Ni Nini Huwachochea Watu Kusilimu? (sehemu ya 1 kati ya 2)
Maelezo: Vipengele mbalimbali vya Uislamu ambavyo huwahamasisha watu kusilimu licha ya taswira mbaya kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari.
- Na Based on an article at iqrasense.com
- Iliyochapishwa mnamo 09 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 10 Apr 2022
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,590
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Tabia ya imani ya kidini ni ya ajabu sana. Kama sehemu ya imani zao za kidini, watu huamini miungu mbalimbali. Kuna watu ambao wana imani ya kidini katika nguvu kuu ya ghaibu isiyo na kifani, na kisha kuna wengine ambao wanaamini wanadamu fulani kuwa miungu, au wanyama (k.m. tumbili), moto, masanamu yaliyotengenezwa kwa mawe, na orodha inaendelea.
Mengi yamehusishwa na kuwa na "imani" ya kidini. Sehemu yake fulani inahusiana na imani zilizopitishwa kupitia vizazi. Utambulisho wa watu, kwa hivyo, hufungamana nayo. Mara nyingi, imani hizi na hisia zinazohusiana nazo haziwezi kuthibitishika kwa ukamilifu kwa kutumia akili au hoja za kimantiki. Hakuna lisilo sahihi au kosa katika jambo hili, lakini hivyo ndivyo tu asili ya imani ya kidini imekuja kuwa.
Karibu kila mtu hufikiria imani yake ni sawa. Kuwa pamoja na watu na makundi yenye imani sawakunaimarisha zaidi imani za watu, na huiona ni sawa, ingawa hoja za kimantiki na majadiliano wakati mwingine haziwezi kuelezea yote hayo. Hiyo ni saikolojia rahisi ya kibinadamu.
Hoja za Uislamu kulingana na hoja za kiakili
Hata hivyo, Waislamu wanaamini kwamba dini ya Kiisilamu ni tofauti katika muktadha huu. Mtu anaweza kutoa hoja kuwa sawa na imani zingine kuna mambo yake fulani ambayo hayawezi kamwe kuelezwa kwa kutumia akili, lakini kwa upande mwingine maandishi ya Kurani, ambayo ni maneno ya Mungu yanayowazungumzia wanadamu wote, hutumia busara, fikira za kina, na mchakato wa mazingatio kama njia sio tu ya kuimarisha imani ya waumini, bali pia kuwaita wasioamini kutafakari juu ya ukweli wa Uislamu kama njia ya maisha kwa wanadamu kwa ujumla. Ingawa hakuna imani ya kidini inayoweza kutegemea kikamilifu mantiki na hoja, Uislamu na Kurani hutoa mifano zaidi ya kutosha na fursa ya kuchunguza ukweli na utimilifu wa ujumbe wake kupitia darubini ya ushahidi wa majaribio na maarifa.
Hakuna mtu (Muislamu au asiye Muislamu) atakayebisha kuwa fikira za kina na mazingatio yanaweza kuwa kichocheo kikubwa cha kubadilisha maisha. Fikira makini zimetumiwa na wengi kuboresha maisha yao kwa sababu tu mhakiki makini huuliza maswali ya uchunguzi juu ya hali, hukusanya taarifa nyingi ziwezekanazo, hupima maoni ambayo yalikusanywa na yaliyotokana na muktadha wa habari inayopatikana, huwa na utayari wa kusikiliza na kukubali maoni mbalimbali au tofauti bila upendeleo wowote, na huchunguza kwa uangalifu mawazo na kutafuta njia mbadala.
Hii ndio sababu, kwa hivyo, Waislamu wapya waliosilimu waliweza kutumia busara, mazingatio na kufikiri kwa kina wakati wa kuelezea safari zao za kuwa Waislamu. Watu kama hao waliweza kusalimika na hisia kali zilizoundwa na vyombo vya habari ambavyo viliumulika Uislamu kwa njia ya kuukosoa na havikuweza kuwayumbisha waliosilimu kuufuata ukweli uliowajia kwa njia ya kimaumbile. Je, mtu anaweza kuelezea vipi kuongezeka watu kusilimu kutokana na ongezeko la matamshi ya wapingaji Uislamu? Je, mtu ataelezea vipi wahubiri wengi zaidi wasio Waislamu wamekuwa wakiingia katika Uislamu kuliko zamani? Ingawa, kama Waislamu, tunaamini kwamba uongofu unatoka kwa Mwenyezi Mungu pekee, matumizi ya hoja za kiakili za mtu alizojaaliwa na Mungu zina mchango mkubwa sana kwa Waislamu waliosilimu kufanya uamuzi huo wa majaaliwa. Na pindi waliposilimu, ni nadra wao kurudia imani zao za awali, kwa sababu imani ambayo misingi yake imejengwa juu ya mantiki na akili ina uwezekano mdogo wa kutikiswa kuliko ile ambayo hujengwa tu juu ya seti za ibada na sakramenti.
