Mambo tunayojifunza kutoka kwa Hadithi ya Mama wa Musa
Maelezo: Hadithi za Qurani zipo pale ili tuweze kupata masomo kutoka kwazo. Katika makala hii, tutajifunza masomo kadhaa kutoka kwa mama wa mmoja wa mitume wakuu wa Mungu, hasa kuhusu kumtegemea Mungu na matokeo ya kufanya hivyo.
- Na Raiiq Ridwan (understandquran.com) [edited by IslamReligion.com]
- Iliyochapishwa mnamo 10 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 2,139 (wastani wa kila siku: 2)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Makala hii itazungumzia hadithi ya mamake Musa, amani iwe juu yake, na alivyojitahidi kumuokoa mtoto wake kutoka kwa kifo cha karibu, na kutoa masomo kutoka kwa hayo. Tutazingatia tu aya za Surah Al-Qasas (Sura ya 28) katika Qur'ani, ingawa hadithi hii imetajwa pia katika sehemu zingine kwenye Qurani.
"Tulimfunulia mama yake Musa kwa kumwambia: Mnyonyeshe. Na utakapo mkhofia basi mtie mtoni, na usikhofu wala usihuzunike. Hakika Sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa Mitume. Basi wakamwokota watu wa Firauni, aje kuwa adui kwao na huzuni. Hakika Firauni na Hamana na majeshi yao walikuwa wenye makosa. Na mkewe Firauni alisema: Atakuwa kiburudisho cha macho kwangu na kwako. Msimuuwe! Huenda akatufaa, au tumpange kuwa mwenetu. Wala wao hawakutambua. Na moyo wa mama yake Musa ukawa mtupu. Alikuwa karibu kumdhihirisha, ingeli kuwa hatukumtia nguvu moyo wake ili awe miongoni mwa Waumini. Naye akamwambia dada yake Musa: Mfuatie. Basi naye akawa anamuangalia kwa mbali bila ya wao kujua. Na tukamjaalia awakatae wanyonyeshaji wote tangu mwanzo, mpaka dada yake akasema: Je! Nikuonyesheni watu wa nyumba watakao mlea kwa ajili yenu, nao pia watakuwa wema kwake? Basi tukamrudisha kwa mama yake ili macho yake yaburudike, wala asihuzunike. Na ajue ya kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya kweli, lakini wengi wao hawajui." (Quran 28:7-13)
Firauni aliona ndoto ambapo aliona ya kuwa mtoto kutoka kundi la watumwa—Wana wa Israili—angeinuka na kumpindua. Baada ya hapo akaanza kumwua kila mtoto wa kiume aliyezaliwa na Wana wa Israeli. Ilikuwa ni wakati kama huo ndipo Musa alizaliwa. Na katikati ya hayo yote, Mungu alimchagua kijana huyu juu ya wengine wote aokolewe kimiujiza. Hivyo, Mungu alituma maagizo yake kwa mama yake Musa.
Somo la Kwanza: Mtii Mwenyezi Mungu, toa wasiwasi kutoka kwa moyo wako, na kuwa na matumaini kwa ahadi Yake
Mwenyezi Mungu anatoa amri mbili— mnyonyeshe na umweke katika kikapu na kisha umtupe mtoni, na vipande viwili vya ushauri kwa moyo—usiogope wala usihuzunike, na ahadi mbili—ya kwamba atarudishwa na atakuwa Mtume. Mungu alitoa amri mbili, moja ambayo ilikuwa rahisi kueleweka (kunyonyesha), na moja ambayo inaonekanahaikuwa na maana (kumtupa mtoto ndani ya mto!!?). Mamake Musa hakuchagua wala kubagua. Alimtii Mola wake Mlezi bila kujali, huku akiwa na wasiwasi, ambalo ni jambo la kawaida, na hivyo Mungu akampa vipande viwili vya ushauri, na ahadi mbili. Somo tunalojifunza hapa ni kwamba licha ya kile kinachoweza kuonekana, katika nyakati ngumu sana, kumtii Mungu hata kama amri yake inaonekana kuwa “ajabu” ndiyo njia sahihi. Chukua uamuzi sahihi kulingana na yale anayosema Mungu, na ujue kwamba ukimtii Mungu hakuna kitu cha kuogopwa na hakuna chochote cha kusikitisha, na kwamba ahadi ya Mungu ni ya kweli, hata kama huioni wakati huo. Je, mamake Musa alikuwa na wazo lolote kwamba mwanawe angeweza kuishi? Tupilia mbali hata kuwa mtume na kurejeshwa kwake?
