Idhini ya Ibada Inayokubalika katika Uislam

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Jinsi Mungu na Mtume wake walivyofanya njia ya Peponi iwe rahisi.

  • Na Aisha Stacey (© 2019 IslamReligion.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 03 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,088 (wastani wa kila siku: 2)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Concession in Worship.jpgImani ya Uislamu ni zaidi ya dini; ni njia ya maisha. Hakuna sehemu ya mambo ya maisha yetu ya kila siku ambayo Uislamu haijaelezea. Kurani na mila ya Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, zinatufundisha jinsi ya kuishi maisha bora. muhimu zaidi tumefundishwa jinsi ya kumwabudu Mungu, kupitia Nguzo tano za Uislamu na katika matendo yetu yote. Hivyo inaweza kuonekana, kwa wale ambao wamekwangua sura ya juu ya imani ya uislam, kuwa Uislamu ni dini ya kanuni na sheria, fanya hivi, na fanya vile. Hata hivyo, hakuna ukweli wowote juu ya hilo.

Uislamu umetengeezwa kwaajili ya kila mtu, wale ambao uwezo wao wa mwili na akili upo katika hali ya juu, na wale ambao wanapata shida katika maisha. Hivyo, wale ambao hawawezi kukabiliana na msukosuko huu wanaona Uislamu hauna hauna mawazo. Miongozo ya Uislamu, Kurani na mila ya Mtume Muhammad, imeundwa kutoa faraja na kufanya maisha kuwa rahisi. Hii ni kwa sababu sheria za uislam zimeundwa kuwanufaisha wanadamu, na Mtume Muhammad, na yote anayowakilisha na kufundisha, ni rehema kwa wanadamu.

"…Mwenyezi Mungu anakutakieni mepesi wala hakutakieni mazito…" (Kurani 2:185)

Mtume Muhammad aliwashauri wafuasi wake kujihurumia na kwa waumini wapya waliosilimu. Alisema, "Dini ni nyepesi sana na yeyote atakayejishughulisha sana katika dini yake hataweza kuendelea kwa njia hiyo."[1] Na, "Wahurumie watu na uwiswe mgumu juu yao; wape habari njema na usiwajaze chuki’’

Mungu anataka tumuabudu yeye na kufuata miongozo yake, lakini hataki tuelemewe. Anataka njia ya Peponi iwe rahisi, na kufikia mwisho huu kuna kanuni katika Uislamu inayosema ugumu unahimiza urahisi. Hii inamaanisha kuwa ikiwa mtu yuko katika shida sheria za Uislamu zinatoa idhini. Idhini kwa kawaida hutolewa katika hali zinazojumuisha kuumia, ugonjwa, uzee, na safari.

Idhini katika Udhu & Kuswali

Mfano bora wa njia ambayo Mungu hutoa idhini ya kumsaidia muumini inaweza kuonekana katika ibada ya mgonjwa . Ikiwa mtu mgonjwa hawezi kuswali akiwa amesimama, basi anaweza kuswali akiwa ameketi. Ikiwa hawezi kusali akiwa ameketi, basi anaweza kusali akiwa amelala upande wake. Ikiwa hawezi kusali akiwa upande wake, anaweza kulala chali na kutekeleza sala. Idhini hizo zinaonyesha wazi kuwa Mungu hambebeshi mtu yeyote mzigo zaidi ya uwezo wake.

Kila Muislamu lazima atawaze kabla ya sala. Mungu huwapa kibali wale ambao ni wagonjwa au waliojeruhiwa katika hali hii pia. Ikiwa mtu huyo hawezi kutumia maji, au anahofia usalama wake au kutopona ikiwa atatumia, anaruhusiwa kutumia ardhi safi kufanya udhu mkavu kwa kuipiga ardhi kwa mikono miwili na kisha kuifuta usoni na mikono.