Sababu zinazohusishwa na Waislamu wapya
Baadhi ya sababu zinatolewa kuelezea kwa nini watu husilimu ni ufasaha wa lugha ya Kurani, ushahidi wake mwingi wa kisayansi na uthibitisho, majadiliano yanayokita mizizi katika hoja za kiakili, na hekima ya Mwenyezi Mungu katika masuala mbalimbali ya kijamii. Upekee na uzuri wa maandishi ya Kurani umekuwa ukiwastaajabisha wanaisimu na wanazuoni bora wa Kiarabu, Waislamu na wasio Waislamu, tangu siku ilipoteremka hadi leo. Kadiri watu wanavyokuwa na ujuzi katika lugha, ndivyo wanavyozidi kuthamini maajabu ya ufasaha wa maandishi ya Kurani. Zaidi ya miaka 1400 iliyopita ilipofunuliwa, Kurani pia ina ukweli mbalimbali wa kisayansi ambao umeweza kuthibitishwa na sayansi katika zama hizi. Isitoshe, ni maandishi pekee ya kidini yanayojulikana kutoa changamoto kwa wanadamu kufikiri, kuzingatia na kusaili juu ya uumbaji kwa ujumla, masuala ya kijamii, uwepo wa Mungu, na mengine zaidi. Kurani, kupitia mifano kadhaa, huwapa watu changamoto ya kutafakari na kufikiri wao wenyewe, badala ya kusikiliza mazungumzo potofu ya wale ambao ukosoaji wao umeegemezwa kwenye misingi isiyo thabiti. Hatimaye, Kurani inatoa suluhisho kwa masuala mbalimbali ya kijamii, tofauti na ilivyo ada ambako kumejulikana kusababisha machafuko ya kijamii katika ngazi zote.
Kurani ni kauli ya kujiamini ya Aliye Mkuu; kitabu pekee cha dini chenye kujulikana kuwa na uthibitisho wa kujiamini wa Aliye Mkuu kuhusu masuala yote kuanzia uumbaji wa ulimwengu hadi vipengele kadhaa maalumu vya mazingira ya kijamii. Fauka ya hayo, Maandishi yake ya Kiungu - lugha na nathari ya Kurani - ni tofauti sana na lugha katika hadithi za Mtume, ambayo hudhihirisha kuwa Kurani haitoki kutoka kwa mawazo ya kiubunifu au maneno yaliyoteremshwa kama wahyi kwa Mtume Muhammad, kama vile walivyodai wengi waliotilia shaka hapo zamani, na wanaendelea kufanya vivyo hivyo hata leo.
Tunaweza kuona kwamba nyingi ya sababu hizi zinaweza kuhusishwa tu na mchakato wa kufikiri kwa kina na mazingatio ya kiakili. Walakini, hoja baridi au hoja zinazopuuza mitazamo mbalimbali hazitoshi. Moyo unapaswa kushirikishwa katika utafutaji: utafutaji ambao lengo lake ni kufikia msingi wa ukweli. Si ajabu, basi, kwamba wakati watu waaminifu kama hao wanaposikia Kurani kwa mara ya kwanza, na kuielewa, wanasema;
“...Tunaiamini. Hakika hii ni Haki inayotoka kwa Mola wetu Mlezi. Hakika, sisi kabla yake, tulikuwa ni Waislamu; tulionyenyekea!” (Kurani 28:53)
Ni Kitu Gani Kinachowachochea Watu Kusilimu? (sehemu ya 2 kati ya 2)
Maelezo: Changamoto ya Kurani kwa wenye akili.
