Maelezo Kuhusu Jahanamu (sehemu ya 4 kati ya 5): Mateso ya Jahanamu I

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Sehemu ya kwanza ya taswira ya mateso, hofu, na adhabu ya Jahanamu kama ilivyoelezwa katika vitabu vya kidini vya Kiislamu.

  • Na Imam Mufti
  • Iliyochapishwa mnamo 11 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 6,862 (wastani wa kila siku: 6)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

A_Description_of_Hellfire_(part_4_of_5)_001.jpgMoto wa Jahannamu utakuwa mkali sana hadi watu watakuwa tayari kuacha mali zao na milki walizozipenda, ili wapate kujiokoa:

"Hakika wale walio kufuru, na wakafa hali ni makafiri haitakubaliwa kutoka kwa yeyote wao fidia ya dhahabu ya kujaza dunia nzima lau wangeli itoa. Hao watapata adhabu chungu, wala hawatakuwa na wa kuwanusuru." (kurani 3:91)

Mtume wa Uislamu alisema:

"Siku ya Kiyama atatolewa katika Watu wa Jahannamu, mtu aliyepata anasa zaidi kabisa za dunia, na ataingizwa katika Moto wa Jahannamu. Kisha ataulizwa: Ewe mwana wa Adam! Je! Umewahi kuona kitu kizuri? Je! Umewahi kufurahia anasa zozote?” Atasema: Hapana, naapa kwa Mwenyezi Mungu, Ewe Mola."[1]

Sekunde chache tu motoni na mtu atasahau nyakati zote nzuri alizokuwa nazo. Mtume wa Uislamu anatujulisha:

"Siku ya Kiyama Mwenyezi Mungu atamwuliza yule ambaye adhabu yake katika Moto itakuwa nyepesi zaidi: Iwapo ungemiliki vyovyote unavyovitaka duniani, je, ungevitoa ili upate kujiokoa? Naye atasema: Ndio! Na Mwenyezi Mungu atasema: Nilitaka kidogo mno kuliko hicho ulipo kuwa katika viuno vya Adam, nimekutaka usinishirikishe na chochote katika ibada, lakini ukasisitiza kuwashirikisha wengine na Mimi."[2]

Hofu na ukali wa Moto ni wa kutosha kumfanya mtu kupoteza akili yake. Angekuwa tayari kuacha kila kitu anachopenda ili aokolewe kutoka humo, lakini kamwe hataokoka. Mungu anasema:

"Atatamani mkosefu lau ajikomboe na adhabu ya siku hiyo kwa kuwatoa fidia wanawe, Na mkewe, na nduguye, Na jamaa zake walio kuwa wakimkimu, Na wote waliomo duniani, kisha aokoke yeye. La, hasha! Kwa hakika huo ni Moto mkali kabisa, Unao babua ngozi ya kichwa!" (Kurani 70:11-16)

Adhabu ya Jahannamu pia hutofautiana kwa matabaka. Adhabu ya baadhi ya matabaka ya Jahannamu itakuwa kubwa kuliko mengine. Watu watawekwa katika tabaka lao kulingana na matendo yao. Mtume wa Uislamu alisema:

"Na wapo ambao Moto utawafikia vifundoni mwao, na wengine kwa magoti, na wengine kwenye viuno vyao, na wengine hata shingoni mwao.."[3]

Na akazungumzia mwenye adhabu nyepesi kabisa katika Jahannamu:

"Na atakaye pata adhabu ndogo kabisa miongoni mwa watu wa Jahannamu Siku ya Kiyama atakuwa mtu, ambapo chini ya upinde wa miguu yake patawekwa kaa la moto. Ubongo wake utachemka kutokana nalo."[4]

Mtu huyu atafikiri hakuna mtu mwingine anayeadhibiwa kwa ukali zaidi kuliko yeye mwenyewe, ingawa atakuwa ndiye anayepokea adhabu nyepesi zaidi.[5]