Ugumu unaosababishwa na ugonjwa au jeraha ni mojawapo ya visingizio halali ambavyo hufanya kutoruhusiwa sala za pamoja. Ikiwa mtu ni mgonjwa au ameumia inaruhusiwa kwake kutojiunga na sala za pamoja za mchana na alasiri, na sala za jioni na wakati wa usiku wakati wa sala ya mapema au ya baadaye, kulingana na urahisi wake. Inapaswa kueleweka hata hivyo kuwa sala zinapaswa kuswaliwa kwa ukamili kwa sababu mwenye idhini ya kufupisha sala amepewa msafiri

Sheikh al-Islam Ibn Taymiyah alisema, "Sababu ya kufupisha sala ni (kwa) kusafiri tu, na hairuhusiwi wakati mtu hayuko safarini. kwa sala za pamoja wakati mtu ana udhuru au hitaji (ugonjwa au jeraha), ikiwa anahitaji, anaweza kuziunganisha wakati wa kusafiri umbali mfupi au mrefu, na anaweza kuziunganisha wakati wa kunanyesha kwa mvua na kadhalika, au wakati anaumwa na kadhalika, au kwa sababu zingine. Lengo la hii ni kuepusha taifa la Waislamu (waumini) kutokana na shida.’[2]

Anas ibn Malik alisema, "Tulitoka na Mtume kutoka Madinah kwenda Makka, na alisali sala zake kwa rakaa mbili kila wakati hadi tuliporudi Madinah"[3]

Idhini wakati wa Kufunga

Waislamu wanawajibika kufunga wakati wa mwezi wa Ramadhani. Ni moja ya nguzo tano za Uislamu, lakini, ikiwa mtu huyo atakuwa mzee au mgonjwa, au kuna sababu nyingine ya kweli, kama ugonjwa sugu, Mwuislam utapata udhuru ya kufunga. Sio lazima walipe siku walizozikosa ila wanahitajika kulisha mtu masikini kwa kila siku ya Ramadhani. Kwa mtu ambaye ni mgonjwa katika kipindi cha kufunga lakini anatarajia kupona anaruhusiwa ama asifunge au afungulie; wanahitajika kulipia kufinga siku yoyote ya kufunga waliyoikosa.

"…Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hisabu katika siku nyengine. Na wale wasio weza, watoe fidiya kwa kumlisha masikini.…" (Kurani 2:184)

Msafiri pia anaruhusiwa kuacha kufunga au kuvunja saumu yao ikiwa wanasafiri umbali unaohitajika katika kufupisha sala. Ila, lazima wafidie siku walizozikosa. Wanawake wajawazito na wanaonyonyesha wanaruhusiwa kupumzika ikiwa wana wasiwasi na afya zao, watoto wao, au watoto wao ambao hawajazaliwa. Wanawake wajawazito na wanaonyonyesha lazima walifidie siku ambazo wamezikosa wakati hali zao au hali yao ikibadilika.

Idhini katika Hajj (Hija Kuu)

Hajj ni jukumu la kila Mwislamu mtu mzima, mwenye akili timamu, na mwenye uwezo wa kifedha. Ni wale tu ambao wana vifungu muhimu na njia wanalazimika kuifanya. Kwa hivyo, maskini sana na wahitaji wametolewa. Kwa kuongezea haya, kuna idhini zingine za kuhakikisha nguzo za Uislamu haziwi ngumu, na shida zote zimetolewa.

"Na kwa ajili ya Mwenyezi Mungu imewajibikia watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. " (Kurani 3:97)

Ikiwa msafiri ni mzee, mlemavu, au hawezi kutembea lakini ana afya njema, anaweza kutumia njia ya usafiri kama vile kiti cha magurudumu. Wakati wa Mtume Muhammad, haikuwa kawaida kuona watu wakizunguka Kabah nyuma ya punda.

Moja ya mila ya Hajj ni kubaki Muzdalifah usiku mmoja na kuendelea hadi Mina kutupa kokoto baada tu ya jua kuchomoza. Ila, Mungu huwapa idhini wazee, dhaifu, na wanawake na watoto, akiwaruhusu kutupa kokoto wakati wa usiku.

Hii sio orodha kamili ya idhini ambazo Mungu anaruhusu ili kupunguza shida kwa waumini. Mifano hii imetolewa ili kudhihirisha kuwa hata katika Nguzo za lazima za Uislamu Mungu anataka waumini wajisikie faraja na urahisi.



Rejeleo la maelezo:

[1] Saheeh Al-Bukhari.

[2] Majmoo’ al-Fataawa (22/293).

[3] Saheeh Al-Bukhari, Saheeh Muslim.

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.