James Den C. Bedico, Mkristo wa Zamani, Ufilipino
Maelezo: Mapenzi ya James kwa Uislamu yalianza kwa kujua dhana ya umoja wa Mungu, kuona jinsi Waislamu wanavyoswali na upendo na uaminifu wanayo kwa Mtume Muhammad.
- Na James Den C. Bedico
- Iliyochapishwa mnamo 14 Dec 2021
- Ilirekebishwa mara ya mwisho mnamo 18 Nov 2021
- Ilichapishwa: 0
- Imetazamwa: 2,817 (wastani wa kila siku: 2)
- Imekadiriwa na: 0
- Imetumwa kwa barua pepe: 0
- Ilitoa maoni kuhusu: 0
Nilikuwa nikiitwa Bwana James Den C. Bedico lakini sasa naitwa Bwana Afraz Saleem C. Bedico, mwanachama wa zamani wa Iglesia Ni Cristo au Kanisa la Kristo katika Jamhuri ya Ufilipino.
Iglesia Ni Cristo ni mojawapo ya makundi ya kikristo kubwa zaidi na kanisa la pili kwa ukubwa hapa nchini Ufilipino baada ya Kanisa Katoliki la Kiroma. Nilizaliwa, kulelewa na kubatizwa ndani ya Iglesia Ni Cristo kwa kuwa wazazi wangu, ndugu na dada, na wengi wa jamaa zangu ni wafuasi na wanachama wakubwa wa Iglesia Ni Cristo.
Utotoni mwangu, nilikuwa nikijihusisha sana na kila shughuli za kidini za Iglesia Ni Cristo huku nikienda kanisani kila Alhamisi na Jumapili. Sijawahi kukosa mkutano isipokuwa wakati nilipokuwa mgonjwa mahututi. Nilikuwa mmoja wapo wa waimbaji wa kwaya na wazazi wangu bado wanashikilia nafasi muhimu katika Kanisa, kama vile shemasi na shemasi wa kike. Nilisomea katika shule inayomilikiwa na Iglesia Ni Cristo ambapo wanafunzi wake wote ni wanachama wa kanisa. Kwa jumla, kwa miaka thelathini ya maisha yangu nilikuwa mwabudu katika Iglesia Ni Cristo. Sijawahi kuwa na nafasi ya kusikiliza mafundisho ya dini nyingine.
Kuhusiana na Uislamu, sikuwa na nia ya kujifunza hio dini kwa sababu ya Waislamu kuwa na wachache humo nchini Ufilipino. Aghalabu mara myingi niliwaona wakielekea nyumbani kwao; walionekana kuwa wa kabila moja, ukoo mmoja, au kundi la wenyeji wanaoishi katika visiwa vya mbali vya Ufilipino. Sijawahi kufikiri kwamba walikuwa na dini! Sijawahi kusikia neno “Uislamu” utotoni mwangu, au ni vile kwamba sikuwa makini na neno hilo. Kimsingi Uislamu hapa Ufilipino ni dini iliyosahauliwa. Ufilipino ni jamii inayoongozwa na Ukristo, hasa katika sehemu za kaskazini na za kati ya nchi. Katika sehemu ya kusini, Waislamu ni wengi sana kwa sababu wako karibu na Malaysia, nchi ya Kiislamu katika Asia ya kusini mashariki.
Miaka ilipopita, nilikuwa nikiondoka mbali na dini yangu, nilihisi kuwa 'tupu', kana kwamba ninatamani kitu fulani. Kisha mwanzoni mwa mwaka 2012, nilikuwa na ndoto ya ajabu kuhusu mtoto wa Kiislamu aliyevaa hijab iliyofunika mwili wake wote isipokuwa macho yake. Mtoto alikuwa na umri wa miaka 6. Alikuwa ananiangalia kwa umbali wa futi 5 kutoka mahali ambapo nilikuwa nimesimama na kisha akatamka maneno: “Assalamu Alaikum!” Niliamka nikiwa nimeshtushwa na kuchanganyikiwa...kwa nini nimekuwa na ndoto kama hiyo?
