Eric Schrody, Mkatoliki wa Zamani, Marekani (sehemu ya 2 kati ya 2)
Maelezo: Mazungumzo na mwimabji wa zamani wa rapu, nyota EverLast na safari yake ya kuelekea Uislamu. Sehemu ya 2.
- Na Adisa Banjoko (interviewer)
- Iliyochapishwa mnamo 14 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 5,123 (wastani wa kila siku: 5)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
AB: Familia yangu ilijaribu hivyo. Kusema kweli, siwezi kuelewa hilo. Lakini unajua nini? Hilo ni mtihani. Ingawa nimebadilisha jina langu kwa miaka kama nane sasa, bado wananiita kwa jina langu la kuzaliwa. Kisha ni, “Oh Nimesahau wewe ni Muislamu.” Kisha ni utani wa nyama ya nguruwe. Haiishi kamwe.
E: Ni mojawapo ya mambo ambapo watu huchekelea kile ambacho hawakielewi. Au wanaogopa wasichoweza kukifahamu. Ukweli ni kwamba hakuna mtu anayeweza kujifanya kuwa haelewi. Kwa sababu sijawahi kukutana na kitu chochote rahisi zaidi kuliko uislamu katika maisha yangu.
Kwa mfano ninakumbuka kwamba nilipokuwa nikiketi na kuuliza, “Sasa, Muislamu anaamini nini,” na nikapewa orodha ya vitu kadhaa. Nikasema, “Hamuweki ukuta kati ya Ukristo na Uyahudi.” Wakasema, “La, ni mambo yale yale.”
Ikiwa utaketi chini na kusoma Qurani, Biblia na Torati, ambayo ni Agano la Kale tu, utaona kwamba Qur'ani ni uthibitisho wa yaliyo sahihi na yasiyo sahihi ndani ya vitabu hivyo (Biblia na Torati). Na kisha unajiambia, “Jinsi gani jambo hilo lilitokea ilhali vitabu hivi vilishuka katika sehemu tofauti tofauti ardhini?” Lakini vyote vinathibitisha mafundisho ya kila moja.
Sahii ninasoma kitabu kinachoitwa Muhammad: Maisha ya Mtume, cha Karen Armstrong. Iliandikwa na mtu ambaye si Mwislamu. Kwa sasa, niko karibu kufika robo ya kitabu hicho; lakini inaanza kukueleza jinsi walivyojaribu kumfanya Muhammad aonekane kama mtu mbaya zaidi duniani; kwamba alianzisha Uislamu kwa kutumia upanga. Lakini unajifunza baadaye kuwa Muhammad alipigana tu ilipobidi apigane. Muhammad alipigana tu ili kulinda Uislamu. Ni kitabu kizuri sana kuhusu mtume. Inakuwezesha kujua kwamba alikuwa binadamu tu. Hatujaribu kukuambia kwamba alikuwa kitu kingine chochote isipokuwa mwanadamu. Tunakuambia kama Waislamu kwamba alikuwa mfano kamili kabisa wa mwanadmu bora aliyewahi kutembea ardhini mpaka sasa. Na kutokana na kile nilichokisoma yeye ndiye wa mwisho kuja wa aina yake.
Unapojiondolea woga wa Farrakhan na anachosema -- na hapa ninaongea kama mtu mweupe -- unapopita kiwango cha ujahili wa kuamini kuwa Uislamu unahusiana tu na watu wanaolipua vitu, unakuja kuelewa kuwa hao hawana uhusiano wowote na Uislamu. Wanaweza kufanya mambo yao kwa jina la Uislamu. Lakini hawahusiani na Uislamu. Huwezi kubishana na hilo.
Ninapoeleza kuhusu Yesu kwa Mkristo, hawezi kubishana na mimi. Wala simaanishi abishane kwa kusema, “Yesu si Mungu!” Namaanisha, ni mantiki ya kiasi gani iko katika kusema kuwa yeye ni mwanadamu? Kama ningekuwa Mkristo, ambayo kwangu ina maana ya kuwa kama Kristo, na Mungu aniulize, “Kwa nini hukuwa kama Yesu?” Nitasema, Sikuwa kama Yesu kwa sababu umemfanya awe nusu Mungu [na] mimi ni mwanadamu tu?” Hiyo haileti maana yoyote.
