Je, Mungu anahitaji ibada yetu? Kwa nini alituumba ili tumwabudu?

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Mungu ndiye Kiumbe pekee anayestahili ibada yetu yote, na tuliumbwa tumwabudu. Makala hii inazungumzia maswali mawili yafuatayo yanayoulizwa mara kwa mara: Je, anahitaji ibada yetu na kwa nini alituumba ili tumwabudu?

  • Na Hamza Andreas Tzortzis (http://www.hamzatzortzis.com)
  • Iliyochapishwa mnamo 07 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 2,266 (wastani wa kila siku: 2)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Njia bora ya kujibu maswali haya ni kuelewa kwanza Mungu ni nani katika muktadha wa ibada. Mungu kwa ufafanuzi Ndiye Anayestahiki ibada yetu; ni ukweli wa lazima wa uwepo Wake. Quran inasisitiza mara kwa mara ukweli huu kuhusu Mungu,

"Hakika Mimi ndiye Mwenyezi Mungu. Hapana mungu ila Mimi tu. Basi niabudu Mimi, na ushike Swala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi." (Quran 20:14)

Does-God-need-our-worship.jpgKwa vile Mungu, kwa ufafanuzi, ndiye Kiumbe pekee ambaye haki Yake ni ibada yetu, basi matendo yetu yote ya ibada yanapaswa kuelekezwa Kwake pekee.

Katika mapokeo ya Kiislamu, Mungu anachukuliwa kuwa Mtu mkamilifu kabisa. Ana majina na sifa zote kamili kwa kiwango cha juu kabisa. Kwa mfano, katika theolojia ya Kiislamu Mungu anaelezewa kuwa Mwenye Upendo, na hii ina maana kwamba upendo Wake ni upendo mkamilifu zaidi na upendo Wake ni upendo mkuu zaidi. Ni kwa sababu ya majina na sifa hizi kwamba Mungu lazima aabudiwe. Daima uwa tunawasifu watu kwa wema, maarifa na hekima zao. Hata hivyo, fadhili, ujuzi na hekima ya Mungu ni ya kiwango cha juu kabisa bila upungufu au dosari. Kwa hiyo, Yeye anastahili aina pana zaidi ya sifa na kumsifu Mungu ni aina ya ibada. Pia Mungu pekee ndiye anayestahiki dua na maombi yetu. Anajua zaidi yaliyo mema kwetu, na pia anataka yaliyo mema kwetu. Kiumbe kama hiki chenye sifa hizi lazima kiombewe, na kuombwa msaada. Mungu anastahili ibada yetu kwa sababu kuna kitu kuhusu Mungu kinachomfanya awe hivyo. Yeye ndiye Mwenye majina na sifa kamilifu kabisa.

Jambo muhimu kuhusu kumwabudu Mungu ni kwamba ni haki yake hata kama hatupokei aina yoyote ya faraja. Ikiwa tungeishi maisha yaliyojaa mateso, bado Mungu anapaswa kuabudiwa. Kumwabudu Mungu hakutegemei aina fulani ya uhusiano wa kubadilishana; Yeye hutupatia uzima, nasi tuna muabudu. Usielewe vibaya ninachosema hapa, Mungu anatunyeshea baraka nyingi; hata hivyo, Anaabudiwa kwa sababu ya Yeye Alivyo na si lazima jinsi anavyoamua—kupitia hekima Yake isiyo na kikomo—kusambaza fadhila Zake. Kuna sababu nyingine nyingi kwa nini Mungu anastahili ibada yetu (ambazo zina husisha upendo, kushukuru kwa baraka zetu, nk.), hata hivyo mada hii maalum itaelezewa katika makala nyingine.

Je, Mungu anahitaji ibada yetu?

Swali hili la kawaida linazuka kutokana na kutomwelewa Mungu katika mapokeo ya Kiislamu. Quran na Hadithi za Mtume zina eleza kwa uwazi kwamba Mwenyezi Mungu ni Mkubwa na hana haja yoyote; kwa maneno mengine, Yeye ni huru kabisa:

"Hakika Mwenyezi Mungu si mhitaji wa walimwengu." (Quran 29:6)

Kwa hiyo, Mungu hahitaji sisi kumwabudu hata kidogo. Hafaidiki chochote kutokana na ibada yetu, na kukosa kwetu kumwabudu hakuondoi chochote kwa Mungu. Tunamwabudu Mungu kwa sababu—kupitia hekima na rehema ya Mungu—Alituumba hivyo. Mungu aliifanya ibada kuwa nzuri na yenye manufaa kwetu, kwa mtazamo wa kidunia na kiroho.

Kwa nini alituumba ili tumwabudu?