Aya nyingi za Kurani zinazungumzia matabaka mbalimbali ya adhabu wa watu wa Jahannamu:

"Hakika wanaafiki watakuwa katika t'abaka ya chini kabisa Motoni, wala hutompata yeyote wa kuwanusuru." (Kurani 4:145)

"Na itapo fika Saa ya Kiyama patasemwa: Waingizeni watu wa Firauni katika adhabu kali kabisa!" (Kurani 40:46)

Na hakika Moto wa Mwenyezi Mungu utachoma ngozi ya watu wa Jahannamu. Ngozi ni kiungo kikubwa zaidi katika mwili na ndipo maumivu ya kuchomwa husikika. Mungu atabadilisha ngozi iliyoteketezwa na kuibadilisha na ngozi mpya ili ipate kuteketea tena, na hii itaendelea bila kuisha kamwe:

"Hakika wale walio zikataa Ishara zetu tutawaingiza Motoni. Kila zitapo wiva ngozi zao tutawabadilishia ngozi nyengine ili waionje hiyo adhabu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu na Mwenye hikima." (Kurani 4:56)

Adhabu nyingine ya Jahannamu ni kuyeyushwa. Maji yenye joto kali sana yatamwagiwa juu ya vichwa vyao, na yatayeyusha vilivyomo ndani:

"… na yatamiminwa juu ya vichwa vyao maji yanayo chemka. Kwa maji hayo vitayayushwa viliomo matumboni mwao, na ngozi zao pia." (Kurani 22:19-20)

Mtume Muhammad alisema:

"Maji yenye joto kali yatamwagika juu ya vichwa vyao na yatapasua njia yao hadi yakatekate matumbo yao, na kuyatoa; mpaka yatoke kwa miguu yao, na kila kitu kinayeyuka. Kisha watarejeshwa kama walivyo kuwa."[6]

Mojawapo ya njia ya Mwenyezi Mungu ya kuwadhalilisha makafiri katika Jahannamu, ni kuwakusanya Siku ya Kiyama wakikokotwa kwa nyuso zao, wakiwa vipofu, na viziwi, na mabubu.

"Na tutawakusanya Siku ya Kiyama hali wakikokotwa juu ya nyuso zao, nao ni vipofu na mabubu na viziwi. Na makaazi yao ni Jahannamu. Kila moto ukifanya kusinzia tutazidi kuuchochea uwake kwa nguvu." (Kurani 17:97)

"Na watakao kuja na uovu, basi zitasunukishwa nyuso zao Motoni. Je! Kwani mnalipwa isipo kuwa mliyo kuwa mkiyatenda?’" (Kurani 27:90)

"Moto utababua nyuso zao, nao watakuwa na nyuso zilizo kunjana." (Kurani 23:104)

"Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto. Watasema: Laiti tungeli mt'ii Mwenyezi Mungu, na tungeli mt'ii Mtume!.’" (Kurani 33:66)

Adhabu nyingine chungu ya makafiri ni kukokotwa kifudifudi Motoni. Mungu anasema:

"Hakika wakosefu wamo katika upotofu na wazimu. Siku watakapo kokotwa Motoni kifudifudi waambiwe: Onjeni mguso wa Jahannamu!’" (Kurani 54:47-48)

Watakokotwa kifudifudi kwa nyuso zao, huku wakiwa wamefungwa minyororo na pingu:

"Ambao wamekanusha Kitabu na yale tuliyo watuma Mitume wetu. Basi watakuja jua. Zitakapo kuwa pingu shingoni mwao na minyororo, huku wanabururwa Katika maji ya moto, kisha wanaunguzwa Motoni," (Kurani 40:70-72)



Vielezi-chini:

[1] Saheeh Muslim

[2] Saheeh Al-Bukhari

[3] Saheeh Muslim

[4] Saheeh Al-Bukhari

[5] Saheeh Muslim

[6] Tirmidhi

Mbaya Nzuri zaidi

Sehemu za Makala hiki

Tazama sehemu zote pamoja

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.