- Na Based on an article at iqrasense.com
- Iliyochapishwa mnamo 22 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,111
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Kurani inawapa changamoto wanadamu wote kufikiria na kuzingatia kuhusu mambo yao katika hali mbali mbali. Haya ni baadhi ya yale ambayo Kurani inayaelezea:
·Namna hivi tunazipambanua ishara zetu kwa watu wanaofikiri. (Yona, Kurani 10:24)
·Je, hawajifikirii nafsi zao? Mwenyezi Mungu hakuumba mbingu na ardhi na viliomo ndani yake ila kwa Haki na kwa muda maalumu. Na hakika watu wengi bila ya shaka ni wenye kukataa kuwa watakutana na Mola wao Mlezi. (Warumi, Kurani 30:8)
·Yeye ndiye aliyekujaalieni usiku mpate kutulia humo, na mchana wa kuonea. Hakika katika haya zipo ishara kwa watu wanaosikia. (Yona, Kurani 10:67)
·Ati anadhani binadamu kuwa ataachwa bure? (Ufufuo, Kurani 75:36)
·Je, mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa? (Waaminio, Kurani 23:115)
·Au wewe unadhani kwamba wengi wao wanasikia au wanaelewa? Hao hawakuwa ila ni kama nyama hoa tu, bali wao wamepotea zaidi njia. (Kigezo, Kurani 25:44)
·Je, hawafikiri? Huyu mwenzao hana wazimu. Hakuwa yeye ila ni mwonyaji aliye dhahiri. (Urefu, Kurani 7:184)
·Lau kuwa tumeiteremsha hii Kurani juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeliuona ukinyenyekea, ukipasuka kwa khofu ya Mwenyezi Mungu. Na hiyo mifano tunawapigia watu ili wafikiri. (Mkusanyiko Mkubwa, Kurani 59:21)
Tunapochunguza visa vingi vya Waislamu wageni waliosilimu, tunaona kwamba wakijishughulisha na kufikiri kwa kina na hoja za kimantiki ni sababu yao kubadili imani zao zisizo za Kiislamu - imani zile zile ambazo hapo awali zingedhaniwa kuhamisha milima, lakini zilishindwa na sauti ya akili inayosikika kwa urahisi katika mizizi ya Uislamu. Mchakato tu wa kufikiri na kutafakari hudhihirisha mengi waziwazi ambayo yangebaki kufunikwa na pingamizi na nguvu za wachambuzi wanaochukia Uislamu. Wale ambao wamedhamiria kuona mabaya tu wanashindwa kuona nuru ya ukweli. Badala yake, wanajihusisha na uchanganuzi wa kijuujuu usioisha ili kuthibitisha bila mafanikio falsafa zao potofu.
Kuna takwimu nyingi kwenye vyombo vya habari zinazoangazia kasi ya ajabu ambayo watu husilimu. Ingawa, usahihi wa vyanzo hivi vyote haujathibitishwa, kwa madhumuni ya makala hii baadhi yao ni pamoja na yafuatayo:
·Kulingana na "The Almanac Book of Facts", idadi ya watu iliongezeka 137% katika mwongo mmoja uliopita, Ukristo uliongezeka 46%, wakati Uislamu uliongezeka 235%.
·Ripoti ya TV: Wajerumani 4,000 HUSILIMU Kila Mwaka.
·Karibu watu 25,000 husilimu kila mwaka nchini Uingereza pekee.
·…mifano mingi zaidi ipo.
Vipi kuhusu Waislamu?
Iwapo sauti za kutumia akili zinazopatikana ndani ya mafundisho ya Uislamu husababisha wasio Waislamu kurejea katika Uislamu kwa wingi, basi kwa nini Waislamu wengi waliozaliwa katika dini hii kawaida hushindwa kufuata kikamilifu, na kwa hivyo kufurahia, mafundisho ya dini? Ukweli ni kwamba inaweza kuwa Waislamu wengine wamekosa kutumia fikira kwa kina na mazingatio, hali inayolazimisha ulimwengu wa Kiislamu kuonekana kuwa na maisha duni kwa ujumla. Uislamu na mafundisho yake unaahidi kutimiza maisha ya kuridhisha na yenye amani kwa wote. Walakini Waislamu wanaendelea kupuuza mambo ya kimsingi na kujitatiza katika masuala ya kijamii na maadili yanayosababisha maumivu yasiyofaa na mateso kwao na familia zao. Ukweli ni kwamba ikiwa wangefikiria na kutafakari juu ya mafundisho ya dini yao wenyewe, wangeweza kuepuka matatizo mengi na changamoto zinazowakabili.
Ujumbe
Kwa wasio Waislamu ambao wameutafuta Uislamu na kuujua kijuujuu na wanaweza kukengeushwa na viongozi wale wapotofu wa dini hii pamoja na sauti za upendeleo kwenye vyombo vya habari, ujumbe kwao ni rahisi - jaribu kutazama mafundisho ya Uislamu kwa umanikinifu. Inawezekana kwamba utaweza kupata sababu zaidi kuliko vile ambavyo hapo awali ungefikiria hazikuwepo. Kwa Waislamu, ujumbe ni kwamba wakati mwingine hatuthamini mafundisho ya dini yetu wenyewe kwa sababu hatufikirii na kukua zaidi ya matendo machache ya kidini katika kuendesha maisha yetu. Juhudi makini za kujifunza, kufikiri na kutafakari zaidi zitatusaidia kukaribia mafundisho ya kidini kwa njia ambazo zinaweza kuboresha maisha yetu kwa kiasi kikubwa.
Ongeza maoni