Maelezo ya Kurani kuhusu tando za buibui (sehemu1 kati ya 2)
Maelezo: Aya ya Kurani inaonyesha kwa usahihi udhaifu wa kijamii wa nyumba ya buibui ambao tumeanza kuujua na kuuelewa hivi karibuni.
- Na IslamReligion.com
- Iliyochapishwa mnamo 23 Nov 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 4,466
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
"Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua." (Kurani 29:41)
Aya hii ya Kurani inatoka katika sura ya 29, Buibui. Sehemu tunayoangalia hapa ni kwamba Mungu anataja kuwa nyumba dhaifu zaidi ni ile ya buibui. Katika lugha tajiri ya Kiarabu, neno “Awhan” linatafsiriwa kuwa (dhaifu zaidi); na kuangalia zaidi katika maana hiyo kunaonyesha kwamba inamaanisha udhaifu mkubwa na kutokuwa na msaada kimwili na kiakili.
Kutokana na upanuzi wa utafiti wa maumbile na wanyamapori katika karne ya 20 na 21, wanasayansi wamefichua, wamerekodi na kupiga video mambo ya ajabu kikweli katika maisha ya buibui.
Uwindaji wa ngono
Kati ya aina zaidi ya 45,000 za buibui zinazojulikana , ni kawaida sana buibui wa kiume kuuawa na kuliwa na wenzi wao wa kike[1]; neno linalojulikana kama uwindaji wa ngono. Haijulikani kwa nini hii inatokea, hata hivyo, nadharia moja iliyopendekezwa na wanasayansi ni kwamba mwili wa kiume humpa mwanamke virutubisho vinavyohitajika sana vinavyomwezesha kutaga mayai yenye afya. Utafiti uliofanywa na Kituo cha Majaribio cha Hispania cha Eneo la Ukame umebaini kuwa katika aina nyingi za buibui, wanawake huwaua wenzi wao bila kujali kama ndume anaonekana kuwa duni au la.[2] Katika aina nyingi, buibui wa kike humuua hata kiume yeyote ambaye hana nia ya kushirikiana naye kimapenzi.[3]
Katika baadhi ya aina za buibui, kama vile buibui mvuvi mweusi, buibui wa kiume hufa moja kwa moja baada ya kujamiana kutokana na sababu za ndani; na kisha huliwa kikatili na bibi yake. [4] Katika aina zingine za buibui, buibui wa kiume hufa moja kwa moja baada ya kujamiana mara chache tu, na katika idadi kubwa ya aina za buibui, wale wa kike huwa na umri mrefu kuliko wa kiume; huku viume huishi kwa miezi michache tu na wa kike kwa miaka michache.
Wanapokuwa na bahati nzuri ya kujamiana na kufanikiwa kuishi, buibui wa kiume wenye miili ndogo, huku wakijua hulka ya mwenzio ya uwindaji, hukimbia hapo hapo kwa ajili ya kuokoa maisha yao [5] na kumuacha mwenzao wa kike akilea pekee yake mayai ya idadi tofauti kutoka machache hadi kufikia karibu na mayai elfu. Hiyo ndio hali ya Buibui Mzururaji wa Brazil.