Kinachofuata kutoka kwa jibu hili kwa kawaida ni swali: Kwa nini Mungu alituumba ili tumwabudu? Mungu ni Kiumbe kizuri zaidi, na kwa hivyo matendo Yake si mazuri tu, ni maonyesho ya asili Yake. Isitoshe, Mungu anapenda mema. Kwa kua Mungu ameumba viumbe wenye akili timamu ambao wangechagua kwa hiari kumwabudu Yeye na kufanya mema, wengine hadi kufikia hatua ya kuinuliwa katika wema kama manabii, na kisha kupewa uzima wa milele mbele ya Mungu, kupita upendo na urafiki wa karibu sana wa milele, ni hadithi kuu kuwahi kusimuliwa. Kwa kuwa Mungu anapenda mema yote, ni wazi kwa nini Angefanya hadithi hii kuwa ya kweli. Kwa mukhtasari, Mungu alituumba ili tumwabudu kwa sababu anatutakia mema; kwa maneno mengine anataka tuende peponi. Amebainisha kuwa wale wanaoifikia Pepo wameumbwa kwa ajili ya kupata rehema yake.[1]

"Na Mola wako Mlezi angeli penda ange wafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana—Isipo kuwa wale ambao Mola wako Mlezi amewarehemu; na kwa hiyo ndio Mwenyezi Mungu amewaumba." (Quran 11:118-119)

Mungu kutuumba sisi ili kumwabudu yeye ilikuwa ni suala la lazima. Majina na sifa zake kamilifu zingejidhihirisha zenyewe. Msanii hutengeneza kazi ya sanaa bila shaka kwa sababu ana sifa ya kuwa kisanii. Kwa sababu kubwa zaidi, bila shaka Mungu angetuumba tumwabudu kwa sababu Yeye ndiye anayestahili kuabudiwa. Kutoepukika huku hakutegemei hitaji bali udhihirisho wa lazima wa majina na sifa za Mungu.

Njia nyingine ya kujibu swali hili ni kuelewa kwamba ujuzi wetu ni wa vipande vipande na una kikomo, kwa hiyo hatutaweza kamwe kufahamu jumla ya hekima ya Mungu. Kama ilivyotajwa hapo awali, ikiwa tungeelewa hekima yote ya Mungu, ingemaanisha tungekuwa Miungu au kwamba Mungu angekuwa kama sisi. Yote mawili ni mambo yasiyowezekana. Kwa hivyo, ukweli wenyewe kwamba kunaweza kuwa hakuna jibu kwa swali hili unaonyesha kupita maarifa ya Mungu. Kwa mukhtasari, alituumba ili tumwabudu kwa sababu ya hekima yake ya milele, hatuwezi kuelewa ni kwa nini.

Njia ya vitendo ya kuangalia swali hili imefafanuliwa katika kielelezo kifuatacho. Fikiria ulikuwa ukingoni mwa mwamba na mtu akakusukuma ndani ya bahari chini. Maji yana samaki papa. Hata hivyo, aliyekusukuma alikupa ramani ya kuzuia maji na tanki la oksijeni ili uweze kusafiri kupitia maeneo salama ili kufikia kisiwa kizuri cha tropiki ambapo utakaa milele katika furaha. Ikiwa ungekuwa na akili, ungetumia ramani na kufika salama katika kisiwa hicho. Hata hivyo, nikiwa nimekwama kwenye swali Kwa nini umenitupa humu? pengine itamaanisha umeliwa na papa. Kwa Muislamu, Quran na Hadith za Kinabii ndizo ramani na tanki la oksijeni. Wanatuambia jinsi ya kuzunguka njia ya uzima kwa usalama. Tunapaswa kumjua, kumpenda na kumtii Mungu, na kuweka matendo yote ya ibada kwake Yeye pekee. Kimsingi tuna chaguo la kudhuru nafsi zetu wenyewe kwa kupuuza ujumbe huu, au kushika upendo na huruma ya Mungu kwa kuukubali.

Ilisasishwa mara ya mwisho 30 Januari 2017. Imechukuliwa na kurekebishwa kutoka kwa kitabu cha "The Divine Reality: God, Islam & The Mirage of Atheism". Unaweza kununua kitabu hapa.



Rejeleo la maelezo:

[1] Mahali, J. na As-Suyuti J. (2001) Tafsir al-Jalalayn. Toleo la 3. Cairo: Dar al-Hadith, p. 302. Unaweza kupata nakala mtandaoni kwenye: https://ia800205.us.archive.org/1/items/FP158160/158160.pdf [Ilifikiwa tarehe 1 Oktoba 2016].

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi
(Soma zaidi...)

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.