Somo la Pili: Mungu anaweza kuleta nuru kutoka kwa giza totoro
Maelfu ya akina mama wangelia kwa sababu ya matendo ya Firauni. Lazima walifanya dua (ombi) ili Mwenyezi Mungu amwangamize huyu jeuri (walikuwa ni Waumini wa wakati huo). Hata hivyo, Mungu akamweka yule kijana ambaye angemwangamiza yule jeuri ndani ya nyumba ya jeuri mwenyewe. Kutoka kwenye mashimo ya giza kabisa ya kufr (ukafiri), jumba la Firauni, Mwenyezi Mungu alitoa nuru—Musa. Mtu aliyewaua maelfu ya watoto, hakuweza kumwua mtoto mmoja ambaye alitakiwa kumwangamiza yeye. Mungu anapomlinda mtu, hakuna anayeweza kumdhuru, hata kama ulimwengu mzima utajaribu. Kwa hakika, Mungu alifanya hivyo kwa namna ambapo mke wa Firauni, Asiyah ndiye aliyempenda mtoto huyo na kumchukua kama mwanawe. Mungu akajibu maombi ya maelfu ya akina mama, ya mamilioni ya Waisraeli waliotiwa katika utumwa kwa njia hii. Mipango yake ni ya kipekee, mipango yake ni mikubwa kuliko ufahamu wetu, lakini Yeye ndiye bora wa wapangaji. Utakapokuwa katika giza totoro, kumbuka kuwa Mwenyezi Mungu ndiye anayeweza kutoa nuru kutoka humo, na kwamba Yeye ndiye ana mpango.
Somo la Tatu: Shaka inapoingia, kuwa na mpango wa pili lakini bado kuwa na tumaini kwa Mungu
Moyo wa mama yake Musa ulikuwa umekwisha ingiwa na baridi, kama moyo wa mama yeyote ungefanya. Alikuwa karibu kufunua kila kitu ili apate kumwona mtoto wake mara nyingine tena. Huu ni mfano wa hisia zisizokuwa na mantiki. Ndiyo anaweza kumwona mtoto wake, lakini hiyo ingeleta kifo cha kweli! Kwa hivyo, akachagua mpango unaofuata na ambao ungewezekana, na ambao ulikuwa wa mantiki na bado ungeweza kutuliza moyo wake. Akamtuma binti yake aende amwangalie kaka yake—afuate kikapu kilichokuwa mtoni. Dada yake Musa, Miriamu, alitazama kwa hofu kikapu kikienda na mto na kuingia ndani ya tundu la simba, kwenye jumba la Firauni! Alikaribia ili kujua hali ilivyokuwa, akagundua kwamba Musa alikuwa analia sana kwa sababu alikuwa na njaa lakini aliwakataa wauguziwote wakunyonyesha. Aliingia na kupendekeza huduma za mama yake. Huku akimtegemea Mungu, na bado akiwa na mpango wa pili, mamake Musa alihakikisha kwamba mtoto wake angebaki salama.
Somo la Nne: Mungu hatimizi ahadi yake tu, bali anapena zaidi
Mungu alimwahidi mamake Musa kwamba angeungana tena na mwanawe. Alipewa amri mbili naye akazitimiza. Na kisha, Mungu kwa Rehema yake, aliwaleta pamoja tena mama na mtoto wake. Badala ya kuwa na maisha magumu ambapo angejitahidi sana kumficha mwanawe asiuawe, sasa alilindwa na watu wale wale ambao walitakiwa kumwua. Zaidi ya hayo, sasa alikuwa mfanyakazi katika Kasri la Kifalme na alikuwa analipwa kufanya kile ambacho angekifanya kivyovyote—kumtunza mwanawe! Mungu alimuahidi kurudi kwa mtoto wake, lakini Mungu hakutimiza ahadi yake tu bali alimpa hata zaidi. Kama Mwenyezi Mungu asemavyo katika Qur'ani,"Na anaye mcha Mwenyezi Mungu humtengezea njia ya kutokea. Na humruzuku kwa jiha asiyo tazamia. Na anaye mtegemea Mwenyezi Mungu Yeye humtosha." (Kurani 65:2-3)
Ongeza maoni