Maajabu zaidi katika mila hatari ya ngono ya buibui, utafiti uliyofanywa na watafiti Lenka Sentenska na Stano Pekar, kutoka Chuo Kikuu cha Masaryk katika Jamhuri ya Cheki mwaka wa 2013, uligundua kuwa katika aina ya buibui ya 'Microcaria Sociabilis' ya buibui inayojulikana kama mjane mweusi, buibui wote wa kike na wa kiume kawaida huuana na mwenye uwezo humla mwenzake baada ya kujamiana; na kwamba katika aina hii kwa mahususi, kinyume na kile kilichoaminika mbeleni, buibui wa kiume huua zaidi na kula mwenzao kuliko buibui wa kike.[6]
Maisha ya buibui wadogo
Katika aina nyingi, buibui wadogo waliozaliwa karibuni wana mama yao tu wa kuwalisha na kuwalinda. Chakula kinapokuwa kichache mama analazimika kuwalisha mayai yake yasiyoanguliwa; hivyo buibui mdogo lazima apitie mshtuko na changamoto ya kula ndugu zake ambao hawajaanguliwa bado ili aendelee kuishi.[7]
Wakati hakuna mayai mengine ya kula tena, na hakuna wadudu wa kutosha wa kuanguka kwenye utando au hawakupatakiana na mama, uchunguzi mwingine unaonyesha ya kwamba buibui wadogo, baada ya kukata tamaa, hugeukiana wenyewe na kila mmoja kumla mwenzake, na utando mdogo huo wenye msongamano hugeuka kuwa jela ya mauaji. Kwa kukosa msaada, buibui mama pia huwaua na kuwala wadogo wake ili kuweza kuishi siku nyingine.
Vielezi-chini:
[1]Pappas, Stephanie. Juni 2016. Male Orb-Web Spiders Are Choosy About Their Cannibal Mate. Live Science. Imetolewa http://www.livescience.com/54944-male-orb-web-spiders-choosy-about-cannibal-mate.html
[2]Gannon, Megan. Aprili 2014. Food vs. Sex: Why Some Female Spiders Eat Males Before Mating. Live Science. Imetolewa http://www.livescience.com/45066-virgin-female-spiders-eat-males.html
[3]Gannon, Megan. Aprili 2014. Food vs. Sex: Why Some Female Spiders Eat Males Before Mating. Live Science. Imetolewa http://www.livescience.com/45066-virgin-female-spiders-eat-males.html
[4]Lewis, Tanya. Juni 2013. Tough Love: Male Spiders Die for Sex. Live Science. Imetolewa http://www.livescience.com/37536-spiders-die-for-sex.html
[5]Szalay, Jessie. Desemba 2014. Tarantula Facts. Live Science. Imetolewa http://www.livescience.com/39963-tarantula.html
[6]Cadieux-Shaw, Lillianne. Mei 2013. Study: Male Black Widow Spiders eat their Mates too. Canadian Geographic. Imetolewa http://www.canadiangeographic.ca/article/study-male-black-widow-spiders-eat-their-mates-too
[7]Englehaupt, Erika. Februari 2014. Some Animals …facts. Science News. Imetolewa https://www.sciencenews.org/blog/gory-details/some-animals-eat-their-moms-and-other-cannibalism-facts
Kurani kwenye Wavuti wa Buibui (sehemu ya 2 kati ya 2)
Maelezo: Mfano mwingine wa machafuko ya kijamii kwenye utando wa buibui - ulaji wa mama. "Kuzimu" iliyo hai ya nyumba ya buibui ni ukumbusho wa matokeo ya ushirikina.
- Na IslamReligion.com
- Iliyochapishwa mnamo 17 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 3,685
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Ulaji wa mama
Walakini sehemu ya kushangaza zaidi ya hifadhi ya buibui ni kile kinachotokea wakati buibui wa kike amefikia kiwango cha kukata tamaa na kuwa na wasiwasi na hawezi tena kuwaweka watoto wake hai. Baada ya kupoteza labda mamia ya watoto wake na bado kubaki na buibui mia kadhaa zaidi; mama, kwa kushangaza, anajitolea mwili wake kama chakula kwa watoto wake kwa kufungua silika ya uuaji ambayo huwafanya wamshambulie na kumla akiwa hai! Utaratibu huu wa kikatili unajulikana kama ulaji wa mama au "kula mama".[1]
Kinacho julikana, hadi sasa, ni kwamba ulaji wa mama ni mchakato unao anzishwa na buibui wa kike na njia zake hutofautiana kutoka aina moja ya viumbe hadi nyingine. Buibui wenye sumu humpa sumu mama yao hadi kufa; lakini katika hali zote ulaji wa mama ni mchakato wa polepole na mchungu ambao huchukua wiki kadhaa kabla ya buibui mama kufa kwa kuwa maji ya mwili wake hatimaye huliwa na watoto wake.[2]
Mchakato kama huo umeangaliwa na kuandikwa katika buibui wa ardhini, buibui aina ya Stegodyphus lineatus[3] na buibui aina ya kaa na kupitia utafiti zaidi tu ndipo inaweza kubainika jinsi ulaji wa mama ilivyoenea katika ulimwengu mbaya wa buibui.
