Akifah Baxter, Mkristo wa zamani, Marekani

Ukadiriaji:
Ukubwa wa herufi:
A- A A+

Maelezo: Akitembea katika duka la vitabu kutafuta mwongozo, Akifah anapata kitabu kuhusu Uislamu.

  • Na Akifah Baxter
  • Iliyochapishwa mnamo 17 Dec 2021
  • Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
  • Ilichapishwa: 0
  • Imetazamwa: 1,564 (wastani wa kila siku: 2)
  • Ukadiriaji: bado hakuna
  • Imekadiriwa na: 0
  • Imetumwa kwa barua pepe: 0
  • Ilitoa maoni kuhusu: 0
Mbaya Nzuri zaidi

Daima nimekuwa na ufahamu wa kuwepo kwa Mungu. Daima nilihisi kwamba yupo. Wakati mwingine hisia hiyo ilikuwa ya mbali, na mara nyingi niliipuuza. Lakini sikuweza kamwe kukataa utambuzi huo. Kwa sababu hiyo, katika maisha yangu yote, nimekuwa nikitafuta ukweli wa Mpango Wa Mungu.

Nimehudhuria makanisa mengi. Nilisikiliza, niliomba, nilizungumza na watu kutoka kwa imani zote tofauti. Lakini ilionekana kwamba daima kulikuwa na kitu ambacho hakikuonekana sawa; nilihisi kuna utata, kama vile kulikuwa na kitu kilikuwa hakiko. Nimesikia watu wengi zamani wakiniambia, “Ninamwamini Mungu, lakini mimi si wa dini yoyote. Zote hazionekani kuwa sahihi kwangu.” Hii ilikuwa hisia yangu hasa, hata hivyo, sikutaka kuiacha hivyo tu basi na kuikubali hivyo tu. Nilijua kwamba kama Mungu yupo basi hangetuacha tu bila mwelekeo, au hata kutuacha na ukweli usioeleweka. Lazima kuwe na mpango, “dini ya kweli.” Kazi yangu ilikuwa ni kuipata tu.

Makanisa mbalimbali ya Kikristo ndipo nilipoelekeza utafiti wangu, kwa sababu hiyo ndiyo niliyolelewa nayo, na yalikuwa na ukweli fulani katika baadhi ya mafundisho yao. Hata hivyo, kulikuwa na maoni mengi tofauti, mafundisho mengi yanayopingana juu ya mambo ya kimsingi kama vile jinsi ya kuomba, ni nani wa kuombwa, ni nani atakuwa wa “kuokolewa”, na ni nani hataokolewa, na mtu alipaswa kufanya nini ili “aokoke.” Ilionekana kuwa na utata mwingi. Nilihisi nilikuwa karibu kukata tamaa. Nilikuwa nimetoka kanisa lingine ambalo maoni yake kuhusu Mungu na kusudi la kuwepo kwetu, yaliniacha nikiwa nimechanganyikiwa kabisa kwa sababu nilijua kile walichokuwa wakifundisha hakikuwa kweli.

Siku moja, nilikuwa katika duka la vitabu nilikwenda kwenye sehemu ya dini. Nilipokuwa nimesimama pale nikitazama vitabu vingi vya Kikristo, nilipata fikra ya kuangalia kama walikuwa na chochote kuhusu Uislamu. Sikujua chochote kuhusu Uislamu, na nilipochukua kitabu cha kwanza, ilikuwa ni kutokana na kutaka kudadisi tu. Lakini nilifurahia na kile nilichokisoma. Mojawapo ya mambo yaliyonishangaza sana ni kauli ya 'Hakuna mungu isipokuwa Mwenyezi Mungu.' Hana washirika, na Maombi yote na ibada zinamwendea Yeye peke yake. Hii ilionekana kuwa rahisi, yenye nguvu, ya moja kwa moja, na kwangu ilipatana na akili vizuri. Hivyo kutoka hapo nilianza kusoma kila kitu nilichoweza kupata kuhusu Uislamu.

Kila kitu nilichokisoma kilikuwa na maana kimantiki kwangu. Ilikuwa ni kama ghafla vipande vyote vya fumbo hili vilikuwa vinaingiliana kikamilifu, na taswira wazi ilikuwa inajitokeza. Nilifurahi sana hadi moyo wangu ungeenda mbio wakati wowote niliposoma chochote kuhusu Uislamu. Kisha, nilipoisoma Qurani, nilihisi nimebarikiwa sana kwa kuweza kukisoma kitabu hiki. Nilijua kwamba hii imetoka kwa Mwenyezi Mungu kwa njia ya Mtume Wake [Rehma na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake.] Hii ndio nilikuwa nikitafuta, ukweli halisi. Nilihisi kwamba wakati wote huu nilikuwa Muislamu lakini sikujua hadi sasa. Sasa ninapoanza maisha yangu kama Muislamu, nina hisia ya amani na usalama nikijua kwamba kile ninachojifunza ni ukweli safi na kitanipeleka karibu na Mungu. Naomba Mungu aendelee kuniongoza. Amiina.

Mbaya Nzuri zaidi

Ongeza maoni

  • (Haitaonyeshwa kwa umma)

  • Maoni yako yatakaguliwa na yanapaswa kuchapishwa ndani ya saa 24.

    Sehemu zilizo na alama ya nyota (*) zinahitajika.

Makala Nyingine katika Aina moja

Iliyotazamwa Zaidi

Kila siku
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
jumla
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Chaguo la Mhariri

(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Orodha Yaliyomo

Tangu ulivyo tembelea mara ya mwisho
Orodha hii ipo tupu kwa sasa.
Zote kwa tarehe
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)

Maarufu sana

Iliyokadiriwa juu zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotumwa  kwa barua pepe zaidi
Iliyochapishwa zaidi
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
(Soma zaidi...)
Iliyotolewa maoni zaidi

Unazozipenda

Orodha ya unazozipenda ipo tupu. Unaweza kuongeza makala kwenye orodha hii kwa kutumia zana za makala.

Historia yako

Orodha yako ya historia ipo tupu.