Idris Tawfiq, Kasisi wa Kikatoliki, Uingereza
Maelezo: Aliyekuwa Kasisi wa Kikatoliki wa Uingereza aukubali Uislamu baada ya kusoma Quran na makutano yake na Waislamu.
- Na Manal Abdulaziz (from The Egyptian Gazette)
- Iliyochapishwa mnamo 17 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 2,656 (wastani wa kila siku: 2)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
“Utawakuta walioshadidi kuliko watu wote katika uadui kwa walioamini ni Mayahudi na washirikina. Na utawakuta waliokaribu mno kwa mapenzi ni wale wanao sema: Sisi ni Manasara. Hayo ni kwa sababu wapo miongoni mwao makasisi na wamonaki, na kwa sababu wao hawafanyi kiburi. Na wanaposikia yaliyo teremshwa kwa Mtume utaona macho yao yanachururika machozi kwa sababu ya Haki waliyo itambua. Wanasema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini. Basi tuandike pamoja na wanao shuhudia.’ (Surat Al-Maida 82-83)”
Hiki ndicho kilichomtokea aliyekuwa kasisi wa Kikatoliki wa Uingereza Idris Tawfiq kwa kuwasomea wanafunzi wake kitabu kitakatifu cha Uislamu, Quran, katika shule moja nchini Uingereza. Na hii ilikuwa ni moja ya hatua muhimu katika safari yake ya kusilimu.
Wakati wa hotuba ya hivi karibuni aliyoitoa katika Baraza la Uingereza huko Cairo, Tawfiq aliweka wazi kuwa hajutii maisha yake ya nyuma na anachoshikilia kuhusiana na kile ambacho Wakristo wanafanya na maisha yake huko Vatican kwa miaka mitano.
“Nilifurahia kuwa kasisi kwa kuwasaidia watu kwa miaka kadhaa. Hata hivyo, ndani kabisa sikuwa na furaha na nilihisi kuwa kulikuwa na jambo ambalo halipo sawa. Kwa bahati nzuri, na ni mapenzi ya Mungu, baadhi ya matukio na sadfa katika maisha yangu viliniongoza kwenye Uislamu,” aliuambia ukumbi uliojaa katika Balaza la Uingereza.
Sadfa ya pili muhimu kwa Tawfiq ilikuwa ni uamuzi wake wa kuacha kazi yake huko Vatikani, hatua iliyofuatiwa na kufunga safari kwenda Misri.
“Nilizoea kufikiria Misri kuwa nchi ya Piramidi, ngamia, mchanga, na mitende. Kwa kweli nilichukua ndege ya kukodi hadi Hurghada.
Nilistushwa kuona kwamba inafanana na fukwe fulani za Ulaya, nilichukua basi la kwanza hadi Cairo ambapo ilikuwa wiki nzuri maishani mwangu.
Huu ulikuwa utangulizi wangu wa kwanza kwa Waislamu na Uislamu. Niliona jinsi gani Wamisri walivyo watu wapole, watamu, lakini pia wenye nguvu sana.
"Kama Waingereza wote, ujuzi wangu kuhusu Waislamu hadi wakati huo haukuzidi yale niliyoyasikia kutoka kwenye TV kama washambuliaji wa kujitoa mhanga na wapiganaji, ambao ilitoa hisia kwamba Uislamu ni dini ya matatizo. Hata hivyo, nilipoingia Cairo niligundua jinsi dini hii ilivyo nzuri. Watu wa kawaida sana wanaouza bidhaa barabarani wakiacha biashara zao na kuelekeza nyuso zao kwa Allah na kuswali mara tu waliposikia mwito wa sala kutoka msikitini. Wana imani thabiti katika uwepo na mapenzi ya Mwenyezi Mungu. Wanaswali, kufunga, kusaidia wahitaji, na huota ndoto ya safari ya kwenda Makka wakiwa na matumaini ya kuishi peponi baada ya dunia kwisha,” alisema.
“Niliporudi, nilianza tena kazi yangu ya zamani ya kufundisha dini. Somo pekee la lazima katika elimu ya Uingereza ni Mafunzo ya Kidini. Nilikuwa nikifundisha kuhusu Ukristo, Uislamu, Dini ya Kiyahudi, Ubudha, na nyinginezo. Kwa hiyo kila siku nililazimika kusoma kuhusu dini hizi ili niweze kufundisha masomo yangu kwa wanafunzi, ambao wengi wao walikuwa wakimbizi wa Kiislamu wa Kiarabu. Kwa maneno mengine, kufundisha kuhusu Uislamu kulinifunza mambo mengi.
“Tofauti na vijana wengi wenye matatizo, wanafunzi hawa wanaonyesha mfano mzuri wa kile ambacho Muislam anaweza kuwa. Walikuwa wenye adabu na wema. Kwa hivyo urafiki ulianza kati yetu na wakauliza ikiwa wanaweza kutumia darasa langu kwa sala wakati wa mfungo wa mwezi wa Ramadhani.