Kwa kurejea nyuma, katika ulimwengu wa kuzaliana kwa buibui, mara nyingi husababisha kifo cha buibui wa kiume na wa kike kua mjane; mama ameachwa peke yake na, kwa wastani, watoto mia kuwalisha na kuwalinda kutoka kwa wanyama wanaowinda, hulazimika kuwalisha watoto wake mayai ambayo hayajatoka ili waendelee kuishi, na kawaida hula watoto wake ili kuwa hai. Buibui wadogo pia hubadilika kuwa walaji na huua na kulana wenyewe kwa wenyewe; na mwishowe na kwa kushangaza zaidi, katika hali mbaya buibui mama hujitoa mhanga kuliwa na watoto wao wenyewe. Matokeo ya mwisho, angalau, ni mamia ya buibui huokoka na kuacha mateso ya kwenye utando.
Sasa, kwa kujua asili ya ukatili ya nyumba ya buibui, Asifiwe Mungu Mwenyezi, Ambaye alitaja kuwa nyumba mbaya zaidi ni ile ya buibui, muda mrefu kabla wataalamu wa asili na wanasayansi kuanza kusoma kwa undani tabia ya buibui. Sasa inaweza kusemwa, kama ukweli, kwamba maisha katika utando wa buibui ni ya kushangaza kabisa na baada ya kulinganishwa na nyumba za viumbe wengine, ni mbaya zaidi, katili na ya unyonge zaidi ya nyumba zote!!!
Ujumbe katika Aya ya Kurani
Kuna onyo dhahiri katika aya inayohusika ya Kurani. Mungu amefananisha wale wanaochukua washirika au miungu, pamoja naye katika ibada, na wale wanaochukua utando wa buibui kama nyumba yao. Quran na mila halisi ya Mtume Muhammad, rehema na baraka za Mungu ziwe juu yake, zote ziko wazi kabisa kwamba ni Mungu tu, Muumba wa yote, anayestahili kuabudiwa, moja kwa moja, sio kupitia kwa wapatanishi au washirika wowote. Hii inajulikana kama Kuabudu Mungu Mmoja.
"Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote" (Kurani 4:36)
"Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake na kaumu yake: Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayo yaabudu, Isipo kuwa yule aliye niumba, kwani Yeye ataniongoza. " (Kurani 43:26,27)
Ujumbe wa Uislamu na Manabii na Mitume wote ni kumwabudu Mungu peke yake na kwamba kumwabudu Mungu kupitia wapatanishi au washirika kama manabii, malaika, watu wacha Mungu, wanyama, viumbe, vitu au chochote ni ushirikina; kaburi la dhambi zote. Matendo yote ya ibada, pamoja na dua, sala, na kuchinja wanyama inapaswa kuelekezwa kwa Mungu tu.
Kurani inataja kwamba washirika hawa hawawezi hata kujibu (na wakati mwingine, hata kuona au kusikia) maombi ya mtu anayewaomba. Ndivyo ilivyo wakati mtu akienda kimakosa kwenye kaburi la Nabii, au mtu mcha Mungu aliyekufa, au sanamu na kuomba na kuwaomba wamsamehe dhambi zake au wamponye na ugonjwa. Waliotajwa hapo awali hawana uwezo wa kufanya yanayo hitajika. Kwa kuongezea, Mungu anataja hilo kwamba hakuwahi kuamuru kiumbe chochote cha uumbaji wake kuwa na washirika Naye; kwa ukweli wanadamu wote waliumbwa na silika safi kwamba Mungu Mwenyezi ni Mmoja na kwamba Yeye Peke Yake ana haki ya kuabudiwa.
