Martin Guevarra Abella, Mkatoliki wa Zamani, Ufilipino

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Utafiti wangu usio wa kutafuta ukweli bila kuchoka.

  • Na Martin Guevarra Abella
  • Iliyochapishwa mnamo 14 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 1,623 (wastani wa kila siku: 2)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Naitwa Martin Guevarra Abella. Nilizaliwa Manila, Ufilipino mwaka wa 1966 kwa wazazi Wakatoliki. Nilibatizwa kikatoliki nilipokuwa na umri wa wiki mbili! Ilikuwa nadra kwa familia yangu kukosa misa ya Jumapili na kamwe hatukukosa kusherehekea shughuli mbalimbali za kikristo, au niseme za ”kikatoliki” kama Krismasi, Siku ya watakatifu wote, Juma Takatifu/Pasaka, nk. Nilipokuwa na umri wa miaka 12, nilikuwa Mkatoliki mcha Mungu. Nilihudhuria hadi misa za “Bikira Maria” kila Jumatano na kuomba “Rozari” kila siku.

Nilivutiwa sana na dini na kusoma Biblia nzima, mwanzo hadi mwisho ila haikuimarisha imani yangu ya Kikatoliki bali iliitetemesha imani yangu. Nilianza kujiuliza kuhusu taratibu za Kikatoliki za kuabudu/kuomba picha za kuchongwa na kuwa na Mungu mmoja mwenye utu tatu? Namaanisha, jinsi gani 1=3? Nilihoji sakramenti tofauti za Kanisa Katoliki kama ubatizo, harusi na misa, kwa kuwa zote zilikamilika na “ada” za kila moja. Hata sala kwa ajili ya wafu na baraka kwa wafu kwa kunyunyizia “maji takatifu” zilitozwa ada.

Nikageukia jamaa zangu wa mbali ambao ni makuhani na watawa na niliwauliza kuhusu mambo haya wakati wowote nilipopata fursa. Hawakuweza kujibu maswali yangu na ningeweza kuona kutoka kwa macho yao kwamba walinifukuza tu kama “Mkatoliki ambaye anaimba shairi tofauti, mwiba kwa mfumo na utaratibu uliowekwa.”

Niliuliza kuhusu mafundisho ya limbo (mahali kati ya pepo na moto) kuhusu hali ya watoto wachanga wasiobatizwa/watu ambao hufa bila kuwa huru kutoka “Dhambi ya asili” (kama Wakatoliki wanavyoamini). Wafanyakazi wa matibabu wanaweza kubatiza wagonjwa walio katika hali mbaya (walio karibu kufa) na hii iliaminika kuwa inatosha iwapo mgonjwa/mtu binafsi atakufa. Lakini iwapo mgonjwa ataishi, bado anahitaji kwenda kwa kuhani ili abatizwe! Sasa hii haikuwa na maana, jinsi gani hii itazingatiwa kuwa 'inatosha' katika mfano mmoja, na kwa mwingine haitoshi?

Ndugu na jamaa wa wafu ambao ni matajiri wanaweza kutoa misa zisizo na ukomo ili kuondoa roho za wapendwa wao kutoka “Toharani” (uvumbuzi wa Kanisa Katoliki), na hilo bila shaka ni kwa kutoa mali nyingi, ambayo tena hulipwa kwa Kanisa. Hii iliwaruhusu matajiri kununua njia yao ya “Mbinguni” wakati nafsi “maskini” ambao jamaa zao hawawezi kulipa, hakika huoza toharani au mbaya zaidi kwenda moja kwa moja Jahannamu. Hata kupigwa kwa kengele za kanisa ili kutangaza kifo cha mtu katika jamii kuna ada yake.

Nilipooa nikiwa na umri wa miaka 21 na nikawa na familia yangu mwenyewe, niliacha kuwa Mkatoliki. Niliacha kuhudhuria misa. Nilianza kutafuta dini ya kweli kwa vile sikuamini tena imani ya Kikatoliki. Hii imenisababisha kujifunza imani ya wale wanaodai kuwa Wakristo wa Kiprotestanti - ambao wanaamini kwamba kukubali tu Yesu kama Mwokozi wako binafsi kutakuongoza kwenye wokovu. Waprotestanti wanaamini kwamba “imani pekee” ni muhimu kwa wokovu. Sioni hilo kama jambo la kawaida. Samahani, lakini naamini kwamba hii lazima iwe dini ya wale “wavivu” wasiotaka kufanya matendo mema kwa radhi za Mungu!

