Msamaha kwa Dhambi Zote Zilizotangulia
Maelezo: Mtu hatakiwi kukata tamaa kutoka kwenye rehema za Mwenyezi Mungu kwa kulinganisha dhambi ambazo mtu alikuwa amezitenda kwenye maisha yake, kwa hakika Mwenyezi Mungu , Mwingi wa Kusamehe na Mwenye Kurehemu, anaweza kusamehe zambi zote.
- Na islam-guide.com
- Iliyochapishwa mnamo 01 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 3,472 (wastani wa kila siku: 3)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Pindi mtu anaposilimu, Mwenyezi Mungu husamehe dhambi zake zote zilizopita na matendo ya kishetani. Mwanaume anaeitwa Amr alikuja kwa Mtume Muhammad, Baraka na rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na akasema, “Nipe mkono wako wa kulia ili nikupe kiapo cha uaminifu.” Mtume akatoa mkono wake wa kulia. Amr akarudisha mkono wake. Mtume akasema: “Kimekupata nini, Wewe Amr?” akajibu, “Ninakusudia kuweka sharti.” Mtume akauliza: “Sharti gani umekusudia kulileta mbele?” Amr akasema, “Kwamba Mungu anisamehe dhambi zangu.” Mtume, baraka na rehema za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akasema,: “Je, haujui kuwa kusilimu kunafuta dhambi zote zilizopita?”[1]
Baada ya kusilimu, mtu atatunzwa kwa matendo yake mazuri na mabaya kulingana na usemi ufuatao wa Mtume Muhammad: “Mola Wako, Mwenye baraka na aliye juu,ni mwingi wa rehema. Kama mtu ameazimia kufanya kitendo kizuri ila hakufanya, kitendo hicho kizuri kitanakiliwa kwake. Na kama akikifanya, (atatunzwa) mara kumi hadi mia saba au mara nyingi zaidi (ya tunzo ya kitendo kizuri), kitanakiliwa kwake. Na kama mtu ataazimia kufanya kitendo kibaya na hakukifanya, kitendo kizuri kitanakiliwa kwake. Na kama akikifanya, kitendo kibaya kitanakiliwa kwake au Mola atakifuta.”[2]
Ongeza maoni