Baada ya kuota kuhusu huyo mtoto Mwislamu, nilitafuta kuhusu Waislamu mtandaoni na kuandika neno “Uislamu”, na moja ya tovuti zilizokuja ilikuwa www.islamreligion.com. Nilifungua hio tovuti na kushangaa kwa sababu sijawahi kufikiri kwamba Uislamu ulikuwa dini, na kwamba ulihubiri UMOJA WA MUNGU. Ilikuwa kutoka wakati huu ndo nilivutiwa sana na Uislamu. Hamu yangu ilizidi zaidi wakati nilisoma makala kuhusu Mungu iliyosema kuwa Mungu hakuwa na mpenzi wala mwana! Mafundisho haya yalifanana na dini yangu ya zamani, lakini kulikuwa na tofauti kubwa. Kutoka kwa imani za kimsingi ambazo tulifundishwa ni kwamba Kristo ni mwana wa MUNGU. Kwa hivyo, nilidhani kwamba ikiwa dini yangu ya zamani inatufundisha kwamba kuna Mungu mmoja tu na kwamba Yesu Kristo ni mwana wa Mungu, basi ingewezekana MUNGU kujizidisha kwa kuwa na mwana mwingine. Utaratibu huu ungeweza kuendelea mpaka kuwe na miungu mingi ambayo ingemsaidia MUNGU MMOJA katika kazi zake yeye kama MUNGU. Kwa sababu hiyo nilipoteza imani katika dini yangu ya zamani na nikaanza kudadisi zaidi kuhusu imani ya Kiislamu.
Mara nyingi nilitembelea tovuti ya www.islamreligion.com na kusoma baadhi ya makala kuhusu Uislamu. Nilistaajabika sana na njia ya sala za Waislamu. Ikawa dhahiri kwangu kwamba sala hizi zilikuwa takatifu zaidi, za kweli, za unyenyekevu, na za utiifu kwa Mwenyezi MUNGU, hasa wakati Waislamu wanapofanya ruku au kuinama (wanainama kuonyesha ishara ya heshima kwa Mola) na kisha sajdah au kusujudu. Kuna heshima kubwa katika sala za Waislamu. Nilijiuliza kwa nini katika dini yangu ya zamani, wakati wa sala tunasimama tu na kucheza cheza na mikono yetu, hii inapoteza umakini kabisa!
Akilini mwangu, nilianza kuona uzuri wa mafundisho ya Kiislamu. Nilifikiri kama tutamsujudia mtu inaonyesha heshima kubwa kwa mtu huyo, kwa nini tusimsujudie MWENYEZI MUNGU? Wakati bunduki inapoelekezwa kwetu, tunasujudu mbele ya mtu huyo kuomba rehema yake, kwa nini tusimsujudie Mwenyezi MUNGU ambaye anaweza kusababisha kifo chetu na ana uwezo wa kuweka roho zetu katika Jahannamu?
Nilitambua kwamba Uislamu ni dini inayowaita watu kumuabudu MUNGU kwa heshima kubwa kupitia ya dua za dhati, imani imara na ya nguvu.
Sababu nyingine ya kufuata Uislamu ni maisha ya Mtume Muhammad (huruma na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake). Nilistaajabika kuona jinsi Waislamu walivyomtunza Mtume wao (rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) hadi pumzi yake ya mwisho na jinsi Mtume alivyopigana kwa ajili ya UMOJA WA MUNGU na mapambano ya Waislamu kueneza ujumbe wa Mungu.
Huu ndio kiini cha Uislamu, tunaamini UMOJA WA MUNGU, na tunamheshimu Mtume wa Mwenyezi MUNGU: Mtume Muhammad (rehema na baraka za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake).
Sasa, kama Muislamu, matendo yangu yameimarishwa zaidi. Nimekuwa mwenye kumcha MUNGU na mwenye ufahamu wa MUNGU. Daima ninamkumbuka MUNGU kwa kuswali kila mara, namkumbuka Yeye katika kila kitu ninachofanya kwa njia ya dua na kumkumbuka kwa kutubu kwake wakati ninapofanya dhambi. Haya ndio mabadiliko mazuri ya maisha yangu. Ninafurahia dini yangu na ninafurahi sana kuwa nimekubali Uislamu kama dini yangu mpya. Ninafurahi sana kuwa sasa nimebadilisha dini kisheria na kuwa muislamu hapa nchini Ufilipino na sasa ninatumia jina langu la Kiislamu Afraz Saleem C. Bedico. Ninamshukuru mwendeshaji wa tovuti Samy kwa kunisaidia katika kutamka Shahadah (Ushuhuda wa Imani) na namshukuru mwendeshaji wa tovuti Tariq kwa kujibu maswali yangu wakati wa vikao vya moja kwa moja kupitia mtandaoni, na ninawashukuru www.Islamreligion.com kwa kuwa mwongozo kwa wale wasiojua njia sahihi.
ALHAMDULILLAH (Sifa zote na shukrani ziwe kwa Mwenyezi Mungu) kwa kuniongoza kwenye njia iliyo sawa.
Ongeza maoni