Dhambi Isiyosameheka
Dhambi kubwa kuliko zote, ushirikina, ni kuhusisha kitu chochote na Mwenyezi Mungu katika ibada. Hii ni dhambi moja ambayo Mungu amesema kwamba hatasamehe huko Akhera; wakati dhambi zingine zote zinaweza kusamehewa.
Fikiria udhalimu wa mtu aliyeumbwa na Mungu (kwa upole na kwa huruma ndani ya tumbo la mama yake) baada ya kuwa si kitu, aliyepewa zawadi ya roho, alibarikiwa na ubongo, moyo, kuona, kusikia, hisia, makazi, ardhi nzuri na ya kupendeza iliyojaa mimea na wanyama wa kula, na malighafi ambayo wanadamu wametumia kujenga miji na miundombinu; alafu mtu huyu haitoi sifa, shukrani na ibada kwa Mwenyezi Mungu, badala yake anatoa hivyo kwa uumbaji wa Mungu (ambavyo havikufanya chochote kwa zilizotajwa hapo juu). "Na Luqman alipo mwambia mwanawe kwa kumpa mawaidha: Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu. Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa."(Kurani 31:13)
Wale ambao hufa, bila kutubu kutokana na kuabudu asiyekuwa Mungu, watapata hasara huko Akhera. Ama washirika wa kibinadamu ambao walikuwa wakiabudiwa katika maisha haya watajitenga na watu ambao walikuwa wakiwaomba. Wakati, washirika wasio wa kibinadamu watageuka na kuwasaliti watu ambao walikuwa wakiwaabudu; na atasema (Mungu atawapa uwezo wa kusema) kwamba kwa kweli hakuna mtu aliyekuwa akiwaabudu kweli. Kama matokeo, wavamizi na washirika wasio wa kibinadamu katika ibada watawekwa kuzimu. "Na alisema: Hakika nyinyi mmeyashika masanamu badala ya Mwenyezi Mungu kwa mapenzi yaliyo baina yenu katika uhai wa duniani. Kisha Siku ya Kiyama mtakataana nyinyi kwa nyinyi, na mtalaaniana nyinyi kwa nyinyi. Na makaazi yenu ni Motoni. Wala hamtapata wa kukunusuruni'"(Kurani 29:25)
Kwa hivyo wavuti wa buibui unaweza kulinganishwa na Kuzimu, mahali penye shida na tabu. Buibui mama ambaye alitoa uhai wake, ili watoto wake waweze kuishi, anaweza kulinganishwa na mtu ambaye alikuwa akiabudu washirika wengi tofauti (watoto wa buibui wengi) na Mungu. Kwa kuwa washirika wasio wa kibinadamu ambao walikuwa wakiabudiwa pia watakuwa kuzimu na watamsaliti mtu ambaye alikuwa akiwaabudu, matokeo yake yatakuwa maumivu yasiyoweza kuvumilika na mateso ya mtu huyo, sawa na jinsi buibui wanavyosaliti na kumgeuka mama yao na ndio sababu ya mateso yake kwenye utando. Ni katika maisha yajayo tu hakutakuwa na kifo; Kuzimu na Mbingu zitakuwa za milele.
Rejeleo la maelezo:
[1]Englehaupt, Erika. Februari 2014. Wanyama wengine hula mama zao, na ukweli mwingine wa ulaji nyama. Habari za Sayansi. Imetolewa kutoka https://www.sciencenews.org/blog/gory-details/some-animals-eat-their-moms-and-other-cannibalism-facts
[2]Tafadhali angalia: http://channel.nationalgeographic.com/wild/worlds-weirdest/videos/mother-eating-spiders/
[3]Zielinski, Sarah. Mei 2015. Mama wa wanyama hujitolea sana - wakati mwingine hata wao wenyewe. Habari za Sayansi. Imetolewa kutoka https://www.sciencenews.org/blog/wild-things/animal-moms-sacrifice-lot-%E2%80%94-sometimes-even-themselves
Ongeza maoni