Maelezo ya Moto wa Jahanamu (sehemu ya 2 kati ya 5): Muonekano wake
Maelezo: Maeneo, ukubwa, viwango, milango na kuni za Jahannamu, pamoja na mavazi ya wenyeji.
- Na Imam Mufti
- Iliyochapishwa mnamo 13 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 7,118 (wastani wa kila siku: 7)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Maeneo Yake
Hakujatajwa kabisa kwa Qur'ani wala hadithi ya Mtume Muhammad jambo linaloonyesha Jahannamu iko wapi. Hakuna ajuaye iko wapi isipokuwa Mwenyezi Mungu. Kutokana na baadhi ya ushahidi wa kilugha na mukhtadha wa baadhi ya hadithi za mtume, baadhi ya wasomi wamesema kuwa Jahannamu iko mbinguni, na wengine wanasema kuwa iko katika ardhi ya chini.
Ukubwa Wake
Jahannamu ni kubwa sana na kina chake ni kirefu mno. Tunajua hili kupitia njia kadhaa.
Kwanza, watu wasiohesabika wataingia Jahannamu, kila mmoja, kama ilivyoelezwa katika hadithi, akiwa na meno ya mwisho yenye ukubwa wa mlima Uhud (mlima kwenye mji wa Madina) [1] Umbali kati ya mabega ya wenyeji wake pia umeelezwa kuwa sawa na matembezi za siku tatu.[2] Jahannamu itakuwa makao ya makafiri wote na wenye dhambi tangu mwanzo wa wakati na bado kutakuwa na nafasi ya wengine wengi. Mungu anasema:
"Siku tutapo iambia Jahannamu: Je! Umejaa? Nayo itasema: Je! Kuna ziada?’" (Kurani 50:30)
Moto wa Jahannamu unafananishwa na kinu kinachosaga maelfu na maelfu ya tani za nafaka na kisha kinasubiri zaidi.
Pili, jiwe linalotupwa kutoka juu ya Jahannamu litachukua muda mrefu sana kufikia chini. Mmoja wa maswahaba wa Nabii, rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, anaeleza jinsi walivyokuwa wamekaa pamoja na Nabii, na wakasikia sauti ya kitu kinachoanguka. Nabii akauliza kama wanajua ni nini? Waliposhindwa kujua, alisema:
"Hili lilikuwa jiwe lililotupwa Jahannamu miaka sabini iliyopita, likawa bado katika njia ya Jahannamu mpaka sasa."[3]
Ripoti nyingine inasema:
"Na lau kuwa likitupwa jiwe kubwa kama ngamia saba wajawazito kutoka juu ya Jahannamu, lingelivuka humo kwa muda wa miaka sabini, na lisingelifika chini."[4]
Tatu, Malaika wengi wataleta Jahannamu Siku ya Kiyama. Mungu anazungumzia hilo:
"Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo..." (Kurani 89:23)
Mtume alisema:
"Siku hiyo italetwa Jahannamu kwa kamba sabini elfu, ambazo kila moja zitashikiliwa na Malaika sabini elfu."[5]
Nne, ripoti nyingine inayoonyesha ukubwa wa Jahannamu ni kwamba jua na mwezi vitakunjwa ndani Jahannamu Siku ya Kiyama.[6]
Viwango Vyake
Jahannamu ina viwango tofauti vya joto na adhabu, na kila moja huhifadhiwa kulingana na kiwango cha ukafiri na dhambi za wale wanaoadhibiwa. Mungu anasema:
"Hakika wanaafiki watakuwa katika t'abaka ya chini kabisa Motoni." (Kurani 4:145)
Kiwango cha chini cha Jahannamu, ndicho chenye joto zaidi. Na lau kuwa wanafiki watapata adhabu mbaya kabisa, basi hao watakuwa katika sehemu ya chini kabisa ya Jahannamu.
