Kuamini kwenye Uwezo wa Mungu

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Imani potofu ya, maamuzi,na uhusiano kati ya Ujuzi wa milele wa Mungu na Uwezo wa tendo la mwanadamu na hatma.

  • Na Imam Mufti
  • Iliyochapishwa mnamo 03 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,962 (wastani wa kila siku: 3)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Belief_in_Divine_Decree_001.jpgKifungu cha sita na cha mwisho cha imani ya Kiisilamu ni kuamini katika uwezo wa Mungu inamaanisha kuwa kila kitu kizuri au kibaya, wakati wote wa furaha au huzuni, raha au maumivu, hutoka kwa Mungu.

Cha kwanza, Maarifa ya Mungu hayakosei. Mungu hajali ulimwengu huu au watu wake. Yeye ni mwenye Hekima na Mpenda, lakini hii isitufanye tuwe watu wenye mawazo mabaya, tukitupa mikono yetu na kusema, ‘nini maana ya kufanya bidii yoyote? maarifa ya Mungu hayaingilii jukumu la mwanadamu. Mungu anatuwajibisha kwa kile tunaweza kufanya, kilicho ndani ya uwezo wetu, lakini hatuwajibishi kwa mambo ambayo hatuna uwezo nayo. Yeye ni Mwadilifu na, ametupatia jukumu mahususi , anatuhukumu ipasavyo. Tunapaswa kufikiria, kupanga na kufanya katika chaguo sahihi, Ila, ikiwa wakati mwingine mambo hayatatokea kama tunavyotaka, hatuhitaji kupoteza tumaini au kuvunjika moyo. Tunapaswa kuomba kwa Mungu na kujaribu tena. Ikiwa mwisho wake bado hatujafikia kile tulichotaka, tunapaswa kujua tumejaribu kadri ya uwezo wetu na hatuwajibiki katika matokeo.

Mungu anajua viumbe vitafanya nini, inajumuisha kila kitu kwa Ujuzi wake. Anajua yote yaliyopo, kwa ukamilifu na kwa jumla, kwa sababu ya ujuaji wake wa milele.

"Hakika Mwenyezi Mungu hakifichiki chochote kwake, duniani wala mbinguni. " (Kurani 3:5)

Yeyote anayelikataa hili anakanusha ukamilifu wa Mungu, kwa sababu kinyume cha maarifa ni ujinga au usahaulifu. Ingemaanisha kuwa Mungu angekuwa amekosea katika maarifa yake ya matukio ya baadaye; Asingekuwa mjuzi tena. Vyote viwili ni mapungufu ambayo Mungu hana.

Cha pili, Mungu ameandika kila kitu kitakachotokea mpaka Siku ya Hukumu katika Ubao Uliohifadhiwa (al-Lauh al-Mahfuz kwa Kiarabu). Muda wa maisha ya wanadamu wote umeandikwa na kiwango cha riziki zao kimegawanywa. Kila kitu ambacho kimeumbwa au kutokea katika ulimwengu ni kulingana na kile kilichoandikwa hapo. Mungu amesema:

"Je! Hujui kwamba Mwenyezi Mungu anayajua yaliomo mbinguni na katika ardhi? Hakika hayo yamo Kitabuni. Hakika hayo kwa Mwenyezi Mungu ni mepesi." (Kurani 22:70)

Cha tatu, Chochote Mungu anachotaka kitendeke, na chochote ambacho Mungu hataki kitendeke hakifanyiki. Hakuna kinachotokea mbinguni au duniani bila mapenzi ya Mungu.

Cha nne, Mungu ndiye muumbaji wa kila kitu.

"…na akaumba kila kitu na akakikadiria kwa kipimo." (Kurani 25:2)

Katika mafundisho ya Uislam kila kitendo cha mwanadamu katika maisha ya kimwili na ya kiroho kimeamriwa, Ila ni vibaya kuamini kuwa hatma ni ya kipofu, ya kiholela, na isiyokoma. Bila kuingiliwa na Mungu katika maswala ya kibinadamu, uhuru wa binadamu unahifadhiwa vizuri. Haipunguzi kanuni ya uhuru wa maadili ya mwanadamu na uwajibikaji. Yote yanajulikana, lakini uhuru pia umepewa.

Mwanadamu sio kiumbe asiye na msaada anayeongozwa na hatma. Badala yake, kila mtu anawajibika kwa matendo yake. Mataifa yenye nguvu na watu wasio na uvumilivu kwa mambo ya kawaida ya maisha wanapaswa kujilaumu, sio Mungu. Mtu analazimika kutii sheria ya maadili; na atapokea adhabu inayostahili au thawabu anapoivunja au kuzingatia sheria hiyo. Ila, ikiwa ni hivyo, mwanadamu lazima awe na uwezo wa kuvunja au kushika sheria ndani ya uwezo wake. Mungu asinge tuwajibisha kwa kitu isipokuwa twenye uwezo nacho:

"Mwenyezi Mungu haikalifishi nafsi yoyote ila kwa kadiri ya iwezavyo." (Kurani 2:286)

Kuamini katika uwezo wa Mungu huimarisha imani ya mtu kwa Mungu. Mtu hutambua kuwa Mungu peke yake ndiye anayedhibiti kila kitu, kwa hivyo anamwamini na kumtegemea. Ingawa mtu anajitahidi kadiri awezavyo, wakati huo huo anamtegemea Mungu kwa matokeo ya mwisho. Bidii yake au akili haimfanyi awe na kiburi, kwani Mungu ndiye chanzo cha kila kinachomjia. Mwisho, mtu hupata utulivu wa akili kwa kugundua kuwa Mungu ndiye Mwenye hikima na matendo yake yanaamriwa na hekima. Mambo hayatokei bila kusudi. Ikiwa kitu kilimfikia, anafahamu kuwa kisingeweza kumuacha. Ikiwa kitu kinamkosa, anajua haikukusudiwa kuwa . Mtu hupata amani ya ndani, anapumzika na utambuzi huu.

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.