Wengi wanaamini kimakosa kwamba Uislamu hauvumilii kuwepo kwa dini nyingine zilizopo duniani. Makala hii inazungumzia baadhi ya misingi ambayo Mtume Muhammad mwenyewe aliiweka katika kushughulika na watu wa imani nyingine, kwa mifano ya kivitendo toka enzi za uhai wake. Sehemu ya 1: Mifano ya uvumilivu wa kidini kwa watu wa imani nyingine inayopatikana katika katiba ambayo Mtume aliiweka Madina.