Mungu anaelezea ngazi za Jahannamu katika Qur'ani:
"Na wote wana daraja mbali mbali kutokana na yale waliyo yatenda." (Kurani 6:132)
"Je! Aliye yafuata ya kumridhisha Mwenyezi Mungi ni kama yule aliye stahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na makaazi yake yakawa Jahannamu? Napo ni mahala pabaya pa kurejea. Hao wana vyeo mbali mbali kwa Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuyaona yote wayatendayo." (Kurani 3:162-163)
Milango ya Jahannamu
Mungu anaongelelea kuhusu milango saba ya Jahannamu katika Kurani:
"Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipo ahidiwa wote. Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio tengewa." (Kurani 15:43-44)
Kila mlango una sehemu iliyopangwa ya aliyehukumiwa atakayeingia kupitia mlango huo. Na kila mmoja ataingia kulingana na vitendo vyake, na atawekewa kiwango cha Jahannamu ipasavyo. Na watakapo letwa makafiri Jahannamu milango yake itafunguliwa, wataingia humo, na watadumu humo milele:
"Na walio kufuru wataongozwa kuendea Jahannamu kwa makundi. Mpaka watakapo ifikia itafunguliwa milango yake, na walinzi wake watawaambia: Kwani hawakukujilieni Mitume miongoni mwenu wakikusomeeni Aya za Mola wenu Mlezi na kukuonyeni mkutano wa siku yenu hii? Watasema: Kwani! Lakini limekwisha thibiti neno la adhabu juu ya makafiri.’" (Kurani 39:71)
Wataambiwa baada ya kuingia:
"Ingieni milango ya Jahannamu mdumu humo. Na makaazi ya wanao takabari ni maovu mno." (Kurani 39:72)
Malango yatafungwa na hakutakuwa na tumaini la kutoroka kama Mungu asemavyo:
"Hakika walio zikataa Ishara zetu, hao ndio watu wa shari wa kushotoni. Juu yao utakuwa Moto ulio fungiwa kila upande.[7]" (Kurani 90:19-20)
Zaidi ya hayo, Mungu anasema katika Qur'ani:
"Ole wake kila safihi, msengenyaji! Aliye kusanya mali na kuyahisabu. Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele. Hasha! Atavurumishwa katika Hutama (motoni). Na nani atakujuvya ni nini H'ut'ama? huo ni Moto wa Mwenyezi Mungu ulio washwa. Ambao unapanda nyoyoni. Hakika huo utafungiwa nao Kwenye nguzo zilio nyooshwa." (Kurani 104:1-9)
Na milango ya Jahannamu pia hufungwa kabla ya Siku ya Kiyama. Nabii wa Uislamu alizungumza juu ya kufunga kwayo katika mwezi wa Ramadhani.[8]
Kuni Zake
Mawe na makafiri wajeuri ndio kuni za Jahannamu kama asemavyo Mwenyezi Mungu:
"Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe..." (Kurani 66:6)
"…Basi uogopeni Moto ambao kuni zake ni watu na mawe, walio andaliwa kwa ajili ya makafiri." (Kurani 2:24)
Na chanzo kingine cha kuni za Jahannamu ni miungu iliyo abudiwa badala ya Mwenyezi Mungu:
"Hakika nyinyi na hao mnao waabudu badala ya Mwenyezi Mungu ni kuni za Jahannamu; huko mtaingia tu. Lau kuwa hawa ni miungu, wasingeli ingia. Na wote watadumu humo." (Kurani 21:98-99)
Mavazi ya Wakazi Wake
Na Mwenyezi Mungu anatuambia kwamba mavazi ya watu wa Motoni yatakuwa nguo za Motowalizoundiwa:
"…Basi walio kufuru watakatiwa nguo za moto, na yatamiminwa juu ya vichwa vyao maji yanayo chemka." (Kurani 22:19)
"Na utawaona wakosefu siku hiyo wamefungwa pingu, na nguo zao za lami, na nyuso zao zimefunikwa na Moto." (Kurani 14:49-50)
Ongeza maoni