetaka kuwaambia kila mtu walichokigundua kwa matumaini hao nao wapate msisimko na kufurahi. Na hilo ndilo jibu fupi na dogo la kwanini Waislamu wanawaita watu wengine kwenye Uislamu. Kwa sababu wameshawishika bila kivuli cha shaka kuwa Uislamu ni maana ya maisha, siri ya ulimwengu na funguo ya furaha ya milele zimefungwa kwenye kifurushi kinachoweza kufikiwa na kueleweka na wanataka kila mtu aliye kwenye uso wa dunia kujua hilo.

Ila kuna jibu refu na linajumuisha kutii amri za Mungu, Kufuata hatua za mitume, na kukusanya thawabu kwa matumaini ya kupata amani ya milele na furaha ndani ya Maisha yanayokuja.

Uislamu muda mwingine unaitwa dini ya kuwabadilisha watu. Hii inamaanisha dini inayojaribu kuwashawishi watu kuwa mfumo wao wa imani ndio mfumo sahihi wa imani. Uislamu sio tu una majibu ya maswali yote makubwa ya maisha ila inajumuisha kutokuwa na kizuizi cha nani anaweza kuwa Muislamu. Uislamu ni dini ya sehemu zote, muda wote na watu wote. Hamna mtu anayeweza kuzuiwa katika kujifunza ukweli bila kujali wamelelewa katika dini gani, au kabila gani au nchi wanayotoka.

Mtu akiwa Muislamu, mwanaume au mwanamke yupo sawa sawa na Muislamu mwingine na haijalishi wanatokea wapi, wanaonekanaje au hali gani ya maisha yao na mioyo ilikuwepo kabla ya kuukubali Uislamu. Ukweli kuhusu Mungu na kusudi Lake kwetu, Uumbaji wake, ni kitu ambacho kila mtu anapaswa kikifikia. Hivyo wale wenye kujua wanalazimishwa na Mungu, kuwaambia wengine.

"Na uwe kutokana na nyinyi umma unao lingania kheri na unao amrisha mema na unakataza maovu. Na hao ndio walio fanikiwa." (Kurani 3:104)

"Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora…" (Kurani 16:125)

Watu wengi wanataka kueneza habari njema kuhusu Uislamu na muda huo huo Kukamilisha amri za Mungu. Wasomi wa Kiislamu wanakubali kuwa kuwaita wengine katika njia ya Mungu ni wajibu, hivyo kila aliyeamini anatakiwa achukue kazi yake nzuri, ila kama sehemu kuna idadi ya kutosha ya watu wanafanya hivyo, wengine wanaachiwa kwenye kufanya jukumu hilo.

Kazi hiyo inaitwa da’wah na mtu anayefanya kazi hii anaitwa da’ee. Ila itakuwa vibaya kufikiria kuwa watu flani ndiyo wanapaswa kufanya da’wah. Hakika, kuhubiri kwenye watu wengi kunahitaji mafunzo, ila ukweli ni kwamba Waislamu wote waliofanya mafunzo wanafanya aina ya da’wah kila siku. Tabia zao za kuishi na kushughulikia wengine ni aina bora ya da’wah. Uislamu ni njia ya maisha na watu wakiona juhudi, Upole na haki zilizowekwa kwa Waislamu katika maisha ya kila siku - ni lazima, na inaonekana, ya kuvutia sana. Kuwa mfano ndiyo mfano mzuri wa kuwaita watu kwenye Uislamu. Dini ya rehema na kusamehe watu wanavyoishi kila siku huvutia, na kwa wale watu ambao maisha yao hayana misingi.

Kutoka kwenye sababu za kuwa wangetumaini kufuata hatua za mitume ya Mungu. Kazi zao zilikuwa kuwatoa watu kutoka gizani na kwenda kwenye mwanga. Walijaribu kuwachukua watu kutoka kwenye kutokuamini hadi kuamini ndani ya Umoja wa Mungu. Mtume Muhammad, wa mwisho katika mstari wa Mitume walitumwa kwa binaadamu na Mungu ili kuwaelezea, pamoja na mambo mengine, kuhusu thawabu kubwa za maisha baada ya hapa kwa wale wanaoamini kwa Mungu mmoja na Kumuabudu yeye kwa usahihi.

"Na hatukukutuma ila kwa watu wote, uwe mbashiri, na mwonyaji. Lakini watu wengi hawajui." (Kurani 34:28)

"Ewe Nabii! Hakika Sisi tumekutuma uwe shahidi na mbashiri na mwonyaji. Na mwitaji kumwendea Mwenyezi Mungu kwa idhini yake, na taa yenye kutoa nuru. Na wabashirie Waumini ya kwamba wana fadhila kubwa inayo toka kwa Mwenyezi Mungu." (Kurani 33:45-47)

Sababu nyingine ya kufanya da’wah ni chanzo cha uzuri na thawabu zisizo na mpaka. Mtu akiukubali Uislamu kwa sababu ya ushawishi wa mtu mwingine aliyemuingiza kwenye Uislamu anapokea thawabu kila mara yule mtu anapofanya ibada. Mtume Muhammad amesema, "Yoyote akimwingiza kwenye haki atakuwa na thawabu sawa na atakaye fuata,bila thawabu kwa wote kupungua"[1] Pia amesema, "Kama Mungu amemwongoza mtu kwako kupitia wewe, hii itakuwa bora zaidi ya kuwa na ngamia wekundu."[2] Katika kipindi cha Mtume Muhammad, ngamia walikuwa na thamani na jamii nyekundu ilikuwa na thamani sana.

Waislamu wanaamini kuwa njia pekee ya kufanikiwa katika maisha haya na ya baadae uishi katika dini nayo ni Uislamu. Wanaamini maswali yote makubwa, yale yanayokufanya uwe macho usiku na yale yanayokufanya uote mchana kuhusu maisha ya milele na kukombolewa, yanaweza kujibiwa na Uislamu. Ukweli ni dhana ya muhimu ndani ya Uislamu; wale wasio wakweli wanajua thawabu zao zitapungua haraka sana. Wale walioamini ambao kwa dhati wanataka kusambaza habari njema ya Uislamu wanaweza kuona thawabu zao zikiongezeka hata kama juhudu zao hazikufanikiwa. Ukweli wa Waislamu ni kutaka kila mtu wa sayari hii kumjua na kumpenda Mungu kwa njia wanazojua na Kumpenda Mungu. Na hiyo ndiyo sababu Waislamu wanawaita wengine kwenye Uislamu.



Vielezi-chini:

[1] Saheeh Muslim

[2] Saheeh Bukhari & Saheeh Muslim

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.