Mungu hataki mambo yawe magumu kwetu. Mwenyezi Mungu anataka mambo yawe mepesi iwezekanavyo. Mungu atayafanya yawe rahisi iwezekanavyo. Ukiuliza, ilhali wewe ni mkweli, Mwenyezi Mungu atakupa. Anaweza kuweka baadhi ya mawe kwa njia yako, ili uteleze na ujikwae. Lakini utaipata hatimaye.
AB: Niambie kuhusu mara ya kwanza na ya pili ulipochukua Shahadah yako (ushuhuda wa imani).
E: Kwa mara ya kwanza ilikuwa ni baada ya kusikia kanda kutoka kwa Warith Deen Muhammad (mwana wa mwanzilishi wa Taifa la Islam Elijah Muhammad, ambaye alipeleka sehemu kubwa ya Taifa la Uislamu kwa Uislamu wa kawaida). Alieleza vizuri mambo yote kuhusiana na Yesu. Alifafanua kwamba sisi (Waislamu) tunawafanyia Wakristo hisani kubwa kwa kumleta Yesu chini kwa kiwango cha mwanadamu. Kwa nini Mungu amuumbe mtu ambaye ni nusu Mungu na kutulinganisha naye? Na hilo lililipua bomu katika kichwa changu. Hivyo nikachukua Shahadah. Na kisha hisia za awali zikaisha.
Ni kama Mkristo anayesema kwamba anamkubali Yesu. Kisha anasema, “Haijalishi ninachofanya sasa, nimeokoka.” Kwa sababu nililelewa na mawazo ya aina hayo. Yaani, “ Nakubali ukweli sasa, hivyo basi wacha tu niende zangu na nifanye madhambi ninayoyataka kwa sababu nimeokoka.”
Kwa kweli sikujidai kuwa Muislamu wakati huo. Nilichukua na kuchagua nilichotaka kuamini. Mungu alinipa nafasi kwa muda. Lakini hatimaye wakati uliwadia. Nilifika kiwango ambapo sikuridhika kihisia na kiroho. Nilikuwa na pesa kwenye benki na gari la dola 100,000, wanawake kushoto na kulia -- kila kitu unachofikiri unakitaka. Na kisha nimekaa tu hapo nikiwaza, “Mbona sina furaha?” Hatimaye sauti hiyo inayozungumza nawe -- sio minong'ono (ya Shetani) -- sauti ikasema, “Naam, kimsingi huna furaha kwa sababu unaishi maisha machafu na hutaki kujaribu kufanya chochote kuhusu hilo.”
Ukaidi wangu wakati huo haungeweza kuniruhusu kuzungumza juu ya hilo wakati huo. Unaingia katika hali hiyo ya akili ambapo unajiambia, “Ninaweza kutatua haya yote peke yangu.”
Hatimaye nilipata unyenyekevu wa kutosha kuzungumza na Divine na Abdullah kuhusu hilo. Wakaniuliza, “Unasikiaje? Unafikiri ni nini?” Kwa hivyo hatimaye nimeketi hapo nikichukua Shahadah tena. Kutoka wakati huo nimejiahidi kuwa nitajaribu kwa kadri ya uwezo wangu. Nitajitahidi sana kuswali sala zangu, hebu tuanze huko. Tusijilaumu vibaya kwa sababu tulitoka jana usiku na kulewa. Hebu tuswali sala zetu na kuomba tupate nguvu ya kuacha kufanya jambo moja kwa wakati. Hiyo ndio bado nashughulika nayo.
Unajua, mara baada ya kujiondolea mambo makubwa, mengine yatafuata kichini chini tu. Unaweza kumwona mtu, na hata usimzungumzie vibaya, lakini unamsengenya akilini. Yale yaliyo rahisi kuyashinda -- sipaswi kusema rahisi -- yale makubwa ni rahisi kuyaona. Ni mabadiliko madogo madogo ya kisaikolojia yasiyoonekana ambayo hukusaidia kubadilika vizuri. Lazima uwe na uwezo wa kukubali ukweli wa hali yako. Kama huwezi kukubali ukweli wako na kujua wewe ni nani, utabomoka kwa urahisi.
Watu wananiuliza , “Wewe ni Muislamu?” Nasema, “Naam, mimi ni Muislamu, lakini mimi pia ni mfanya dhambi mtaalamu.” Najaribu kuziacha, najaribu kustaafu. Siwezi simama mbele na kusema mimi ni bora kuliko wewe. Ninaamini tu kwamba nimeonyeshwa ukweli na ninatumai ukweli huo utaniokoa.”
Adisa Banjoko ni mwandishi huru katika eneo la Bay la San Francisco.
mada
Ongeza maoni