Kisha nikasoma Biblia na Mashahidi wa Yehova ambao wanasisitiza kwamba jina la Mungu ni Yehova, licha ya kukubali wenyewe kwamba Yahweh lazima iwe ndio jina sahihi zaidi la Mungu kwani hakuna vokali katika lugha ya Kiebrania!

Pia nikawa mwanachama wa Iglesia Ni Cristo (INC). [1] Tena, nilikuwa na maswali mengi kuhusu taratibu zao ndani ya INC ambayo ilinifanya kuendelea na utafiti wangu kuhusu dini ya kweli.

Ilikuwa wakati wa kazi yangu katika kisiwa cha Mindanao kwa miaka miwili, hasa mji wa Cotabato mwishoni mwa miaka ya 1980 ndipo nilikutana na Uislamu; na ingawa sikupata nafasi ya kujifunza Uislamu, mfiduo huu baadaye ungenivuta kwa Uislamu.

Wakristo wanawaona ndugu zetu Waislamu kama wasumbufu, magaidi wanaooa wake wengi, wauaji, watekaji nyara, wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, walipuaji mabomu na kujitoa muhanga, hadi kuna msemo maalumu unaosema “Muislamu mwema ni Muislamu aliyekufa”. Kuwa Muislamu wakati huu katika maisha yangu ilikuwa jambo ambalo sikutarajia kamwe, kwani niliamini kuwa lazima kuwe na mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu (kutokana na miongo yangu miwili ya kujitahidi katika Ukristo) na kwamba dini haipaswi kuleta vurugu (ingawa pia ninafahamu historia ya Mabaraza ya Kuhukumu Wazushi ya Kikatoliki).

Kwa ujumla, ilinichukua zaidi ya miongo miwili au miaka 23, nilipoacha kutumia Biblia kama kiwango cha kipimo cha kile ninachokiona kinapaswa kuwa dini ya kweli. Nilianza kusoma Qurani Takatifu na kufanya tafiti nyingi kwenye mtandao ili kujua zaidi. Maswali ya kina kabisa katika akili yangu yalijibiwa moja kwa moja wakati nilipojifunza kuhusu tovuti hii, IslamReligion.com. Kuna makala mengi yenye manufaa yanayopatikana kwa urahisi kwa yule anayetafuta ukweli. Mtafutaji wa ukweli lazima awe mwangalifu sana wakati wa kutafuta mtandaoni, kuna tovuti nyingi ambazo zinaeneza uongo, kupotosha ukweli au kujaribu kuenda kinyume na mafundisho ya Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake.

Kwa huruma ya Mungu, macho yangu yalifunguliwa. Jitihada zangu za kutafuta ukweli zilikuwa zimeamka zaidi. Nilitambua somo muhimu sana, si kila Muislamu anashikilia Uislamu kama inavyopaswa; kwa hivyo sio haki kuhukumu Uislamu kulingana na kile ambacho Waislamu wanafanya.

Nilijifunza kwamba Uislamu ni dini ya amani na kwamba vurugu ni mbali zaidi na mawazo ya Muislamu wa kweli. Nilijifunza nguzo sita za imani na taratibu za msingi katika Uislamu. Hatimaye nilikuwa na imani ya kusema Shahada (Ushuhuda wa Imani) na kuingia katika Uislamu.

Maisha sio tu kuzaliwa, kusoma ujuzi wa kidunia katika chuo kikuu fulani, kupata pesa ya kutumia kwa mahitaji ya mtu, na kisha uzee, ugonjwa na hatimaye kifo. Kwa maana kama hii ndiyo maana ya maisha, basi maisha yangekuwa duni kwa sababu “hata kama utashinda mbio ya panya, bado utaendelea kuwa panya mwenye mateso tu.”

Bila kukubali Uislamu na kuishi maisha ya mtu kwa ajili ya radhi za Mungu, maisha yatabaki kuwa yasiyo na maana na yenye kujaa matatizo.



Vielezi-chini:

[1] (http://en.wikipedia.org/wiki/Iglesia_ni_Cristo)

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.