“Kwa bahati nzuri, chumba changu pekee ndicho kilikuwa na zulia. Kwa hiyo nilizoea kuketi nyuma, nikiwatazama wakiomba kwa mwezi mmoja. Nilijaribu kuwatia moyo kwa kufunga wakati wa Ramadhani pamoja nao, ingawa sikuwa Muislamu.
"Wakati mmoja nikisoma tafsiri ya Quran Tukufu darasani nilifikia aya:
“Na wanapo sikiliza ufunuo ulio pokelewa na Mtume, utaona macho yao yanatokwa na machozi, kwa kuwa wao wanaijua haki.
Kwa mshangao nilihisi machozi yakinilenga na nikajaribu sana kuwaficha wanafunzi.”
Tukio la kutikisa dunia
Mabadiliko katika maisha yake, hata hivyo, yalikuja baada ya mashambulizi ya kigaidi nchini Marekani mnamo Septemba 11, 2001.
“Siku iliyofuata, nilikuwa nikijificha na kuona jinsi watu walivyoogopa. Pia niliogopa kurudiwa kwa vitendo hivyo huko Uingereza. Wakati huo, watu wa Magharibi walianza kuogopa dini hii waliyoilaumu kwa ugaidi.
“Hata hivyo, uzoefu wangu wa awali na Waislamu ulinipeleka katika mwelekeo tofauti. Nilianza kujiuliza ‘Kwanini Uislamu? Kwa nini tunaulaumu Uislamu kuwa ni dini kwa kitendo cha magaidi waliotokea kuwa Waislamu, wakati hakuna aliyeutuhumu Ukristo kwa ugaidi wakati baadhi ya Wakristo nao alifanya vitu kama hivyo?
“Siku moja nilielekea kwenye Msikiti mkubwa zaidi wa Uingereza, ili kusikia zaidi kuhusu dini hii. Kuingia katika Msikiti Mkuu wa Uingereza, kulikuwa na Yusuf Islam, mwimbaji wa zamani wa pop, ameketi kwenye duara akizungumza na baadhi ya watu kuhusu Uislamu. Baada ya muda, nilijikuta nikimuuliza” ‘Unafanya nini hasa ili kuwa Muislamu?’”
“Akajibu kwamba Muislamu anapaswa kumwamini Mungu mmoja, kuswali mara tano kwa siku na kufunga Ramadhani. Nilimkatisha nikisema kuwa niliamini haya yote na hata nimefunga Ramadhani. Kwa hiyo akauliza, ‘Unangoja nini? Ni nini kinachokuzuia?’ Nikasema, ‘Hapana, sikusudii kubadili dini.’
“Wakati huo wito wa maombi ulitolewa na kila mmoja akajiandaa kusimama kwenye foleni kuomba.
"Nilikaa nyuma, na nililia na kulia. Kisha nikajiambia, ‘Ni nani ninayejaribu kumpumbaza?’
“Baada ya kumaliza maombi yao, nilielekea kwa Yusufu Islam, nikimuomba anifundishe maneno ambayo natangaza kusilimu kwangu.
"Baada ya kunifafanulia maana yake kwa Kiingereza, nilikariri kwa Kiarabu kuwa hakuna Mola isipokuwa Allah na kwamba Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu," alisimulia Tawfiq, akiyazuia machozi yake.
'Bustani za Uislamu'
Hivyo maisha yake yamechukua mkondo tofauti. Akiwa anaishi Misri, Tawfiq aliandika kitabu kuhusu kanuni za Uislamu.
Akieleza kwa nini aliandika kitabu chake cha "Gardens of Delight": Utangulizi rahisi wa Uislamu, Tawfiq alibainisha kwamba kila mtu anasema kuwa Uislamu si dini ya ugaidi na si dini ya chuki, lakini hakuna anayejaribu kueleza ni nini.
“Kwa hiyo niliamua kuandika kitabu hiki ili kuwapa wasio Waislamu wazo kuhusu kanuni za kimsingi za Uislamu. Nilijaribu kuwaambia watu jinsi Uislamu ulivyo mzuri na kwamba Uislamu una hazina za ajabu zaidi, muhimu zaidi kwa Waislam ni upendo wa wao kwa wao. Mtume anasema ‘Hata tabasamu kwa ndugu yako ni sadaka.
Tawfiq aliliambia Gazeti la Serikali kwamba anakifanyia kazi kitabu kuhusu Mtume Muhammad [rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake] ambacho anadhani kitakuwa tofauti na vitabu vingi vilivyokwisha andikwa juu yake.
Anadhani kwamba “njia bora na ya haraka zaidi” ya kuufahamisha ulimwengu na sura halisi ya Uislamu ni kuwa mfano mzuri katika maisha halisi.
Ongeza maoni