Rangi za Umoja wa Uislamu (sehemu ya 3 kati ya 3)
Maelezo: Usawa wa Kiasili ulioungwa mkono na Uislamu na mifano ya kweli ya kihistoria. sehemu ya 3: Hija na Utofauti unaopatikana kati ya Waislamu wa leo.
- Na AbdurRahman Mahdi, www.Quran.nu, (edited by IslamReligion.com)
- Iliyochapishwa mnamo 01 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 5,112 (wastani wa kila siku: 5)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Undugu huu wa kilimwengu unaohubiriwa na uislamu ulitetewa na maswahaba wa mtume baada yake. Pindi Sahaba, Ubada ibn as-Samit, alibeba ujumbe kwenda Muqawqis, askofu mkuu wa Kikristo wa Alexandria, barua ilisema: ‘Mtoe mwanaume huyu mweusi kwangu na mlete mwingine badala yake azungumze na mimi! ... Mnawezaje kukubali mtu mweusi awe bora zaidi yenu? Je, haifai zaidi awe chini yenu?’ ‘Kwa hakika hapana!’, Ndugu wa Ubada wakajibu, ‘Japokuwa yeye ni mweusi kama unavyoona, yeye bado ni wa kwanza kati yetu kwenye uongozi, akili na hekima; kwa weusi haudharauliki kati yetu.’
“Hakika, waumini ni ndugu...” (Kurani 49:10)
Ni Haji, au safari ya Makka, ambayo inabaki kuwa ishara ya msingi ya umoja na undugu kwa mwanadamu. Hapa, tajiri na masikini kutoka nji zote husimama na kuinama kwa umoja mbele ya Mungu katika makutano makubwa ya mwanadamu; kushuhudia maneno ya Mtume aliposema:
“Hakuna mbora kwa Mwarabu juu ya asiyekuwa Mwarabu; au asiyekuwa mwarabu juu ya Mwarabu; au kwa mtu mweupe juu ya mtu mweusi; au mtu mweusi juu ya mtu mweupe; Ila tu kwa njia ya uchamungu.” (Ahmad)
Na hii inasadikisha Kurani, inaposema:
“Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi.…” (Kurani 49:13)
Kuhusu utaifa, na mgawanyiko kwa Waislamu kulingana na mstari wa utaifa na kabila, inachukuliwa na uvumbuzi mbaya.
“Ikiwa baba zenu, na wenenu, na ndugu zenu, na wake zenu, na jamaa zenu, na mali mliyo yachuma, na biashara mnazo ogopa kuharibika, na majumba mnayo yapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Jihadi katika Njia yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake. Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu wapotovu.” (Kurani 9:24)
Mtume anasema:
“... Yeyote mwenye kupigana chini ya bendera ya vipofu, anakuwa na hasira juu ya utaifa, akiuita utaifa, au kusaidia utaifa, na akafa: basi amekufa kifo cha jahiliyya (mf. ujinga kabla ya uislamu na asiyeamini).” (Saheeh Muslim)
Ila, Kurani inasema:
“Pale walio kufuru walipo tia katika nyoyo zao hasira, hasira za kijinga-hasira na hasira za kijinga za jahiliyya, Mwenyezi Mungu aliteremsha utulivu juu ya Mtume wake na juu ya Waumini…” (Kurani 48:26)
Hakika, waislamu ndani yao na wenyewe wanaunda mwili mmoja na taifa kuu,kama ilivyoelezwa na Mtume:
“Mfano wa Walioamini katika upendo wao na huruma ni kama wa mwili ulio hai: kama sehemu moja ikisikia maumivu, mwili wote utateseka kwa kutokulala na homa.” (Saheeh Muslim)
Kurani inathibitisha umoja huu:
“Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani...” (Kurani 2:143)
Labda moja wapo cha kikwazo kikubwa cha kutoukubali Uislamu kwa Wamagharibi wengi ni uzushi kuwa msingi wa dini ni kwaajili ya Wamashariki au watu wenye ngozi nyeusi. Hakuna shaka, ubaguzi wa rangi dhidi ya watu weusi wengi, kuwa watumwa wa Abyssinia Waarabu kabla ya Uislamu, au karne ya 20 Waafrika wa kimarekani, waliwataarifu wengi kuukubali Uislamu. Ila hii ni nje ya mada. Mtume Muhammad alikuwa ni mweupe, alivyoelezewa na maswahaba zake kuwa ‘mweupe na mwekundu’ - wasifu wa mamia na mamilioni ya Waarabu, Berber na Waajemi wnafanana. Hata blondi wenye macho ya bluu sio nadra sana kwa watu wa Wamashariki. Zaidi, Ulaya ina Waislamu wenye asili nyeupe zaidi ya waamiaji weusi’ . Wabosnia, kwa mfano, ambao idadi yao ilipunguzwa katika karne ya 20 ila, kwasababu ya ushujaa wao na uvumilivu, imechangia Balkan kuwa yenye utulivu na amani. Waalbania pia, waliotokana na WaaIllyrian wa ulaya, pia wengi wao ni Waislamu. kwa hakika, Moja ya wasomi wa Kiislamu wa karne ya 20, Imam Muhammad Nasir-ud-Deen al-Albani, alikuwa, kama jina linavyojieleza, Mualbania.
“Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.” (Kurani 95:4)
Watu weupe wamekuwa wakiitwa ‘Wazungu’ tangu wana anthropojia walipotangaza milima ya wazungu, nyumbani mwa vilele vya juu zaidi vya Uropa, kuwa ‘Chimbuko la Asili Nyeupe.’ Leo, wenyeji wa milima hii ni Waislamu. Moja ya makabila ya uchache sana ni wafuasi wa milimani na wasichana wa Kizungu wanaojulikana kwa ujasiri na uzuri na ambao, kama mtawala wa Mamluke wa Syria na Egypt, alisaidia kutetea ulimwengu ulioendelea na kulinda ardhi yake takatifu kutokana na uharibifu wa vikosi vya Wamongoli. Pia kuna Wachenchen walio tendewa ukatili bila shaka ni watu dhaifu kuliko viumbe vyote wa Mungu, ambao kwa ushupavu na upingaji wamesaidia hatma ya Wazungu. Muda huo huo, zaidi ya Wamarekani 1,000,000 na Wazungu weupe wa Ulaya ya Kaskazini - Waanglo-Wasaxon, Franks, Wajerumani, Wascandinavia na Wacelt wakiwemo - sasa wanaukubali Uislamu. Hakika, Uislam umeingia kiamani sehemu ya Ulaya kabla ya Ukristo, tangu: ‘Muda wingi uliopita, tangu Slav wa Kirusi hajaanza kujenga makanisa ya Kikristo Oka au kuchukua maeneo haya kwa jina la Ulaya, Bulgar ilikuwa inasikiliza Kurani kwenye benki za Volga na Kama.’ (Solov’ev, 1965) [mnamo 16 Mei 922, Uislamu ukawa dini rasmi ya taifa la Volga Bulgars, ambapo leo Wabulgaria wanashirikiana kwa asili hii.]
Kila imani ila Uislam inataka ibada ya uumbaji wa aina flani,umbo au taswira. Zaidi, asili na rangi ina jukumu kubwa la kugawanya karibu katika mifumo yote ya imani isiyo ya Kiislamu. Ukristo maana ya Yesu na santi au Buddist katika maana ya Buddha na Dalai Lamas wana watu wa jamii flani na rangi huabudiwa katika kumdharau Mungu. Ndani ya Uyahudi, ukombozi unazuiliwa na mtu asiye Myahudi. Mfumo wa tabaka wa Kihindu vivyo hivyo huangalia matarajio ya kiroho, kijamii na kisiasa na kiuchumi dhana ya 'uchafu’ tabaka la chini. Uislamu, hivyo hivyo, unatafuta kuwaonganisha na kuwafanya kiumbe mmoja wa ulimwengu katika ushirikiano na umoja wa Muumba wao. Hivyo, Uislam pekee ndio unaokomboa watu wote, asili na rangi katika kumuabudu Mwenyezi Mungu Peke yake.
“Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuzi.” (Kurani 30:22)
Ongeza maoni